Timu ya uchunguzi wa Makosa makubwa kutoka ofisi ya DCI yatumwa kuchunguza Mauaji ya Ali Kibao wa CHADEMA

Inasikitisha. Nilidhani tumeshatoka humu. Kumbe bado tuko humu. Au ndio tunakwenda humu?
Yeyote mwenye kumpenda mama yetu Tanzania wa Amani hawezi kuliona hili ni kawaida. Ila nachojua tabia moja ya damu ni kwamba huwa inasema, inalia, inatoa sauti. Aonaye sirini anajua wa kumlipa
 
Mbona wanajizungusha sana,watuhumiwa ni Polisi
 
Kufuatia kutekwa na kuuawa kikatili kwa bwana au ndugu ALI KIBAO AMBAE ALISHUSHWA KWENYE GARI KAMPUNI YA TASHRIF na watu anbao walijifanya kuwa ni polisi kumbe sio wao kwa mujibu wa polisi makao makuu dodoma!

Na pia hii inatupa picha kuwa hii nchi imeoza imebaki kunuka tu ,ki vip nasema hivi how come polisi wanatoa statement nyepesi kiasi kile.????? Kiasi kwamba mtu yeyote anaweza kujifanya polisi na kufanya mauaji na asichukuliwe hatua hata na wananchi mana wamelala usingizi wa pono

Na pia hapa tunapata fundisho kuwa hawa wanaokuja kukamata kumbe sio polisi kwa sababu wakishafanya yao polisi makao makuu wanakanusha kuhusika moja kwa moja.

Je nini cha kufanya.??????

Kinachoendelea kule kenya na gen z huu wa hawa watu wa serikali wasio taka kuwajibika ambao wanaona wapinzani wao kama vikwazo
 
unafikiri hao watu wangekuwa wanakuja mikono mitupu polisi wangolopoka na kubwabwaja upuuzi huo???
 
Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko au mkoba auchukue. Asiye na upanga, auze koti lake anunue upanga...".

Luka 22:36
 
 
Kuna taarifa kwamba Kibao alipotekwa, kulikuana Askari mwenye uniform za polisi usalama barabarani.
Waanza na huyo trafik. Je alipoona raia anatekwa na watu ambao hawana uniform lkn walikua na silaha, aliichukua jukumu gani? Aliripoti mahali popote ?
Kwanini hakuzuia utekaji Kama kweli hakuwajua watekaji kwamba Ni wenzake?
WAANZE NA HUYO TRAFIK.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…