Tozo za Miamala: Serikali yapunguza viwango kwa 30%. Watoa huduma za simu waridhia kupunguza 10%
Sheria imeweka tozo lakini haikutaja kiasi cha tozo, kanuni ndio zinazoweka viwango vya tozo, na waziri wa fwdha ana mamlaka kisheria ya kubadilisha kanuni
Kwa hiyo aliposema kuwa yeye kama waziri hana uwezo wa kuzibadilisha tozo kwa vile zimepitishwa na Bunge alikuwa anadanganya umma?

Naona kabisa hapa serikali imepunguza viwango kwa shinikizo toka kwa wananchi, lakini kama vitu vingine bado hawajavigusa kama mafuta ya kupikia, gas na mengine.

Nadhani watatafuta sehemu nyingine wakafidie hilo pengo, serikali isimkandamize mwananchi wa kawaida, ibuni na kusimamia vikubwa tulivyojaliwa na Mungu.

Nashauri serikali ingebaki na hivyo viwango vipya bila kuongeza pengine.
Tayari wamefidia kwenye mafuta ya petroli na dizeli
 
Kwahio Punguzo hilo, litakuwa ni Ongezeko la Asilimia ngapi kutoka tulipokuwepo Awali....

Hii inanikumbusha story ya ukitaka kumchemsha chura ongeza moto kidogo kidogo..., ila huenda hapa ni kuweka moto mkali kuliko ili ukipunguza kidogo mtu aone ahueni ila kumbe bado ni moto mkali
Swali zuri sana, binafsi nimegundua hizi tozo hazina formula maalum, yaani kuna miamala mingine tozo ya kodi ni kubwa Mara tatu kuliko tozo ya ada mtoa Huduma, mfano mie mwenye coda nikitaka kutuma elf40 kwa voda mwenzangu jumla ya tozo ni 1910. Tozo ya ada ni 400 wkt tozo ya kodi ni 1510, miamala mingne unakuta tozo ya ada na kodi zinalingana, pengine tena unakuta ada ni kubwa kuliko kodi, yaani formula ya hizi tozo kwa kwel ni magazijuto.
 
Ilitakiwa waiondoe kwa Yule anayetumiwa,mtumaji akatwe tozo,siyo haya mazingaombwe.
Hapana wazo lako haliko sahihi, mtumaji ndo hapaswi kukatwa kodi, hii ndo inaitwa double taxation, miamala inayotakiwa kutozwa kodi ni ile ya kutoka fedha kwa wakala, make anayetoa pesa kwa wakala anahesabika ndo final consumer, na hiyo ndo misingi ya taxations
 
Naona kabisa hapa serikali imepunguza viwango kwa shinikizo toka kwa wananchi, lakini kama vitu vingine bado hawajavigusa kama mafuta ya kupikia, gas na mengine.

Nadhani watatafuta sehemu nyingine wakafidie hilo pengo, serikali isimkandamize mwananchi wa kawaida, ibuni na kusimamia vikubwa tulivyojaliwa na Mungu.

Nashauri serikali ingebaki na hivyo viwango vipya bila kuongeza pengine.
Kumbe hufahamu sababu ya mafuta ya kupikia na gas kupanda bei unailaumi serikali
 
nimekasirika sana kwa TOZO kupunguzwa.
nilikuwa najisikia fahari sana kwa mapato yaliyo kuwa yanakusanywa, haswa baada ya kupatikana zaidi ya 40billion, lkn basi kwakuwa wameamua kupinguza wacha kazi iendeleee.
 
Hii serikali isiyofuata sheria zake ni serikali ya ajabu sana; kama sheria ilipitishwa na Bunge iweje Waziri wa fedha aibadilishe kienyeji kwa maelekezo ya rais tu? Utaratibu ni kuwa atayarishe muswada mpya wa kuirekebisha na kuupeleka Bungeni. Halafu swala siyo kupunguza kodi tu, inabidi bajeti nzima ifanyiwe marekebisho, kwani bajeti hiyo pamoja na mambo mengine ilitegemea mapatao yatokanayo na kodi hiyo ya miamala.
Hahaha elimu ni tatizo hufahamu kuna kitu kinaitwa kanuni? Ndio maana kuongoza watanzania ni kazi watu hamjisomei unakariri tu, waziri apo kabadilisha kanuni
 
Kwahio Punguzo hilo, litakuwa ni Ongezeko la Asilimia ngapi kutoka tulipokuwepo Awali....

Hii inanikumbusha story ya ukitaka kumchemsha chura ongeza moto kidogo kidogo..., ila huenda hapa ni kuweka moto mkali kuliko ili ukipunguza kidogo mtu aone ahueni ila kumbe bado ni moto mkali
Hii imekaa sawa na Inaonesha ukomavu kuliko upupu aliouandika kwa kukurupuka Salary Slip kama kawaida yake Tozo za Miamala: Serikali yapunguza viwango kwa 30%. Watoa huduma za simu waridhia kupunguza 10%
 
Nchi INAJENGWA na watanzania wenyewe......

Tulijenge taifa letu kwa hizo TOZO na KODI MBALIMBALI....👊

#NchiKwanza
#SiempreJMT
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesaini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya kutuma na kutoa Fedha na kupunguza viwango vya tozo kwa 30%

Pia Serikali imejadiliana na watoa huduma za simu ambao nao wameridhia kupunguza viwango vya tozo wanazotoza kati ya mtandao na mtandao mwingine kwa 10%

Viwango vilivyopunguzwa vitatangazwa rasmi Septemba 01, 2021

Taarifa Kamili:

View attachment 1918332
Ni usanii tupu hakuna jipya
 
nimekasirika sana kwa TOZO kupunguzwa.
nilikuwa najisikia fahari sana kwa mapato yaliyo kuwa yanakusanywa, haswa baada ya kupatikana zaidi ya 40billion, lkn basi kwakuwa wameamua kupinguza wacha kazi iendeleee.
Wapunguze matumizi kama kununua mashangingi, kulipana posho za kukaa pale Mjengoni na anasa nyingine nyingi.
 
Umeshawahi kukutana dukani unakuta nguo imeandikwa bei ya kuuza 9.9 Tsh utasema sio mbaya lakini ikiandikwa 10 Tsh unaweza kusema ghali lakini kiuhalisia ni ileile tu. Waziri kusema 30% je ni 30% ya kiasi gani maana number kubwa unaweza kusema punguzo kubwa lakini ukweli bado ni juu sana makato sana tu. Lazima waseme 30% ya ngapi tunaweza kujikuta tunafurahia shilling 500 hii kodi haikutakiwa kabisa maana VAT ipo hii ni double taxation.
 
Back
Top Bottom