The New York Times lasambaza uongo Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze, au uongo tukanushe?

Na unacho takiwa kutambua ni kwamba ipo siku utakuja kusimamishwa mbele ya aliye kuumba, na utatakiwa kuutolea ufafanuzi huu unafiki unao andika humu kila siku.

Njaa isikufanye ukajitoa akili,usipende kuishi maisha ya kujipendekeza kiasi cha kujivua utu wako jamani.
 
Nakumbuka kuna chapisho ulitoa kudeclare umeachana na journalism na kujiunga na siasa. Sasa hivi kila unachopost nadhani kina mrengo wa kisiasa zaidi.
 
Hakuna uwongo hapo, walichoandika ni ukweli mtupu. Kituo nilichopigia kura mimi wakala wa Chadema alizuiwa katakata kuingia ndani, hii nimeona kwa macho yangu kabisa sijaambiwa na mtu! - Sasa uchaguzi gani huo!
Huyu mpuuzi usimsikilize, maana ya Mayalla maanake ni njaa acha atangulize njaa zake kwanza kusubiri uteuzi, yupo tayari kuua hata wanae ili yeye apate mkate.
 
Kwakweli najuta kusoma huu walaka/Uzi wako kwasababu nimejikuta nakushangaa kama na wewe ndio unatafuta Uteuzi kwa nguvu kiasi hichi,

SMS na Call zilikuwa zinasumbua sana tena sana kwa taarifa yako mawasiliano yalikuwa ya shida na kwasababu ni Haki yetu kupata Mawasiliano ndio maana watu walipaza sauti kudai hiyo HAKI....

ukijipa kazi ya Kutetea taasisi zilizokuwa zinatakiwa kutuhudumia unakuwa UMEJIONGOZA VIBAYA na nakuahidi inakushushia heshima yako sana kwasababu wao wameomba radhi na wanasema maneno yanayopingana na haya yako.
 
Mkuu achana na huyu mchumia tumbo
 
Wameandika KWELI TUPU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…