TFF yapokea barua ya Malalamiko ya Yanga dhidi ya Feisal

Mkuu, nakushangaa kwa haya unayoongea. Sipendi nirejee sakata la Morrison na ushahidi wa wazi jinsi TFF ilivyohusika kuhujumu mfumo wa usajili. SIPENDI KUBISHANA MRADI TUNAVUTIA KILA MTU UPANDE WAKE.

Jibu jepesi kwako ni hili, soka la Tanzania sote tunalijua. Ushawishi wa Simba na Yanga TFF sote tunajua. Hoja unayilalamikia wewe ni ya ufinyu wa uelewa. Yanga wameandika malalamiko yao rasmi kwa CHOMBO KINACHOHUSIKA KUSIKILIZA MALALAMIKO HAYO, wewe unapinga.

Swali kwako: ungetaka wapeleke wapi malalamiko hayo kama wanadhani mwajiriwa wao amekiuka mkataba wake?

Swali jingine: unafahamu kuwa ili kufika CAF na FIFA ni lazima shauri lako kwanza lisikilizwe na chama cha soka cha nchi husika ambaye ndiye msimamizi wa mikataba yote ya wachezaji wa nchi husika?
 
Hiyo TFF iliyomlinda Hersi na Manara kwenye ile kesi yao ya kuropoka siku ya Mwananchi, mpaka leo wako kimya hawajalitolea maamuzi lile suala...
 
Sasa nyinyi utopolo si Amna Imani na tff nendeni uko mkapate aki au shida ni mwiko uko nyuma
Mbumbumbu FC, tunaanzia kwanza TFF ili asipotenda haki tuende mbele. Kama hamuelewi jambo si mumuulize Rage awaelewesheni. Mnajidhalilisha kwa hoja zenu mandazi
 
Haya unayo yasema uliyatoa wapi? kiongozi gani alitamka haya,?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Yanaanza maneno maneno ka yale ya Morisson kipindi kilee

Tuwekeeni mkataba wake na timu tuusome --- mikataba mingi ni ya siri
Naomba nioneshe mkataba uliowazi kati ya mchezaji & club anayochezea hapa bongo..!
 
[emoji23][emoji23][emoji2772]! Mashindano ya Africa unamtegemea Feisal? Acha masikhara mkuu.. Hapo viongozi wanaendeshwa kwa mihemko tu ya mashabiki ila Feisal hata akiondoka bado Yanga itabaki na ubora ule ule...! Feisal ni mashabiki / media tu ndio zinamjaza( Kuonekana mchezaji wa kiwango hicho) ila kiuhalisia ni mchezaji wa kawaida tu...
 
Ni mchezaji wa kawaida ni kweli ila alikuwa na umuhimu wake mkubwa pale Yanga.
 
Ni jambo zuri kukaa meza moja ili haki ipatikane kwa pande zote mbili. Ingekuwa Yanga ndiyo imevunja mkataba kama alivyofanya huyo Feisal; naamini kelele zingekuwa ni nyingi sana.

Hivyo sioni sababu ya watu kulalamika, na wakati huo mkataba uliingiwa kati ya Yanga na Feisal! Sasa nongwa iko wapi kwa mwajiri kumshtaki mwajiriwa wake kama ameona kuna mambo hayakobsawa kwenye mkata waliongia?


Ingekuwa Feisal ndiyo kaishtaki Yanga kwa kukiuka vipengele vya mkataba wao, mngekuwa upande wa Yanga, au bado mngeegemea kwa Feisal?
 
Hilo la Morrison bora umechagua kuliacha maana humo mliumbuliwa sana na usiihukumu TFF kwa hilo maana hatua ya mwisho swala hilo limeamuliwa na CAS

Na CAS ni chombo huru kilicho jui ya TFF otherwise uijumuishe nayo kama ni idara inayoichukia Yanga pia.

Hilo la Morrison limeisha...

Sijakataa Yanga kuandika malamiko kwa TFF

Naomba uelewe hilo kwanza

Mimi nahoji tu kivipi chombo hiki ambacho uongozi wa Yanga uliweka mashaka na kusema hauna imani na TFF hii?

Usinipe majibu kuwa huo ni utaratibu, kwasababu kuna mambo mengi ya kiutaratibu ambayo yapo kisheria na TFF iliwataka myafanye lakini mmekuwa mkipingana nayo kwa kusema hamna imani na TFF

Na mifano ipo

Nafahamu kuwa ili ufike CAF au FIFA ni lazima uwe umepita TFF

Namimi nakuuliza swali hapo

Unaelewa kuwa swala la Morrison lilianzia TFF huko huko ambapo hamna imani napo na liliamuliwa kuwa Yanga ndio wenye makosa na mwisho mkalipeleka CAS ambapo majibu yalikuja vile vile?
 
Mbumbumbu FC, tunaanzia kwanza TFF ili asipotenda haki tuende mbele. Kama hamuelewi jambo si mumuulize Rage awaelewesheni. Mnajidhalilisha kwa hoja zenu mandazi
Kwenda si mnawakataaga wanatuhujumu muende sasa
 
TFF Kwa kushirikiana na utopolo ni kama wamepanga kumkomoa feitoto ndio maana wamepanga tarehe ya karibu huku wakijua feitoto yupo nje ya nchi lakini wajiandae kupata pigo takatifu kwanza hata yanga wakishinda feitoto ataenda cad huku akiomba kibali fifa Cha kutafuta timu ya kuchezea kulinda kiwango chale wakati shauri lake linasikilizwa so ajabu akaibukia Simba
 
Sasa mimi swali langu ni moja,je kama yanga atashinda kesi hii na feisal akatakiwa kurudi yanga JE ATACHEZA KWA MOYO MMOJA AU NDO ATAJIVUNJA KILA MECHI??.

Nadhani ni heri kumuacha mtu mzima akishaamua aende zake.

Huwezi kumlazimisha mtu mzima,akiamua lake ndo kashaamua hivyo.
 
Utopolo wakishindwa hii kesi watakimbilia kumroga kijana wa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…