The last days of Prof. Kighoma Ali Malima, July/August 1995

Siku hizi nikiona maandishi yako wala sihangaiki kusoma. Najua kuna chuki kali kwa Nyerere na mfumo Kristo na jinsi ulivyoonea Waislamu. Hii ndiyo constant pekee katika maandishi yako mengi (hapo juu). Cha ajabu hata hutoi any suggestions au masuluhisho ya kuwakwamua waislamu wenzio. OK, Prof. Malima aliuawa na Nyerere na mfumo Kristo then what? Tufanye nini sasa hasa ukizingatia kuwa Nyerere mwenyewe naye alishakufa? Unataka Waislamu wafanye nini? Na Wagalatia (makafiri) nao wafanye nini? UNATAKA NINI?

Look. Uislamu wa kweli naujua na nimefaidika nao sana. Na mimi ni MTETEZI mkuu wa Uislamu hasa katika jamii ambazo hazina imani nao. Pale Stanford University niligombana na watu wengi nikitetea Uislamu kuwa ni dini ya amani na upendo kwa sababu wema huu na upendo huu wa Waislamu nimeuona na sijasimuliwa.

Tatizo la uislamu kwa sasa (inawezekana na dini zingine katika vipindi tofauti) ni kutekwa na watu wachache na kuanza kutumiwa kwa maslahi binafsi. Kila Mwislamu wa kweli anakubali kuwa uislamu unaohubiriwa na Al Qaeda, ISIS, Boko Haram, Al Shabaab na magaidi wengine siyo uislamu wa kweli. Uislamu wa kuua wanawake na watoto; na watu wengine wasio na hatia.

Nasikitika kusema kwamba hata wewe unaingia katika upande huu. Juhudi zako hizi za kujaribu tena bila kuchoka kueneza chuki non stop siamini kama ndiyo uislamu wa kweli. Unautumia uislamu tu kwa faida zako za kibinadamu na hata ujaribu vipi kujificha katika uanahistoria na usomi watu makini bado tunaweza kuona unachojaribu kufanya. Na kama nilivyosema acha tu waendelee kukuchekea na kukusifia eti unafanya investigative history wataona utakakowafikisha siku moja.

Jaribu sana angalau kutoa mwongozo. Ndiyo Waislamu wameonewa sana na Nyerere na Mkapa (na wakafaidika sana na Mwinyi na Mrisho), sasa nini kifanyike? Hapa chini nakuwekea angalizo kuhusu matokeo mabovu ya kidato cha nne katika seminari nyingi za Kiislamu. Toa angalau mwongozo jinsi seminari hizi zinavyoweza kuboresha elimu na kuhakikisha vijana wake wanafaulu vizuri. Hii itasaidia zaidi kuwainua Waislamu mara bilioni kuliko kuwaambia tu Kigoma Malima wetu aliuawa na Nyerere halafu huwaambii wafanye nini. Allah Akufungue moyo wako uhame kabisa kutoka upande wa giza ili ukawe kurunzi itakayowaonyesha njia Waislamu wapendwa wa Tanzania hasa katika kipindi hiki ambacho uislamu wa kweli umetekwa na magaidi. Molla na Akusaidie na hata usiponisikia tena KAMWE usijivike kiburi cha usomi na kuusahau ushauri huu wa kibinadamu na kizalendo. Maisha ya watu wengi sana yako mikononi mwako kupitia kalamu yako hiyo inayotema sumu kali bila kuchoka.
 
Shimba...
Unasema ukiona maandishi yangu huangaiki kuyasoma...
Husemi kweli.

Ungekuwa husomi usingenijibu hapa.
Ukishanisoma mara moja huwa shida kuyatambuka maandishi yangu.

Huu ndiyo ukweli.
Mimi sina chuki na yoyote wala sina chuki na Nyerere.

Nilichofanya na hiki ndicho bila shaka ndicho kinachokuchoma ni
kuwa nimeandika upya historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Historia ambayo kwa sasa Nyerere anakuja na picha nyingine si ile
iliyozoeleka kuwa yeye alianzisha TANU nk. nk.

Nimewaleta Waislam waliofutwa kwa kukusudia katika historia na
leo kizazi hiki kimejua ukweli.

Hili ndilo linalowakera wengi sana.

