TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

RIP baba yake mayala Former RSO, ila hao watekaji sio toka idarani ni watu tu wasiokua wastaarabu

What a troll!

Ukipewa akili na maarifa basi tumia japo kidogo..

Mbona munakua stupid kiasi hicho!

7ef51147c46e26c23dbe28706305736a.jpg
 
Mkuu,pasikali kumbuka mzizi uliojichimbia chini zaidi ulisha kuambia kua wewe ni njaaa tuu(usukumani)hivyo hata akisoma uzi wako huu bado ataamini kua njaa tu ndo inakusumbua.jiandae kwa uteuzi[emoji2] [emoji2] .

Ila shukrani mkuu kwa kutuwekea mifano hai,tena ukiwa wewe mwenyewe ni muhanga.

Chakushangaza bado kuna boss binadamu wenzetu watakuona wewe kua ni mchochezi.
 
TISS iko chini ya rais ambaye Mimi Mwanakijiji alifunga siku 40 ili Magufuli awe rais

Kwa yote yanayoendelea naamini Mwanakijiji atakuwa kafurahi sana rohoni mwake na anachekelea
 
Ile kesi ya uhaini 1982 hao jamaa wa TII SSM nakumbuka watuhumiwa wa uhaini waliwakuta TISS wamo gerezani wanajifanya nao wafungwa lakini kumbe walikuwa kazi yao bado wanaifanya humo.gerezani kuna mtuhumiwa wa ile kesi alikuwa anasumbuliwa na huyo mtiss kila akirudi kutoka mahakamani jamaa yule wa TISS anamshika shati jamaa anamuuliza hivi wewe humu ndani umekuja kufanya nini wakati ulipokuwa jeshini ulikuwa unakula bure unavaa nguo za jeshi bure unalala bure yule mwanajeshi Yale maswali baadae akaniambia huyu sio.mfungwa mwenzetu huyu ni M TI I SS M
 
Unamhoji kaka msomi wa spesho skul na UDSM?

Utakuwa kilaza wewe...
Sasa mtu anashindwa kutofautisha hizi scenarios mbili. Ya mzee wake Mayalla tayari kulikuwa na facts ambazo Nyerere alizitumia kuwawajibisha watu. Sasa hii ya bungeni na kelele za bavicha na kina Lissu utaiwajibishaje TISS? Kwenye speculation tu!
 
1. CIA ilikumbwa na skendo kubwa nyingi sana ikiwemo waterboarding pamoja na interrogation techniques nyingi ambazo zinahusisha torture, lakini haijawahi kufumuliwa wala kuvunjwa but wahusika waliweza kuchukuliwa hatua ipasavyo.

2. Matukio mbalimbali hapa nchini wengi wameweza kuyaunganisha kwamba eti yamefanywa na TISS bila ya kuweka ushahidi (i can neither confirm nor deny that) lakini basi tuseme uenda labda matendo hayo yamefanywa na baadhi ya vijana wasio na maadili wa Taasisi hii ambao vijana hawa uenda walitenda for their personal gain, ego, promotion au just to follow orders (kumbekeni vijana wote hawa ni Paramilitary Operations Officers (PMOO) na kazi yao ni ku-follow orders).

3. Mengi yanafanywa na hii idara, ukubwa na mazuri wafanyayo sio rahisi kujulikana kwa wazi wazi ukilinganisha dhidi ya makosa machache yaliyotokea, makosa ambayo eti leo hii yanataka kutumika kama kigezo cha kutaka kuivunja au kubadili mfumo wa TISS!; Nawaombeni Watanzania msisahau kila ukiona umeweza kulala na kuamka salama na kula ugali wako na ukashiba ukaweza kuingia Jamii Forum basi ujue ni siku nyingine ambayo Idara imeweza kuiweka Tanzania salama; Ukiweza kwenda shopping mall na kununua mahitaji yako salama tofauti na mataifa mengine basi ujue ni siku nyingine ambayo Idara imeweza kuiweka Tanzania salama, n.k. Tuvunje kitu kisichokuwa na mafanikio lakini ukipima mafanikio ya hii Idara basi haina sababu ya kutaka kuivunja ata siku moja, Sasa Mzee Mwanakijiji, Pascal Mayalla et al kwanini tuivunje/tuifumue hii idara?!

