The New York Times lasambaza uongo Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze, au uongo tukanushe?

The New York Times lasambaza uongo Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze, au uongo tukanushe?

Ulishapuuzwa na almost 85% na members wa JF wenye kuutumia vema ubongo wao hasa katika mambo ya kidiplomasia na masuala ya chaguzi zilizopita

Ingekupendeza nakala kama hizi ziandike katika magazeti ya serikali, uhuru au Tanzanite kwa mbumbumbu wasio-evaluate mambo.

Endelea kupambania kombe huenda ukamtoa Hassani katika kiti!
 
Mmetiwa uoga wa kuisema kweli nchini kwenu, mmekuwa vipofu na pengine kwa maksudi ili kufurahisha mamlaka muambulie ‘some favor’ kwenye mishe zenu.

Deep down mioyoni mwenu mnashuhudia kweli ilivyo, na inawatafuna kweli kweli.

Acheni waliohuru wapaze sauti, wasioogopa au walio kwenye mazingira salama.

Paskali sio mmoja wa wale wanaoweza kunena mema kwa ajili ya Taifa letu, not anymore!

I’ve said a million times.
 
Ukiona mjuzi wa sheria uchwala Yuko huko, makala zote zinazoihusu TANZANIA ujue ni yeye!!

Anashobokea wazungu kuwauzia nchi yetu Kwa bei ya uchochezi na uwongo!!

Huyu ni Kati ya wanasiasa ambao watakufa masikini sana na ambao mpaka mauti inawakuta, hawajui kuridhika, kazi Yao ni kutafuta madaraka Kwa namna yoyote Ile!

Ni Kati ya wanasiasa ambao shetani amewekeza maroho ya mauti paspo kujali ni Nani atakaye Kufa mbele Yao! Wanasiasa ambao hudhani, ikiwa nchi yake itavamiwa na majeshi ya kigeni, kisha kuachwa raia wakiuwana wao Kwa wao, eti husema mauwaji hayo wao hawahusiki!

Tanzania na imlaani mtu huyo, Amina
 
Prof. Kabudi kwa kasi ile ile atarekebisha mambo.
Hilo ni gazeti wameandika wala lisitutishe.

Uchaguzi umeisha na hakuna uchaguzi mwingine mpaka 2025.Na bahati mbaya kwa ukosefu wa pesa uliopo sidhani kama kuna chama kitakwenda mahakamani kupinga hata udiwani.
 
Hakuna uwongo hapo, walichoandika ni ukweli mtupu. Kituo nilichopigia kura mimi wakala wa Chadema alizuiwa katakata kuingia ndani, hii nimeona kwa macho yangu kabisa sijaambiwa na mtu! - Sasa uchaguzi gani huo!
Huyu Pascal tunajua anajitambua Ila kwa vile ni Kipindi cha Kutafuta Ulaji ni muda muafaka pia Kwake Kujionyesha. Uchaguzi wote tulikuwepo na Tumeona so yeye Kujipendekeza Kwake asituletee hapa.

Ni Bora Aelekee Kwa Wenye Mamlaka akawaeleze Anataka Nini Wampe ili Asituvuruge. Uchaguzi Umekwisha Mshindi alishapatikana ya Nini Kutukumbushia Machungu tuliyoyashuhudia.

Pathetic
 
Hilo gazeti linapaswa lishugulikie uchaguzi wa kwao na pia waeleze kwanini kwao Corona inaongezeka wakati huku kwetu pamoja na kwamba ni dunia ya tatu pamoja na kutokuwepo kwa takwimu bado maisha yanaendelea
 
NI KWELI MNYAMAZE,MKIJIBU MTAZIDI KUJIVUA NGUO..
Huu hamuwezi kuita uchaguzi.View attachment 1625388View attachment 1625390

Screenshot_20201028-191013.jpg
 
Simchukii Magufuli ila ninapenda haki. Uchaguzi ungekuwa huru na haki Magufuli asingekua rais wetu.
Muongo mkubwa wewe!

Yeye mwenyewe alikuja huku akijua hawezi kushinda na ndio Maana alikata tiketi ya kurudi kwao kabla hata ya kupanda pipa kuja Tz,

Sema kilichokuwa kimemleta kimepuuzwa na Watanzania wengi ukiwemo na wewe
 
Kwani SMS zenye jina Lissu, Mbowe, Zitto Kabwe, Lipumba na Maalimu Seif nilikuwa zinaenda?

Wiki moja kabla tulizuliwa ,kwa mfano Mimi jina langu linakaribiana na moja ya majina hapo lakini nilipata tabu hadi kupokea hela kwa emoney
 
Back
Top Bottom