Hayo mengine sioni kama kuna haja ya kujibu ila nitakupa sababu
za shule za Misheni kuwa zinafanya vizuri kuliko shule za Kiislam.

Nadhani unajua kuwa Kanisa linapata mabilioni kila mwaka kupitia
Memorandum of Understanding kati ya serikali na Kanisa.

Fedha hizi zinatumika kuliimarisha Kanisa, hosptali za Kanisa na shule
za Kanisa.

Shule za Kanisa hazina shida ya kitu chochote kuanzia kuajiri walimu
wazuri na kuwalipa vizuri, majengo hadi chakula kwa wanafunzi.

Si haki kabisa shule zenye upendeleo kama huu ukazifananisha na
shule zetu ambazo zinaendeshwa kwa jasho letu sisi wenyewe Waislam
wengi tukiwa masikini.

Nadhani unajua kuwa kwa miaka mingi Waislam wameitahadharisha
serikali kuhusu dhulma ifanywayo na Wizara ya Elimu dhidi ya vijana
wa Kiislam.

Ipo taarifa maaarufu ya mwaka wa 1981 iliyotayarishwa na Warsha
kuhusu jambo hili na taarifa hii ilisambazwa kwa Waislam wa nchi nzima.

Hiki ni kisa kirefu kama nitakueleza vipi Warsha iliandamwa kwa kueleza
dhulma hii na baadhi ya viongozi wake wakafukuzwa nchini na wengine
kupigwa marufuku kuongoza taasisi yoyote ya Kiislam.

Haya yote kwa kuwa walisema kweli.

Naamini unajua kuwa hata Prof. Malima alipochaguliwa kuwa waziri wa
kwanza Muislam kuongoza Wizara ya Elimu mambo aliyoyakuta pale
yalimtisha na aliandika waraka kwa rais kuhusu kile alichoshuhudia.

Ilikuwa mwiko katika utawala wa Nyerere Muislam kuongoza Wizara ya
Elimu.

Matokeo ya waraka ule Prof. Malima aliondolewa katika wizara hiyo.

Yawezekama ukafahamu kuwa miaka miwili tu iliyopita Waislam walifanya
maandamano makubwa yaliyoongozwa na Sheikh Ponda dhidi ya NECTA
na Mkurugenzi wake Dr. Joyce Ndalichako wakimtuhumu kwa kuhujumu
wanafunzi wa Kiislam.

Huyu Ndalichako leo ndiyo Waziri wa Elimu.

Haya yote niliyoeleza si mambo ya kufikirika ni mambo ambayo tunayo
nchini kwetu.

Tatizo serikali inaogopa kuyajadili kwa uwazi.
 
Nimeshakuaga Mpendwa na yote niliyotaka kukwambia nimeshayasema. Roho na dhamira yangu ni nyeupe na najihisi kuwa nimetimiza wajibu wangu. Ukiweza rudia tena kusoma comment yangu hapo juu tena na tena na tena na tena na tena na tena na te...Daima nitaendelea kupigania heshima ya Uislamu wa kweli na sitasita kusimama kidete kupinga watu hatari kama wewe mnaojificha katika dini hii tukufu ili kutimiza malengo yenu dhaifu ya kibinadamu. Na kama nilivyosema acha tu wakuchekee na kukuachia mpaka ufanikiwe kuuwasha huo moto unaohangaika kuuwasha usiku na mchana. Kila la Kheri. Allah Akusaidie!
 

Shimba...
Ni vigumu sana kunitambuka...
Wengi wamejaribu wameshindwa.
 
Hiki kizee kinafiki kimejaa uzandiki na udini
 
Umepewa link za Mada au maandiko aliyoandika ambayo ni ya Wakristo, bado unaanza kulalama, acha hizo!
 

Hakuna hata mmoja atakayeweza kutetea, kwa sababu kwa kiwango kikubwa maandishi ya Mzee MS yanafacts. Wengi watatukana na kubwabwaja, hawana ujasiri wa kujibu hoja za mzee MS mstari kwa mstari neno kwa neno wakibainisha hapa mzee Uko sahihi, hapa UMEKOSEA. Wengi wataishia kutukana tu, kutokwa na mapovu nk. Hakuna hata mmoja atakuja na hoja za kukana kile alichokisema Mzee MS kuhusu ziara za Garang, Sudenese Delegates, Matamshi ya Deceased Rev C Mtikila(R.I.P)!

