TPDC yaingia mkataba na Kampuni ya Uingereza ya Baker Botts kwa ajili ya ushauri wa Kisheria

TPDC yaingia mkataba na Kampuni ya Uingereza ya Baker Botts kwa ajili ya ushauri wa Kisheria

Yaani ingekua vizuri iyo mikataba ingekua na uwazi, tusome wananchi wote kupitia mitandao au gazetini. Tujue nini.

Unaweza kuta iyo kampuni consultation fee tuu inayopokea ni robo tatu ya bajeti yetu ya dawa.

Hii nchii ccm sijui tuliwakosea nini
 
Makamba ameingia na upigaji wa aina yake!
Lango liko wazi,watu wanajipimia tu!
 
Local firm gani ina uzoefu na mikataba ya Gesi?

Vitu vingine ni bora kutafuta msaada kuliko kuleta ubish halafu tuangukie pua. Hawa kina Rex Attorneys na Mkono Advocates walikuwa wanaiwakilisha TANESCO na kila siku walikuwa wanakula knock out kwenye kesi.

..Mkono Adv walikuwa wanakodi mawakili wa nje kuiwakilisha / kuitetea Tanesco.

..Kila upande unakuwa na mawakili waliosajiliwa kutetea mashauri ktk mahakama ambayo kesi husika inasikilizwa.

..Kwa maana nyingine Mkono Adv wanakodi mawakili wa " kibeberu " na wanaoshtaki nao wana mawakili wao wa " kibeberu. "

..Na kila upande unakuwa umeahidiwa DONGE NONO ikiwa utapata ushindi.

..Ukiona Tanesco imeshindwa huko nje ujue kuna mahali walikosea au walivunja mkataba.

Cc Pascal Mayalla
 
Hao mnaowaita mabeberu ndio wanaoendesha shughuli za nchi nyingi duniani.

Hizi kampuni ni kama kampuni nyingine.... ziko kufanya kazi. Changamoto ni kwako mtoa kazi, umeweka vizuri nini unataka? Utapimaje mafanikio ya kazi uliyoagiza ifanyike?

Leo hii sehemu kubwa na uchumi Middle East wameshika wazungu, hata CEO wa Dubai Airport ni Mwingereza, President wa Emirates Airlines ni Mwingereza. Ingekuwa hapa kwetu tungesema amekuja kuua shirika letu ili British Airways inufaike.
 
Mkono Adv walikuwa wanakodi mawakili wa nje kuiwakilisha / kuitetea Tanesco.
Ni kweli kabisa, Mkono wenyewe walikuwa wanatumia British Lawyers, lakini Watanzania wasiojua eti wanadhani "Mzalendo" Mkono anaenda kwenye kesi kama yeye.

The bigger point, ni kwamba kama kuna kitu hatuna ufundi nacho, tutafute wanaoweza kutusaidia.
 
Amewekwa pale kimkakati. Subiri biashara ya ma-generator ianze. Wasomi wa Kitanzania hawana chao tena.

..watakula kwenye sgr, jnhpp, na lng.

..hiyo ni miradi ya matrilioni na hawawezi kutoka mikono mitupu.
 


Yaani nimemsikiliza waziri mpaka mwili umenisisimuka.

Hivi nyie watu mnajua ya kwamba Professor Muhongo hayo mambo anayoyaoengelea waziri ndio aliyoyapigania hadi kupitishwa kwa sheria za hati ya dharura ambazo wawekezaji awakuzitaka.

Zitto akatumika na CDM kufuata mkumbo kuzipinga.

Dah si hata mimi naweza ishauri serikali kwenye mambo hayo. Yaani hawa watu ukiwasikiliza wana uwezo mdogo kweli.

No wonder kuna watu wanamchukulia mtu kama Professor Muhongo poa, even I accept dakika za mwisho kawa mtu wa ovyo baada ya kuingia CCM.

Lakini alichokuwa anapigania Muhongo alipoletwa na JK ndio icho anaongea waziri leo kwa kutafuta msaada wa nje. But then hayo mambo Muhongo kayaweka kwenye sheria ya hati za dharura ambazo wawekezaji awakuzitaka.

Very sad
 
Miaka 60 ya uhuru hatuna law firm ya kuiamini? Pale jalalani anapotoka kabudi kumbe ni jalalani kweli.
Mkuu nakuomba tu upitie wasifu wa hiyo kampuni ya Baker Botts ndio utajua maana ya law firm infact wanasheria wetu ni kwa ajili ya kutafsiri vifungu ,hatuna wanasheria ambao unaweza sema ni commercial lawyers .Leo wansheria wetu wasipopewe standard draft contract hawezi andaa mkataba wa kibiaashara
 
Hao mnaowaita mabeberu ndio wanaoendesha shughuli za nchi nyingi duniani.

Hizi kampuni ni kama kampuni nyingine....
Mkuu,tatizo kubwa hapa jamii forum wengi wanajua kulaumu tu na kwa kuwa kwa zaidi ya miaka kumi walilishwa sana matango pori na uwelewa wao mdogo basi ni shida tupu .Ni maajabu sana wanapinga hata issue za kitaalamu
 
Back
Top Bottom