3b. Watanzania wenzangu naomba Mtambue TISS ni mti mkubwa wenye mizizi mingi mikubwa na matawi mengi; Sasa endapo jani moja likidondoka kutoka kwenye tawi moja la mti huu mkubwa basi nawaomba Watanzania wenzangu kwa heshima na taadhima tusilete hukumu kwenye mti wote; Tukemee makosa ya hao vijana/kikundi na viongozi wao ikiwezekana wachukuliwe hatua ipasavyo kama ikidhibitika lakini tusilete SIASA kwenye jambo hili la msingi sana kwa mustakabali wa taifa letu; Je tumeshajiuliza ni nani yupo nyuma ya pazia?? Kwanini vugu vugu hili linatokea sasa mpaka chombo kikaanza kusemwa/kushutumiwa? Je walio nyuma ya pazia wanataka kuleta ile notion ya wagawanye/wavuruge watawale?? Kumbukeni maadui wetu ni wengi (wanao onekana na wasio onekana) na wanaongezeka kila siku (direct or through their Proxies) na uenda hivi sasa hapa tulipo tunacheza mziki wa adui, Mkivunja TISS leo kumbukeni kesho mtapata tabu sana kulinda Tanzania yetu; Kumbukeni tuna reserve kubwa ya Gas/Mafuta na madini mengi tuliyonayo hivyo basi tunahitaji TISS hii imara kupambana na maadui wanaotaka kuingusha Tanzania na kuchukua rasilimali zetu!!

3c. Vijana wa Idara hii ndani na nje ya Tanzania wanafanya kazi kubwa na kurisk au kupoteza maisha yao 24/7/365 kwa ajili yetu na kwa ajili ya Taifa la Tanzania kazi ambayo sio kazi ndogo kabisa, Kazi ambayo Mataifa mengi Afrika na duniani wanashindwa kabisa kufanya kama wafanyavyo TISS siku zote yaani kuiweka Tanzania salama na kuondoa threats zozote kila siku. Tusikubali kelele za wachache kutaka kuvuruga mafanikio ya Idara, Wahusika walio ichafua kwa makosa yao wachukuliwe hatua kama ikidhibitika ili Idara isonge mbele NA SIO KUIFUMUA.

4. Viongozi wote waandamizi wa kila idara, tumieni hekima/busara/uzoefu wenu kuiweka TISS imara zaidi na izidi kusonga mbele; jitahidini kuitoa Siasa ndani ya Idara na mifano itolewe kwa wale wote wanao enda kinyume na ABCD za Idara. Natumaini bado wazee wengi wenye hekima bado wapo basi tumieni hekima zenu kulinda idara na kulinda heshima ya Idara hii na mkumbuke uimara wa Tanzania ya kesho inategemea sana na uimara wa TISS ya leo. Hiki ni kipimo cha uongozi wenu kuiokoa na kuisafisha Idara.

Mungu ibariki TISS, Mungu ibariki Tanzania.
Pascal Mayalla,
 
Pasikali, ninapendaga stori zako. Maswali 2.
1. Huyu Dkt. Nkulila uliyemtaja ndiye yule mweye Hospitali huku Arusha?
2. Murtaza Lakha ndiye yule aliyewatetea kina nani wale wa kesi ya miaka ya 80?
 
Hoja binafsi ilishakataliwa jana....
Wanadai tz hakuna utekwaji au mauaji holela wakati kila siku wanaokotwa watu wameuawa.[emoji20] [emoji20]

.
.
Wabunge wa ccm wanasema hauna mauaji,,, ally kessy kasema, roma angeuawa......mmmhhhmm!!!