Kwa Great Thinkers nilitarajia hayo aliyoyasema Mzee Said yangekanushwa au kufafanuliwa kwa hoja na facts. Ila kuishia kumtukana na kutokwa tu na povu, kunaashiria andiko la MS ni kweli tupu. Mwenye Ufafanuz wa kupinga alichosema Mzew MS aje ili tupime ukweli
 

Ni povu tu hilo umeandika. Weka facts wa hayo madai yako. Lakini kanusha kama Mfumo wa kutumia Namba haukuongeza haki katika ufaulu!
 
Umepewa link za Mada au maandiko aliyoandika ambayo ni ya Wakristo, bado unaanza kulalama, acha hizo!
Sijalalama mkuu,hizo link ukizifungua hamna jipya nimezifungua sana kwenye mabandiko mengine humu ni yaleyale ya siku zote so kusema nizifungue tena ni kupoteza muda na kuchosha akili ndo mana nikahitimisha kumshauri mzee wetu kwamba,kwa sifa ya utunzi aliyonayo ingependeza zaidi kama akajikita kuandika vitabu viakavyosomwa na jamii nzima ya wa-Tanzania sio kama hivi anavyopigania kutugawa,huyu ni hazina kwa taifa but halitendei haki taifa letu,kwamba anaitumia kalamu yake vibaya.
 
Mzee Mohammed Said kwa maandishi haya na kazi nyingi ulizofanya ulipaswa kuwa professor kwenye moja ya vyuo vyeti hasa vile vinavyosemesha historia. Why delaying with these rich materials? Distribute to others especially young generation.
 
Fact: CHUO KIKUU CHA KIISALAM MOROGORO LINGANISHA NA ST. AUGUSTINE, SEMINARY ZA KIISALAM LINGANISHA NA SEMINARY ZA KIKATOLIKI HALAFU UKAWAAMBIE WANAFIKI WENZIO WAPI ELIMU NI BORA KWA WALA NGURUWE AU WAPIGA MADUFU BAADA YA HAPO SITARAJII KUKUONA UKIBWABWAJA HAPA TENA KWAMBA UNAONEWA.
 
Duuu hatari maoni yako. Taratibu mkuu
 
Shimba...
Ni vigumu sana kunitambuka...
Wengi wamejaribu wameshindwa.
Allah siku moja "Atakutambuka" tu. Wewe wala usiwe na wasiwasi. Na ikibidi jifunge hata mabomu kama wenzako wanavyofanya uende Butiama kwenye kaburi la Mwalimu "ukajitambuke" huko!
 
 
Shimba...
Hayo usemayo ni kweli tupu wala hakuna anaeweza kupinga.
Na ungeweza ukaeleza hayo yote kiungwana bila matusi.

Lakini mafanikio hayo ya shule hizo yanaelezeka bila wasiwasi.

Kanisa linapokea mabilioni ya fedha kutoka serikalini kupitia ile
Memorandum of Understanding (MoU) kati yake na serikali.

Fedha hizi Kanisa inazitumia kuimarisha Kanisa lenyewe, Hospitali
za Kanisa na Shule za Kanisa.

Katika hali kama hii shule za Misheni hazina upungufu wa chochote.
Kuanzia majengo hadi kuajiri walimu wenye ujuzi na kuwalipa ujira
mzuri nk. nk.

Huwezi kufananisha shule hizi na shule za Kiislam ambazo ni yatima.

Mfano huu ni sawa ya kumfananisha mtu mwenye afya na mgonjwa
wa utapiamlo.
 
Ukitazama kamusi kupata tafsiri ya seminari utagundua waislamu waliparamia kutumia neno hilo bila kutafakari. Walifikiri kuita tu seminari basi ni kufaulu.
Ngalikivembu,
Nakuomba usome hayo ninayokuwekea hapo chini ni kutoka
mswada wa kitabu changu (hakijachapwa):

''Warsha turned four schools built by the EAMWS which were under BAKWATA into Muslim seminaries that from there on the schools would only accept Muslims. Within a short period of time, discipline was restored into the schools and it was compulsory for students to observe prayers and for girls to dress in hijab. Mussa Mdidi and Burhani Mtengwa were fully involved in this project. Warsha conducted a social research project which no Muslim organisation had attempted before. It commissioned its educationists to write a research paper to show why Muslim students were lagging behind in education.

