Pascal Mayalla,
Zamani hakuna idara ilikuwa na heshima kama Tiss,,heshima iyo haikuwepo kwa nidham ya uwog au walilazimisha kuheshimiwa,,HAPANA ila WELEDI,,USIRI NA UMAKINI wa watumishi wa idara husika.
Kazi kubwa ya Idara hii ni INTELIJENSIA na kazi iyo ufanywa na watu wenye uwezo mkubwa kiakili na SIO WANYANYUA VYUMA WALA WAPIGA KARETI.
Katika nchi zote zilizoendelea duniani,,idara zenye watumishi wenye uwezo mkubwa KIAKILI,,KUFANYA MAHAMUZI SAHIHI KWA WAKATI SAHIHI NA WADADISI WA MAMBO KWA KINA ni Idara 3 tuu,,nazo ni;
1)USALAMA WA TAIFA
2)ELIMU
3)AFYA.
Sasa hapa kwetu mambo yamebadilika sana tena sana,,mtu anapata zero kidato cha 4 au 6 anapewa jukumu la kulinda USALAMA WA TAIFA,,je kwa vigezo vipi?ndio maana ugonvi kidogo wa bar mtu anatoa bastola na kukutisha me usalama wa Taifa.
Zamani maofisa wa usalama ilikuwa ngumu mno kumjua kwa kuwa walikuwa wanajua "MAADILI NA MIIKO YA KAZI ZAO",,mtu hata mke/mme wake anaweza ishi naye nyumba,,kitanda 1 kwa zaidi ya miaka kadhaa hasijue mumewe/mkewe anafanya kazi usalama wa Taifa.
Vitendo vinavyosemekana sasa kama vinafanywa na idara hii kwa kweli ni aibu sana na mnaishushia hadhi idara nyeti kama hii.
Ili kurudisha HESHIMA NA HADHI ya idara hii LAZIMA MABOLESHO yafanyike.