PostGE2025 THRDC Yapendekeza Oktoba 29 kuwa siku ya kitaifa ya kumbukizi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kituo cha Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kimependekeza Oktoba 29 ya kila mwaka iwe Siku ya Kitaifa ya Kumbukizi ya matukio ya Oktoba 2025, ili kuwakumbuka wahanga na kuweka mikakati ya kuzuia kujirudia kwa vifo, majeruhi na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Katika taarifa yake iliyotolewa Oktoba 23, 2026, THRDC imesema siku hiyo inapaswa kuwa zaidi ya maombolezo kwa kuwa fursa ya kutafuta ukweli, kutenda haki, kuimarisha uwajibikaji na kujenga mshikamano wa kitaifa.

Kituo hicho kimesisitiza kuwa kumbukizi hiyo inapaswa kuongozwa na falsafa ya “Yasijirudie Tena” (Never Again), huku juhudi za maridhiano zikienda sambamba na uchunguzi wa kuaminika na uwajibikaji pale makosa yatakapothibitishwa.

Aidha, THRDC imependekeza kutathminiwa kwa mifumo ya ulinzi wa raia na uwajibikaji wa vyombo vya usalama, pamoja na kuhifadhi kumbukumbu za matukio hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Kituo hicho kimetolea mfano Rwanda, ambayo huadhimisha kumbukizi ya mauaji ya kimbari kuanzia Aprili 7, na Afrika Kusini, ambayo huadhimisha Siku ya Haki za Binadamu Machi 21, inayohusishwa na mauaji ya Sharpeville ya mwaka 1960.

THRDC imependekeza kumbukizi ya kwanza kufanyika Oktoba 29, 2026, kwa kushirikisha familia za wahanga, taasisi za umma, viongozi wa dini, asasi za kiraia na wananchi katika ngazi za kitaifa, mikoa na wilaya.

Shughuli zinazopendekezwa ni pamoja na ibada na dakika za ukimya kuwaenzi waliofariki, ushuhuda wa hiari wa familia za wahanga, kongamano kuhusu ukweli na haki, pamoja na elimu kwa vijana kuhusu haki za binadamu na amani.

Pia, kituo hicho kinapendekeza kuanzishwa kwa utaratibu wa kuhifadhi kumbukumbu za matukio hayo na hatimaye kujenga makumbusho rasmi, huku tathmini ya kila mwaka ikifanyika kuhusu utekelezaji wa hatua za kuzuia kujirudia kwa matukio kama hayo.

Kaulimbiu iliyopendekezwa ni na kituo hicho ni "Kumbukizi, Ukweli, Haki, Uwajibikaji na Uponyaji, Kamwe Yasijirudie Tena.
Chanzo : Jambo tv

======

WITO WA KITAIFA: TAREHE 29 OKTOBA KUTENGWA KUWA SIKU YA KITAIFA YA KUMBUKIZI YA MATUKIO NA WAHANGA WA 29 OKTOBA 2025Kila uhai una thamani. Kila familia iliyopoteza mpendwa inastahili kusikilizwa, na kila jeraha la taifa linahitaji ukweli, haki na uponyaji.

THRDC inatoa wito kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuitambua tarehe 29 Oktoba ya kila mwaka kuwa Siku ya Kitaifa ya Kumbukizi ya Matukio na Wahanga wa Oktoba 2025.

Kumbukizi hii si ya kuendeleza chuki au kulipiza kisasi, bali ni ya kuwaenzi wahanga, kutafuta ukweli, kuhakikisha uwajibikaji, kuponya majeraha na kujenga maridhiano ya kweli.

Taifa haliwezi kujenga mustakabali imara kwa kusahau maumivu ya jana. Tukumbuke, tujifunze na tuchukue hatua kuhakikisha historia hii haijirudii tena.

🕯️ KUMBUKIZI, UKWELI, HAKI, UWAJIBIKAJI NA UPONYAJI — KAMWE YASIJIRUDIE TENA.

Sijui kwanini Serikali inawachekea hawa, hatua za haraka zichukuliwe kuzuia huu ujinga wao.
 
Ukiona mtu mzima anashabikia ujinga inabidi ujiulize jukukoni. Unataka tusherehekee maafa, ilu iweje?

Tarehe 19 Juni 1886 kule Ulaya kulifanyika Kikao (Berlin Conerence 1886) Wakiloni wakaigawa Afrika (wao wakiita the Dark Continent) sisi tukawekwa chini ya Ujeeumanu.

UNATAKA TUSHEREHEKEE SIKU HIYO?

Tarehe 3 Agosti 1978 tulivamiwa na Ndulu Iddi Amin.

UNATAKA TUSHEREHEKEE SIKU HIYO?

Tarehe 29 Oktoba 2026 mahaini wa CHADEMA walituma vijana wao kuvuruga Uchaguzi wa 2025 kwa msaada wa Kenya na ufadhilu wa Ford Foundation, magaidi 518 tukawawahi tukawawaua wai kabla hawajatuua sisi:

UNATAKA TUSHEREHEKEE VURUGU HIZO? TUWALILIE TULIOWAUA TUWAOMBEE KWA KUSHINDWA KUTUUA?
 
Back
Top Bottom