Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
Mkuu, nakushangaa kwa haya unayoongea. Sipendi nirejee sakata la Morrison na ushahidi wa wazi jinsi TFF ilivyohusika kuhujumu mfumo wa usajili. SIPENDI KUBISHANA MRADI TUNAVUTIA KILA MTU UPANDE WAKE.Mkuu upande uliosimama wewe ndio upande unaotoa hoja za kishabiki na sio mpira
Club kubwa haiwezi kuendeshwa kihuni kama vile eti kwakua tu huwezi kubali kila kitu.
Kubisha ni mwanzo wa kuruhusu maarifa mapya lakini sio kila ubishi unatija
Nakupa mfano swala la mkataba wa GSM walioingia na TFF uliona namna Club ya Simba ilivyosimamia msimamo wake ambao ulikuwa supported na sheria mpaka TFF wenyewe wakagundua wamefanya makosa?
Niambie katika yale madai yenu ya kuilaumu TFF ni wapi mlikuwa na hoja zaidi ya malalamiko yasio na tija??
Jibu jepesi kwako ni hili, soka la Tanzania sote tunalijua. Ushawishi wa Simba na Yanga TFF sote tunajua. Hoja unayilalamikia wewe ni ya ufinyu wa uelewa. Yanga wameandika malalamiko yao rasmi kwa CHOMBO KINACHOHUSIKA KUSIKILIZA MALALAMIKO HAYO, wewe unapinga.
Swali kwako: ungetaka wapeleke wapi malalamiko hayo kama wanadhani mwajiriwa wao amekiuka mkataba wake?
Swali jingine: unafahamu kuwa ili kufika CAF na FIFA ni lazima shauri lako kwanza lisikilizwe na chama cha soka cha nchi husika ambaye ndiye msimamizi wa mikataba yote ya wachezaji wa nchi husika?