Timu ya uchunguzi wa Makosa makubwa kutoka ofisi ya DCI yatumwa kuchunguza Mauaji ya Ali Kibao wa CHADEMA

Yaani Kingai ndiye wa kuunda timu ya uchinguzi?
 
DCI Kingai Mzee wa kubambika kesi ndio mchunguzi mkuu.
 
Watz walivyo wa hovyo(si wote) hata sishangai kwa comment zao na wasio na msaada wowote pale wanapohitajika wao ni kubonyeza bata za simu na kuandika tu malamishi na makasiriko.

Watz wamejaa malalakisha na unafiki mtupu, wamejaa ulimbuken wanapohitajika kutoa msaada wao hurudi nyuma.

Watz n kuandika andika tu na kupost mapicha picha ila ukiwauliza we ulichukua hatua gan ulipoona tukio hiloooo???? Majawabu hakuna

Tushirikiane,tupendane,tushiriki kutoa taarifa ambazo tunaamin zitasaidia kufichua wahalifu na tuondokane na kulaumu vyombo ilihali hatuvipi ushirikiano. Pia tuwe na iman na vyombo husika.
 
Kinachoendelea nchini ni masikitiko hakuna alie salama kwa sasa kila mmoja anaweza kutekwa na kuawa pasina kujulikana wahusika,

Rais anatoa amri ya Uchunguzi kwa wakati huu wakati kuna kijana alie mchora na kuichana picha alio ichora huku akijirekodi taarifa zake hakuna anae zijua wapi aliko,

Kuna idadi kubwa ya watanzania waliotekwa na kufichwa na hakuna hatua zozote zilizo tolewa kuwahusu,

Jeshi la polisi na vyombo vingine vya kuchunguza matukio ni kama kuna jeshi jipya ndani ya mifumo ya kiutawala kazi yake ni kunyamazisha yeyote anae jifanya kuhoji au kuelezea hisia zake bayana.
 
Viongozi na familia zao wapo salama
 
Mhe. Rais kwa unyenyekevu Mkubwa na Mapenzi Makubwa niliyonayo kwako, Kwa Nchi yangu na Chama changu CCM.
Naomba kama utaona Comment yangu hii, wafuatao washauriwe kujiuzulu ili kuendelea kulinda Heshma yao na Mchango wao Mkubwa kwa Taifa letu! na endapo watasita kujiuzulu basi usisite kuwatumbua wafuatao ndani ya wiki hii.

1. Mh. Waziri wa Mambo ya Ndani
2. IGP
3. Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Rais wetu na watu wake.

Naomba kuwasilisha.
 
Kunakitu umeandika sijui unajua umeandika ukwe au umehisiii.

KAtika haya maandishi yako kuna ukweli umeundika.
 
Wapi Tena Mwalimu Nyerere na Mobutu Sesesekoo...! Amina Chifupa Eeeh na Chacha Wangwe, waliokuwa na Heshima na Madaraka Duniani leo hii hawapoo, sembuse mimi na wewe Wapangaji Tunanyanyasana! Ndoto ya Mwenda kwa Miguu kumiliki Baskeli, na huyo Mwenye Baskeli anaota lini atapata piki piki! Ukipata Pikipiki unatamani Umiliki Corola Eeeh..! Ukipewa Corola unataka uwe na Prado.....!
Ahsante Patcho Mwamba kwa kipande hiki

Good bye Mtanzania Mwenzetu Mr. Kibao, Pole kwa Familia, Pole kwa Chama Chake na pole kwa Watanzania wote.
 
Wameshajua tz waoga ukiambiwa mambo ya kwenda police kutoa taarfa n jambo lingne utaskia siku2 au 3 hili jambo limepita limekuja lingne maana hili sio la kwanza luna yule dogo alitechoma picha ya rais had leo hajapatikana!! Tuombe msaada kwa wale vijana wa 🇰🇪 sisi 🇹🇿 hz mambo hatuwez wanasiasa wametupanda kichwan kwenye katba wao ndo wenye ndugu tofaut na Kenya 🇰🇪
 
Tunaunganisha watu waliopotezana kwa bei nafuu, wahi sasa kazi ni nyingi muda ni mchache.
 
Sasa hapo sielewei.abiria anashushwa kwenye garia then unaendelea na safari bila kupata taarifa za mteja wako amepelekwa wapi? shenzi kabisa .tuanze kwanaza konda,dreva, na bairia wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…