When these s findings were made public and distributed to throughout the country it came as a shock to Muslims and the government. For the first time it was revealed that there was a system in the Ministry of Education supported by Christian functionaries which was discriminatory to Muslim youths, purposely barring them from institutions of higher learning and the president of the country Julius Nyerere and the Catholic Church was not unconnected in this plot. Such accusations and disclosure, particularly coming from Muslims, threatened national unity. The government did not want to find out whether those findings on education were correct or not. Its interest was to know the brains behind Warsha isolate them from Muslims and then persecute them. The government was unprepared for such revelations and was worried by the direction which BAKWATA was taking. BAKWATA was now serving the cause of Islam. This was not what Nyerere had bargained for when he subverted the EAMWS and helped to found BAKWATA. Sheikh Mohamed Ali as secretary of BAKWATA was taken to task for allowing the organisations to be hijacked by were perceived to be hot headed youths. Warsha were accused of being anti-government, anti Christian and perpetrating animosity between Muslims and Christians through their writings. President Nyerere ordered Aboud Jumbe the Vice President to close down the Muslim seminaries.


A meeting between Aboud Jumbe and BAKWATA was held at Jumbe’s official residence at Laibon Road. In attendance were Rashid Mfaume Kawawa, Adam Nasibu, Sheikh Mohamed Ali and Sheikh Abbas Makbul a representative of Darul Iftar. The stand of Sheikh Mohamed Ali was that if those Muslim seminaries have to be closed then the decision to take that step should be laid upon the government. This was a difficult step to be taken by the government as such an act would provoke Muslims. The meeting left the decision to close the seminaries upon BAKWATA. [2] BAKWATA took a unilateral decision and reverted the schools back to its original state. Warsha not agreeing to BAKWATA’s decision called a meeting of all Muslims to discuss the problem. What Warsha was strategising was to draw Nyerere and his government into direct conflict with Muslims. The government saw through Warsha’s plot and the Christian lobby used its powers and a crisis was fomented. The government issued a directive to reinstate the schools taken over by Warsha to their former secular status, that is, any Tanzania irrespective of faith should have access to them. The Christian lobby through the state- radio issued a warning that the meeting called by Warsha was illegal and any Muslim attending that meeting would be arrested. For effectiveness this announcement was read by the Director of Radio Tanzania, [3] David Wakati. The government accused Warsha of trying to divide the country along religious lines. The government saw the two Muslim seminaries which were established less than a year as divisive but turned a blind eye to 19 Christian seminaries which were in existence for almost a hundred years.



[1] Muslim Writers’ Workshop, “The Importance of Establishing Islamic Seminaries,” 21 December, 1981.

[2] See article by Burhani Mtengwa, ‘Mikutano ya BAKWATA ni Njama za Kuhujumu Uislam” in Mizani 18-31 Januari, 1991.

[3] In the EAMWS crisis of 1968 the state owned radio was used very effectively as a propaganda tool against Muslims.
 
Allah siku moja "Atakutambuka" tu. Wewe wala usiwe na wasiwasi. Na ikibidi jifunge hata mabomu kama wenzako wanavyofanya uende Butiama kwenye kaburi la Mwalimu "ukajitambuke" huko!
Shimba,
Tunaweza tukajadiliana kiungwana hapana haja ya kutukanana.
Huu ni mjadala tu kila mtu anajaribu kueleza kile anachokijua.

Haya ya Nyerere na kujifunga mabomu inaonyesha umekasirika.

Ukinisoma mimi mara moja huwezi kuona nilichoandika ukapita
wima.
 
Mzee Mohammed Said kwa maandishi haya na kazi nyingi ulizofanya ulipaswa kuwa professor kwenye moja ya vyuo vyeti hasa vile vinavyosemesha historia. Why delaying with these rich materials? Distribute to others especially young generation.
Ngalikivembu,
Mie bado mwanafunzi.

JF imenikutanisha na watu wengi sana na nimejifunza mengi kutoka kwenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…