Kuna mwanajamvi kauliza humu, kwa nini hili suala lipigiwe mchapo namna hii wakati huu?

Jibu ni rahisi tu, viongozi wa upinzani hawana mahala pa kutokea katika utawala wa Magufuli, kilichobaki ni kuongelea matukio kwa kupaza sauti, wakitegemea wajomba zao huko watasikia na kuingilia kati. Bahati mbaya kwao hao wajomba ndiyo kwanza wanaipongeza kwa kuipa misaada na mikopo Serikali ya Magufuli.

Bunge liko kwenye kikao muhimu cha bajeti, wanakuja na hoja za matukio na kudai ni hoja za dharura, bajeti iwekwe kando! Bajeti ya mwaka jana walisusia kisa ati wananyimwa uhuru wa kuchangia bungeni, hadi wakatoka nje wameziba midomo.

NYIE WABUNGE WA UPINZANI ACHENI UTOTO MJADILI BAJETI. NYIE WENYEWE MLITUNGA SHERIA ZA KUANZISHA IDARA ZA ULINZI NA USALAMA WA TAIFA LETU, MZIACHE ZIFANYE KAZI ZAKE NANYI KAZI ZENU. KAMA KUNA MAPUNGUFU KATIKA SHERIA ZA UANZISHWAJI WAKE TOENI HOJA YA MAREKEBISHO. HIYO NDIYO KAZI YENU. WALIOONEWA WAFIKISHE TUHUMA MAHAKAMANI CHOMBO KINGINE KIKATIBA KWA AJILI YA HAKI.

Tunawachoka na mipasho yenu nje na ndani ya Bunge. Wengine kama Mh Mdee, bila aibu, anasema bajeti hewa, qakati yeye ni mmoja wa wahusika kupitisha hiyo bajeti. Kama hakuhusika, wapiga kura watamwuliza alikuwa wapi wakati bajeti hewa inapitisha. HUKO NDIKO KUKURUPUKA.
 
TISS hawana makosa yoyote kwani kuna uzushi na mambo yanayatengenezwa. Kosa kubwa ni kuwa Wananchi Tanzania waliachiwa kufanya mambo yoyote . mahali popote na hamna mtu yoyote wa kumfanya kitu chochote hata kama amevunja sheria. Aidha kuna watu walijiona na bado wanajiona wako juu ya sheria. hili ndio tatizo kuuubwa sana. Kuna watu walikuwa hawalipi kodi na mpaka sasa wanaona walistahili kutokulipa kodi. Can you imagine?!?!? Kuna watu hawataki kufanya kazi lakini wanataka luxury life! Iliwezekana then sasa kwa sababu kwa sasa haiwezekani basi wanatumia mbinu yoyote kuvuruga nchi. Mbona wewe mwanfdishi una bidiii na ninaamini unalipa kodi? Kwa nini wengine wasilipe jkodi? matokea yake wanachochea watu kwa chinichini Ewwe Mtanzania usikubali kutumiwa bila kujijua!
 
TISS iko chini ya rais ambaye Mimi Mwanakijiji alifunga siku 40 ili Magufuli awe rais

Kwa yote yanayoendelea naamini Mwanakijiji atakuwa kafurahi sana rohoni mwake na anachekelea
Hizi ndo zama mpya walizotaka.juzi kati hapa mello alivyotiwa nguvuni mzee wa zama mpya alicharuka kama mbogo.

Uzuri wa haya mambo yanapo kukuta ndo akili zinarudi
 
Sasa mtu anashindwa kutofautisha hizi scenarios mbili. Ya mzee wake Mayalla tayari kulikuwa na facts ambazo Nyerere alizitumia kuwawajibisha watu. Sasa hii ya bungeni na kelele za bavicha na kina Lissu utaiwajibishaje TISS? Kwenye speculation tu!
Mkuu hata ya bashite na clauds bado nayo sio fact?
 
Back
Top Bottom