The Daily Telegraph: Iran ilipiga kambi 5 za kijeshi za Israel

Vita ishaisha, tuendelee na mishe zetu...
 
Kazi ipo.

Hivi kwanini Israel na U.S waliomba ceasefire haraka baada siku chache tu please kwa anayejua sababu ?

Na kwa nini Israel imekuwa mgumu kukubali ceasefire hapo Gaza pamoja hata akiwa ana bembelezwa ?
Imagine 😁
 
Iran ilijitutumua kiasi chake japo pia ilishindwa kabisa kulinda anga lake.
 
😁😁😁😁

Acha uongo haujui kitu , Iran aombe cease fire kwani yeye ndiye aliyeanzisha vita !? Iran hakuwa na mpango wote na hiyo vita Ilimlazimu kujibu mashambulizi kwakuwa alikuwa amevamiwa akaona kukaa kimya ni unyonge

So inakuwaje Sasa nchi ambayo sio iliyo anzisha vita iombe kusimamishwa kwa vita hiyo !?

Unatuona hatuna akili sindio !?


Israel ndio walio omba Pooh maana hakutaraji kukutana na mkong'oto kama ule 😁😁
 
Iran ilijitutumua kiasi chake japo pia ilishindwa kabisa kulinda anga lake.
Iran haikujitutumua,Bali ilijibu kulingana na ilivyoshambuliwa.
Iran ni nchi Tajiri lakini imeishi kwenye vikwazo kwa miaka mingi.Ingekua huru nadhani ingeweza kununua ADS za kutosha.
China inatengeneza silaha zake na nyingine inanunua kutoka Russia.
Iran Imejaribu kujitengenezea silaha zake na imeweza.
Haikuweza kununua ADS za kutosha kwa sababu ya vikwazo nadhani.
Lkn hata hivyo ilisimama peke yake wakati Israel ilisimama na Big USA some westerners na some Arabs kuyatungua makombora mengi ya Iran.
Kumbuka Israel Kuna
ADS za Israel na nyingine zile zilizotengenezwa USA.
Kama Israel aliweza peke yake ni kwa Nini Ile ndege B2 Stealth ya USA ilotoka USA kujua kupiga Iran?
 
Pro western akili zao zipo brainwashed usijile
 
We jamaa mbona huwa unapenda sana kupotosha!?
Iran hakuomba ceasefire hata mara Moja.
Hiyo kauli uliyosema ya kuwa Iran alisema angeacha kurusha makombora kama Israel atasitisha mapigano aliisema Abbas Araghchi waziri wa mambo ya nje wa Iran akijibu kauli za EU members na USA walipomwambia aje mezani wazungumze.
Alisema kuwa hakuna mazungumzo na hakuna amani hadi Israel iache kushambulia na sisi tutaacha mashambulizi.
Na kama haujui katika Baraza la mapinduzi Iran kilitokea mgawanyiko,nusu wakisema vita isimame nusu wakisema hakuna kusimamisha vita hata kama kutaombwa ceasefire.
Aliyeomba ceasefire ni Israel kwa kumtumia USA.
Muwe mnasoma taarifa vizuri sio kutudanganya humu ndani.
After that USA ndiye aliyeishinikiza hiyo ceasefire.
 
Na hapo ADS za Iran Khordak na Bavar zimeonesha kuwa na ufanisi kuliko Iron dome ya Israel.
Licha ya mashambulizi makubwa ila somehow wame contain yale mashambulizi,maana ndege zaidi ya mia kukushambulia kama ni dhaifu kabisa kwa Air defense aisee nchi yako INAGEUKA kifusi.
Tuisifu Bavar -373 air defense system kwa hilo.
 
2006 kwenye vita ya Hizbullah na Israel, Israel alipoteza askari wengi na vifaa vingi viliharibiwa akaretrieve . Israel ilipoibukia Hezebulah bada ya miaka kadhaa, tuliona kilichofanyika. Tutegemee raundi ya pili inayokuja, Iran kufinywa sana. Hasara aliyopata Israeli ilikuwa calculated,na ndo maana Netanyahu kasema lengo lilitimia.
 
Enyi wajukuu wa Mudi ni nani aliewaroga? Tunaomba picha za uharibifu wa kambi zilizoharibiwa!!
 
Hizbollah bado wako imara,kitu ambacho mmekisahau France na US waliishinikiza serikali kuu ya Lebanon wawashurutishe Hizbollah wasaini makubaliano ya kusitishwa vita.
Ila Hizbollah bado wapo na uimara ule ule,pia fahamu Hizbollah ni kundi lenye limited fire power.
Hasara alizopata Israel sio ndogo hata kidogo,majengo tu ya kiraia more than $20 billions inatakiwa kuyakarabati.
Hujagusa kambi za jeshi, research centres na jengo la uwekezaji pamoja na jengo la Microsoft yaliyolipuliwa.
Iran sio sawa na Hizbollah,Iran ni taifa kamili lenye nguvu kamili ya kijeshi,ili Israel kumpiga Iran kama unavyodai anatakiwa aungwe mkono na USA mwanzo mwisho sio kwa kubahatisha.
Hivyo hivyo Israel inavyojiandaa na Iran imejiandaa mara dufu,wiki ilopita kapokea Air defense system batteries kutoka China,na yupo katika mazungumzo ya kupokea ndege za J10-c kutoka China.
 
Mkuu hivi unapata wapi muda wa kuwajibu wapumbavu!

Ni bora ungemuachia licomment lake ambalo limekosa like hata 1.
 
Kama Iran ikipata/nunua silaha mfano: ADS na latest jet fighters kutoka Uchina, basi hapo Iran kila kitu kitakuwa balabala,hivyo Israel itafikilia mara mbili mbili kabla haija ichokoza tena Iran - Israel ikijifanya tena kichwa ngumu itachakazwa kweli kweli this time around na asitegemee kwamba Trump atasumbuwa kichwa chake kumtetea tena binadamu ambaye simsikivu na mwenye kiburi.
 
Iran ameshapokea ADs kutoka China Bado ndege tu.
 
Iran ameshapokea ADs kutoka China Bado ndege tu.
Kama ndiyo hivyo basi hapo Iran itakuwa imefanya jambo la maana sana sana, nikiona au kusoma jinsi Israel inavyo tumia ndege zake za vita kuchinja mamia ya mamia ya Wapalestina almost kila siku, wanapiga mabomu makazi yao si hilo tu, hivi sasa wanafanya operation ya kuwahamisha kinguvu Wapalestina na kuwapeleka kwenye makambi ambayo hayaeleweki vizuri, huku Trump anakaa kimya tu hawajali Wapalestina - kuna wakati nadhani mwaka jana Trump na Natenyahu walikuwa na mpango wa kuwahamisha Wapalestina wote kwenda nchi jinari lakini Dunia ikamshtukia na Waarabu karibu wote wakapiga vikali mpago wake ovu, kumbe Trump alikuwa anataka aridhi yote ya Gaza waitumie yeye na Natenyahu kujenga Golf Courses, Kumbi za starehe na Beach za Watalii, watu wa ajabu sana hawa!!
 
Kwa mfuatiliaji ambaye hayuko biased iko wazi sana ndani ya siku nne tu Iran ilishatepeta tepetepe dhoof lihali chali mlalo wa mende na ilishaanza kuomba ceasefire tena kwa nguvu mnoo maana walishaona hiyo vita kamwe hawatoimudu
 
Inawezekanaje unasema taarifa inasema miundombinu ya jeshi haikuguswa wakati heading tu inasema kambi tano zimepigwa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…