TFF yapokea barua ya Malalamiko ya Yanga dhidi ya Feisal

TFF yapokea barua ya Malalamiko ya Yanga dhidi ya Feisal

Headcorner

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2020
Posts
205
Reaction score
292
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (Kamati) limepokea malalamiko dhidi yako (FEISAL SALUM ABDALLAH) kutoka kwa Young Africans Sports Club (Klabu) kuhusu hali ya mkataba wako na Klabu.

Kwa barua hii, unaitwa kufika binafsi na mshauri wako wa kisheria mbele ya Kamati siku ya Jumatano, tarehe 4 Januari 2023 saa 10:00 katika Ofisi ya TFF, Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza malalamiko hayo.

CA94F7BE-F2D2-4D3E-8142-70A804E85442.jpeg
 
Barua imekaa kihuni kwasababu.
1. Kwa ulimwengu wa Sasa Tff ingempelekea malalamiko kamili na Kupewa muda wa kuyajibu kwa maandishi bila kumlazimisha kukutana nae.

2. Kesi za mikataba mikataba ingeangaliwa. Kuambiwa kipengere alichokiuka. Na Tff wangejua Kuna haja ya kujibu Kama Kuna hoja na Kama hakuna hoja wanamaliza wenyewe.

3. Huo mkutano Yanga wameshapanga hoja zao. Fei anaenda akiwa gizani. Nashauri kikao Cha siku hiyo kiwe kifupi Sana. Fei apewe malalamiko ya Yanga ayapitie na ayajibu baada ya kufanya upembuzi baada ya wiki.

Na tff wazingatie kuendesha kesi bila kuweka usumbufu usio na maana.
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (Kamati) limepokea malalamiko dhidi yako (FEISAL SALUM ABDALLAH) kutoka kwa Young Africans Sports Club (Klabu) kuhusu hali ya mkataba wako na Klabu.

Kwa barua hii, unaitwa kufika binafsi na mshauri wako wa kisheria mbele ya Kamati siku ya Jumatano, tarehe 4 Januari 2023 saa 10:00 katika Ofisi ya TFF, Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza malalamiko hayo.
Nimesema jana hapa. Yanga wameumizwa sana na hili jambo, ni kama bado wamepigwa na butwaa. Hawajui hata hatma yao hasa katika mashindano ya Afrika itakuwaje bila huyu dogo kuwepo.

Cha msingi, waachane naye, waimarishe timu yao ya wanasheria na watoe mikataba stahiki kwa wachezaji wao. Yanga inaharibiwa na siasa na kujiweka karibu na wanasiasa, hili litaendelea kuwasumbua sana katika kujenga club ya kisasa.
 
Yanga waaache Roho mbaya na Chuki za kipumbavu. Kijana kawatumikia kwa Moyo wote, Kitambaa cha Unahodha kavaa kwa adabu zote. Leo kaaamua kuyasaka maisha Nje ya Nchi mnamletea Giza na Uchawi wa kijinga. Kweli hii mijitu akili zao ni nyeusi nyeusi sana fooolish sana
 
Kwa nini wame release mawasiliano ya mtu binafsi. Hii kwangu naona haijakaa vizuri
 
Back
Top Bottom