TPDC yaingia mkataba na Kampuni ya Uingereza ya Baker Botts kwa ajili ya ushauri wa Kisheria

TPDC yaingia mkataba na Kampuni ya Uingereza ya Baker Botts kwa ajili ya ushauri wa Kisheria

Profile ndio kitu gani?

Tunaongelea vitu vya msingi hapa wewe unaleta ushambenga.

Profile yao iwe kubwa ama ndogo inatuhusu nini sisi Watanzania?

Hii mada huiwezi, kajadiliane huko Instagram na kila Shilole.
Nadhani hata hujui maana ya Transaction Advisor ndio maana umeamua kupiga kelele tu
 
Zile zama za makampuni ya nje kupiga hela kwa mgongo wa ushauri zimerudi.

TPDC imeingia mkataba ya kampuni ya Uingereza za Baker Botts kwa ajili ya ushauriwa kisheria kwenye mikataba ya gesi....
Jamani tuache ulimbukeni wa kuona kila tunachofanya na kampuni za nje tunapigwa. Haya mambo ya onshore LNG au Offshore LNG bado hatuna uzoefu wa kutosha.

Kuna uwezekano tumesomesha watu kwenye maeneo hayo, lakini hawana uzoevu wa kuingia mikataba mikubwa ya kimataifa inayohusisha mabilioni ya dola. La muhimu, ni kuhakikisha maslahi ya nchi yanawekwa mbele, na nchi inafaidika fairly
 
Kila binadamu ana mapungufu yake na mema yake . Kwa kutetea rasilimali za umma kwa manufaa ya umma wa watanzania hayati JPM alikuwa mstari wa mbele....
Ndio dunia ilivo, sasa kitu hukijui ufanyaje? Kwahiyo ufanye maamuzi tu kwa kitu usicho kijua?. Kwanini ulienda shule wakati una mamlaka ya kufanya maamuzi yako? Kwa nini ulilipa kupata elimu?
 
Zile zama za makampuni ya nje kupiga hela kwa mgongo wa ushauri zimerudi.

TPDC imeingia mkataba ya kampuni ya Uingereza za Baker Botts kwa ajili ya ushauriwa kisheria kwenye mikataba ya gesi...
Sasa sijaelewa hapa, maana hii kampuni ya wingereza ndio mshauri wa Tanzania wa mikataba ya Gesi na Mafuta wakati wabia wetu ni hao hao nchi za kibeberu, British Gas, Shell etc.

kutakuwa na ushauri wa dhati kweli wakati mshauri ana conflict of interest, hata kama amedeclare kwenye makaratasi kuwa hana? yale mambo ya local content,16% undilluted shares za government etc
 
Sasa sijaelewa hapa, maana hii kampuni ya wingereza ndio mshauri wa Tanzania wa mikataba ya Gesi na Mafuta wakati wabia wetu ni hao hao nchi za kibeberu, British Gas, Shell etc.kutakuwa na ushauri wa dhati kweli wakati mshauri ana conflict of interest, hata kama amedeclare kwenye makaratasi kuwa hana? inafikirisha
Mkuu wenzetu kuna professionalism ya ukweli kwa kuwa tu wametoka nchi mmoja ndio useme kuna conflict of interest?
 
Ndio dunia ilivo, sasa kitu hukijui ufanyaje? Kwahiyo ufanye maamuzi tu kwa kitu usicho kijua?. Kwanini ulienda shule wakati una mamlaka ya kufanya maamuzi yako? Kwa nini ulilipa kupata elimu?
Haiwezekani Taifa la watu 60 million likakosa mtaalam wa maswala ya oil and gas.

Kuna taasisi inaitwa PURA kwanini wasitumie wataalam toka huko.

TPDC yenyewe inawataalam wa sheria waliosoma UK maswala hayo hayo ya oil and gas.

Kwanini wasiwatumie??

Kuchezea fedha zetu bure.
 
Makamba hafai kwa lolote serikalini, asiuhadaa umma wa watanzania. Hakuna kitu kitabadilika chini yake zaidi ya kuongezeka kwa matatizo. Acha aendelee kuuficha ukweli ila muda utaweka bayana ndipo huyo aliyembeba atamtua kwa uzito atakao mpa.
Tuwekeee ubaya wa Makamba hapa ,vinginevyo unapiga tu kelele zinazotokana na ushambabna uwivu pia (shame)
 
Haiwezekani Taifa la watu 60 million likakosa mtaalam wa maswala ya oil and gas.

Kuna taasisi inaitwa PURA kwanini wasitumie wataalam toka huko.

TPDC yenyewe inawataalam wa sheria waliosoma UK maswala hayo hayo ya oil and gas.

Kwanini wasiwatumie??

Kuchezea fedha zetu bure.
Mkuu nadhani hujaelewa scope ya kazi yenyewe ,unadhani TPDC wangetangazi kazi husika kama wangekuwa na uwezo nayo ?
 
Mkuu wenzetu kuna professionalism ya ukweli kwa kuwa tu wametoka nchi mmoja ndio useme kuna conflict of interest?
Hiyo mikataba ya huko nyuma tulionyonywa haikuwa na proffessionalism?.kwenye suala la kuloot rasilimali nchi za kibeberu zipo pamoja sana.Ndio maana Mwendazake alipofanya reforms kwenye milki na uendeshaji wa haya makampuni eg.madini alipigwa vita mpaka kususiwa misaada.
 
Haiwezekani Taifa la watu 60 million likakosa mtaalam wa maswala ya oil and gas.

Kuna taasisi inaitwa PURA kwanini wasitumie wataalam toka huko.

TPDC yenyewe inawataalam wa sheria waliosoma UK maswala hayo hayo ya oil and gas.

Kwanini wasiwatumie??

Kuchezea fedha zetu bure.
Si tetei ila tr 70 ni hela nyingi sana ku gamble, hao ulio wataja wana uzoefu wa maswala ya gas kiasi gani. Hao tpdc zaidi ya kununua crude oil wana jua vipi uchimbaji na usindikaji wa gas?
 
Si tetei ila tr 70 ni hela nyingi sana ku gamble, hao ulio wataja wana uzoefu wa maswala ya gas kiasi gani. Hao tpdc zaidi ya kununua crude oil wana jua vipi uchimbaji na usindikaji wa gas?
Tuna taasisi inayoitwa PURA ambayo majukumu yake ni kuishauri serikali na waziri katika mambo kama haya.

Sasa kuwapa wazungu majukumu ya PURA ni kuzidhalilisha taasisi zetu wenyewe na pia ni matuzi mabaya ya rasilimali fedha na watu.

Back
Top Bottom