Tozo za Miamala: Serikali yapunguza viwango kwa 30%. Watoa huduma za simu waridhia kupunguza 10%
Unatengeneza tatizo unapiga kadhaa kisha unalitatua kwa kupunguza kidoogo halafu unapongezwa

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
Ndugu yangu Mshana Jr Tanzania ni nchi yenye wananchi wa pekee kabisa. Niseme wazi sisi wananchi ujinga na woga wetu ndiyo mauti yetu. Hebu fikiria: Mtu unafanya kazi serikalini au kwenye shirika la umma/binafsi au unafanya biashara. Huko kote unalipa kodi zote kwa mujibu wa sheria. Unapokea mshahara amabo ni haki yako. Siku unaamua kumtumia mzazi wako huko kijijini fedha za matumizi, unakatwa tena kodi! Huu ni uhuni wa hali ya juu kabisa. Yaani pato lako ambalo umeshalipia kila kitu unakatwa tena! Hapa amabo walitakiwa kuchaji mtumaji fedha ni makampuni ya simu tu (kama gharama ya kutuma). Inasikitisha wananchi nao tuko kimya kwa uhuni kama huu.
 
Mleta mada nimekuelewa vizuri sana kuhusu tozo minimization.
Kiukweli ingepungua kwa walau 50% ingeleta matumaini lakini chini ya hapo bado ni mtihani!
Tena waongeze iwe nusu kwa nusu ukitumiwa 50 inatakiwa tozo iwe 25,000/
 
Nikajua ita-take immediate effect ila hamna tofauti kati ya Monday na leo usiku 🥴🥴
20210831_212327.jpg
20210831_212346.jpg
 
Ili Kujua Punguzo la Kweli unapaswa Kujua Ongezeko la tangu awali kwa hili punguzo ni Ongezeko la kiasi gani....

Kumbuka Tuzo zilikuwepo..., Zikaongezeka Maradufu..., Hili Punguzo ni kupunguza hilo Ongezeko

Kwahio Serikali imepunguza Ongezeko. Correct Statement ni Serikali Kuongeza Tuzo kwa Asilima kadhaa ni dhihaka kwa watumiaji
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba tozo zilikuwepo tokea awali kabla ya ubunifu wa comrade zungu? au unataka kutuingiza chaka.....
 
Ndugu yangu Mshana Jr Tanzania ni nchi yenye wananchi wa pekee kabisa. Niseme wazi sisi wananchi ujinga na woga wetu ndiyo mauti yetu. Hebu fikiria: Mtu unafanya kazi serikalini au kwenye shirika la umma/binafsi au unafanya biashara. Huko kote unalipa kodi zote kwa mujibu wa sheria. Unapokea mshahara amabo ni haki yako. Siku unaamua kumtumia mzazi wako huko kijijini fedha za matumizi, unakatwa tena kodi! Huu ni uhuni wa hali ya juu kabisa. Yaani pato lako ambalo umeshalipia kila kitu unakatwa tena! Hapa amabo walitakiwa kuchaji mtumaji fedha ni makampuni ya simu tu (kama gharama ya kutuma). Inasikitisha wananchi nao tuko kimya kwa uhuni kama huu.
Halafu naye akipokea na kwenda kutoa anakatwa tena[emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827]

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Serikali isiyoweka madarakani na wananchi Katu haiwezi kuwa na huruma na wananchi wake
 
Umerithi miradi ya kimkakati na kudhamiria kuimaliza...SGR ,BWAWA LA UMEME MWALIMU NYERERE ,UPANUZI WA BANDARI ,VIWANJA VYA NDEGE n.k

Umepandisha madaraja watumishi wa umma.....(miaka mingi ilipita)

Umeanza kuajiri vijana 8000(Tamisemi+Wizara ya Afya)....vijana hao wako mitaani toka wamalize vyuo 2012...(miaka mingi hawakuajiriwa kwa wingi huo)....

Umerudisha kazini watumishi 3300 ambao WALIKWENDA KUJIENDELEZA ELIMU YA KIDATO CHA NNE.....

Umeongeza FEDHA katika "kapu" la BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU(HESLB)ili vijana wengi wanufaike....

Umefuta TOZO ya RETENTION FEE ya 6% kwa wanufaika wa HESLB....

Umeahidi kupandisha mishahara watumishi wa umma mwaka ujao wa fedha......

Unadhamiria kuinua KILIMO CHETU kwa kuzijenga barabara mpaka mashambani.....

Unadhamiria KUONGEZA IDADI YA VITUO VYA AFYA viwafikie mpaka maeneo YA NDANI HUKO....

*******************
YOTE HAYO UTAYAFANYAJE KAMA HUTOBUNI NA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO NA TOZO?!!!

Hebu tuweni wa kweli jama...😲😲

#NchiKwanza
#TozoNiMuhimu
#SiempreJMT
 
Hebu tuweni wa kweli jama...[emoji44][emoji44]

#NchiKwanza
#TozoNiMuhimu
#SiempreJMT
We nawe hujui WanaNchi wanalalamikia nini.
WanaNchi hawapingi Tozo. Wanachopinga ni Tozo inayoumiza.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Agosti 31, 2021 ametia saini mabadiliko ya tozo za miamala ambapo serikali imepunguza 30% na makampuni ya simu Kupunguza 10% kutoka kwenye gharama za awali za ufanyaji wa miamala.
Hata wakipunguza kwa 90% bado serikali haina hoja za msingi za kuhalalisha uchukuaji wa fedha za wananchi kupitia kivuli cha tozo. Serikali inaficha mapato halisi kutokana na tozo. Idadi ya miamala ifanyikayo kwa mwaka nchini, 10% walio iweka toka mapato ya makampuni inazidi lengo walilolisema. Tozo zimepunguzwa, mafuta kuanzia kesho yamepandishwa. Maisha bora kwa wateule, kazi iendelee.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
We nawe hujui WanaNchi wanalalamikia nini.
WanaNchi hawapingi Tozo. Wanachopinga ni Tozo inayoumiza.
Imeshapunguzwa bwashee.....

Baadhi ya wenye nyumba wanalalamikia hadi TOZO ya "buku" kwa mwezi........

TUJIKUMBUSHE KULIJENGA TAIFA LETU SISI WENYEWE....

Hata misaada inayotujia huwa inatoka katika kodi za WANANCHI WAO......
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Agosti 31, 2021 ametia saini mabadiliko ya tozo za miamala ambapo serikali imepunguza 30% na makampuni ya simu Kupunguza 10% kutoka kwenye gharama za awali za ufanyaji wa miamala.

Miamala haturejei hadi Tozo za uzalendo = 0
 
Back
Top Bottom