1. CIA ilikumbwa na skendo kubwa nyingi sana ikiwemo waterboarding pamoja na interrogation techniques nyingi ambazo zinahusisha torture, lakini haijawahi kufumuliwa wala kuvunjwa but wahusika waliweza kuchukuliwa hatua ipasavyo.
2. Matukio mbalimbali hapa nchini wengi wameweza kuyaunganisha kwamba eti yamefanywa na TISS bila ya kuweka ushahidi (i can neither confirm nor deny that) lakini basi tuseme uenda labda matendo hayo yamefanywa na baadhi ya vijana wasio na maadili wa Taasisi hii ambao vijana hawa uenda walitenda for their personal gain, ego, promotion au just to follow orders (kumbekeni vijana wote hawa ni Paramilitary Operations Officers (PMOO) na kazi yao ni ku-follow orders).
3. Mengi yanafanywa na hii idara, ukubwa na mazuri wafanyayo sio rahisi kujulikana kwa wazi wazi ukilinganisha dhidi ya makosa machache yaliyotokea, makosa ambayo eti leo hii yanataka kutumika kama kigezo cha kutaka kuivunja au kubadili mfumo wa TISS!; Nawaombeni Watanzania msisahau kila ukiona umeweza kulala na kuamka salama na kula ugali wako na ukashiba ukaweza kuingia Jamii Forum basi ujue ni siku nyingine ambayo Idara imeweza kuiweka Tanzania salama; Ukiweza kwenda shopping mall na kununua mahitaji yako salama tofauti na mataifa mengine basi ujue ni siku nyingine ambayo Idara imeweza kuiweka Tanzania salama, n.k. Tuvunje kitu kisichokuwa na mafanikio lakini ukipima mafanikio ya hii Idara basi haina sababu ya kutaka kuivunja ata siku moja, Sasa Mzee Mwanakijiji, Pascal Mayalla et al kwanini tuivunje/tuifumue hii idara?!
3b. Watanzania wenzangu naomba Mtambue TISS ni mti mkubwa wenye mizizi mingi mikubwa na matawi mengi; Sasa endapo jani moja likidondoka kutoka kwenye tawi moja la mti huu mkubwa basi nawaomba Watanzania wenzangu kwa heshima na taadhima tusilete hukumu kwenye mti wote; Tukemee makosa ya hao vijana/kikundi na viongozi wao ikiwezekana wachukuliwe hatua ipasavyo kama ikidhibitika lakini tusilete SIASA kwenye jambo hili la msingi sana kwa mustakabali wa taifa letu; Je tumeshajiuliza ni nani yupo nyuma ya pazia?? Kwanini vugu vugu hili linatokea sasa mpaka chombo kikaanza kusemwa/kushutumiwa? Je walio nyuma ya pazia wanataka kuleta ile notion ya wagawanye/wavuruge watawale?? Kumbukeni maadui wetu ni wengi (wanao onekana na wasio onekana) na wanaongezeka kila siku (direct or through their Proxies) na uenda hivi sasa hapa tulipo tunacheza mziki wa adui, Mkivunja TISS leo kumbukeni kesho mtapata tabu sana kulinda Tanzania yetu; Kumbukeni tuna reserve kubwa ya Gas/Mafuta na madini mengi tuliyonayo hivyo basi tunahitaji TISS hii imara kupambana na maadui wanaotaka kuingusha Tanzania na kuchukua rasilimali zetu!!
3c. Vijana wa Idara hii ndani na nje ya Tanzania wanafanya kazi kubwa na kurisk au kupoteza maisha yao 24/7/365 kwa ajili yetu na kwa ajili ya Taifa la Tanzania kazi ambayo sio kazi ndogo kabisa, Kazi ambayo Mataifa mengi Afrika na duniani wanashindwa kabisa kufanya kama wafanyavyo TISS siku zote yaani kuiweka Tanzania salama na kuondoa threats zozote kila siku. Tusikubali kelele za wachache kutaka kuvuruga mafanikio ya Idara, Wahusika walio ichafua kwa makosa yao wachukuliwe hatua kama ikidhibitika ili Idara isonge mbele NA SIO KUIFUMUA.
4. Viongozi wote waandamizi wa kila idara, tumieni hekima/busara/uzoefu wenu kuiweka TISS imara zaidi na izidi kusonga mbele; jitahidini kuitoa Siasa ndani ya Idara na mifano itolewe kwa wale wote wanao enda kinyume na ABCD za Idara. Natumaini bado wazee wengi wenye hekima bado wapo basi tumieni hekima zenu kulinda idara na kulinda heshima ya Idara hii na mkumbuke uimara wa Tanzania ya kesho inategemea sana na uimara wa TISS ya leo. Hiki ni kipimo cha uongozi wenu kuiokoa na kuisafisha Idara.
Mungu ibariki TISS, Mungu ibariki Tanzania.
Pascal Mayalla,