TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Pascal Mayalla,
Pasco
TISS wamefanya kazi nzuri over the years.
Kwa wale mnaoweza kuwafuatilia kazi zao hazina kujitangaza wala kutangaza mafanikio yao.
Silence to them is a tool of the game.

Kuwasema sema sana haisaidii sana lakini kwa vile sasa mambo wanyotupiwa kama lawama na wanasiasa, unaweza kuona kuwa ,pengine, nasema pengine, kuna viongozi wanawatumia visivyo.

Uzuri wa TISS, is, they are everywhere, anytime, na wanajua yote yanayoendelea.
Tatizo ni kwamba hawawezi kusema, but time will absolve and prove them right.

Tiss ni kama bata bwawani, anapiga pedali ya kufa mtu, lakini usoni wala haonyeshi.
 
Ibambasi,

Ndugu yangu naona hapa umeamua kuleta ujuaji tu. Wewe unatambua fika kwamba huwezi kuwa na data zinazohusu shughuli au kashfa za idara hii halafu ukawa salama. Hata huko mbele waliostaarabika hawaruhusu mtu asiye na clearance aone taarifa za wanausalama hata kama anafanya kwa nia njema (whistleblower). Wote tunajua kwanini Snowden kajificha Russia na kwanini Asange alishtakiwa.

Taasisi hizi zimejengwa ili watu waishie kwenye speculations tu, kwa nia njema. Sasa wakati mwingine hiyo nia njema ya usiri ndio inatumiwa vibaya.Lakin hatuzuiwi kuwasema kwakuwa tu hatuna ushahidi. Hata kuhisiwa tu hilo ni kosa kubwa kwao. Tukumbuke idara hii iliwahi kuheshimiwa na kila mtu na kuogopewa. Sina hakika kama bado wanaheshimiwa. Chombo cha kizalendo kama hicho hakipaswi kuchukiwa na jamii.
 
Mwl Nyerere, Huwezi kumfaninisha na bastard fulani. Kuongoza Nchi si sawa na kuongoza kijiwe.
Pascal Mayalla Kisa cha Mzee wako kina fanana na issue ya Mzee wangu, katika ubalozi fulani Mwaka 1983. Mwl Hakusita kuchukua hatua, ilituathiri,lakini hatua ilichukuliwa.
TISS, ain't demigods. They're powerful yes, but accountable before the law.
 
Pole Pascal kwa uliyopitia , cha msingi taasisi yoyote inayoendeshwa na binadamu sio ya kuamini asilimia mia.
 
Sheria inayoanzisha Idara hii inapiga marufuku kabisa Afisa Usalama kujitambulisha hadharani(nadhani isipokuwa wale wenye nafasi za kisiasa kama DSO na RSO)

Na ikifahamika umejitambulisha basi unafukuzwa kazi

Lakini Siku hizi kwenye Bar, akizidiwa kete tu kwa demu analipuka


Wanavaa suti zao bastola zinaonekana nje nje,maswali mengi "unanijua mimi ni nani" nikujue so what? You are a secret service employee,ujulikane iweje? Kama kuna uhalifu basi relay taarifa mapema kwa polisi walio karibu au la chukua taarifa bila Ku disclose identity !!

Miaka ijayo kuna vijana wataomba wawe wanavaa hata vitambulisho kifuani,
 
Kelele nyiiingi,ROMA aeleze ametekwa na nani?kuvipaka matope vyombo vyetu vya ulinzi na usalama bila ya kuwa na facts,ni ujuha tu

TISS wanafanya kazi kubwa sana,lakini mwisho wa siku ni wao wanaotupiwa lawama na wanasiasa haswa wa upinzani baada ya mipango yao ovu,ya kuivuruga nchi kuharibiwa na TISS.

Kwenye uchaguzi wa 2010,TISS walichafuliwa sana na Chadema,kiasi cha Jacky Zoka,kuita waandishi na kusema wanasiasa msituingize kwenye mambo yenu.TISS hii mnayoilaumu,tuliambiwa zaidi ya nusu yao wanaripoti Chadema,imekuaje tena leo ndio wawe wanalaumiwa na wapinzani?

Mpaka sasa kuna tukio moja tu la utekaji,alietekwa hataki kusema katekwa na nani na kwa sababu ipi.Je kama walidhulumiana bangi au madawa ya kulevya?

Tuache ramli chonganishi,na chuki za kisiasa TISS bado wapo vizuri sana,hawahitaji hata kuguswa achilia mbali kuvunjwa
 
Of all the Important things ni kumteka Roma Mkatoliki kweli?, yaani Mtoto yule ambaye hajawahi kuchinja hata mbuzi, unamchukua , unamteka, unamtorture!. For what?, hii ni aibu kubwa sana, sikutegemea kama haya yanaweza kutokea katika ardhi ya Tanzania! shame! shame! shame!
 
Kwa vile umethubutu kusema taasis hiyo yaTISS ndiyo inatesa mbona unashindwa kumtaja hata mmoja kwa jina.
Acha kuwalaghai watu ili wakuonee huruma.
Hujui hata tofauti ya mhaini wa nchi na mhalifu au ha mchochezi.
 
Mimi naomba haya yafanyike...
Kwanza, TISS iwe taasisi tengevu inayojitegemea katika maamuzi na uendeshaji. Namaanisha, TISS isiwe chini ya Rais, wala isiagizwe kufanya jambo kwa maslahi ya mtu fulani au kwa sababu ya Chama chake. Yote yawe kwa ajili ya Manufaa ya Taifa zima.

Pili, TISS iwe wazi. Kuanzia shughuli zake, uendeshaji wake pamoja na ofisi zao hata na vyuo vyao vya mafunzo. Watu huogopa kwa sababu ni watu wasiri sana. Yaani, mtu anayehisiwa kama mwanausalama anaogopwa sana. Wameshajengewa dhana kuwa ni watu watesaji, wauwaji,watekaji na majina yanayofanana na hayo. Hili ni kutokana na usiri uliogubika humo.

Tatu, TISS wawe wanatoa matamko ya kukana kuhusishwa na mambo wasiyohusika nayo. Naam, mara nyingine watu wanatekwa na kufanyiwa ndivyo sivyo lakini usalama wakawa hawajahusika kwa namna moja ama nyingine. Watu wakaanza kusema maneno yao wajuavyo, inabidi TISS wajitokeze na kupinga kabisa kuwa hawajahusika ili kuondoa wasiwasi. Kutokukanusha taarifa hizo inaipa nguvu hoja kwamba wamehusika ingali hawajatenda lolote.

Nne, wananchi wapewe Elimu juu ya Usalama kuwa ni walinzi wao. Wamejitoa kwa namna yeyote ili kuhakikisha nchi inakuwa salama na wala hawana nia yoyote mbaya kwa wananchi wake.

Hili wimbi la kuwahusisha TISS katika matukio ya Utekaji utafikia kikomo.
 
Back
Top Bottom