TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

Mkuu huogopi kuuziwa mbuzi kwenye gunia?, maana ndo tatizo kubwa ambalo wengi wanalikimbia kununua magari bongo
Gari ambazo ni mtori ni zile za bei ya chini ya 7.5m!

Utakuta labda namba ni ya miaka kibao nyuma. Which means imetembea sana bongo na ishapitia sana mafundi.

Ila ukinunua gari ya usajili December last year au usajili wa February mwaka huu ambazo zinauzwa 8-9m kwa sasa kwa zile economical kama RAUM, IST, VitZ n.k huwezi kuta gari ni mbovu. Labda anaekuuzia awe ni mtu asiyejua nini maana ya gari na hela zake ni za kuunga unga.

Cha muhimu ujue gari.
 
Sure!
 
nunua tu hapa hapa bongo utakachopata ndo bahati yako
 
Acha kuleta theory zisizokua na msingi tunalize ubishi huu nenda beforward.co.jp angalia gari inaitwa VW Jetta ya 2009 au 2010 utaona CIF yake ni kuanzia $3000-4000 lakini ukija lwenye calculator ya TRA CIF iliyowekwa ni $9000 ambayo inaleta kodi ya 18,500,000 sasa hapo unasema evidence zipi zinatakiwa kuletwa ? Proof of payment? Commercial Invoice ? Wakati hizo documents zote haziwi attached kwenye TANCIS?
 
Lengo ni kuleta unafuu kwa mwananchi wa kawaida.
Serikali ikiendelea kutafsiri umiliki wa gari ni anasa,hapo imemnyima mwananchi fursa ya unafuu wa maisha.
Inaonekana,wataalamu wanaogopa kusema ukweli,kuwa ukipunguza idadi na viwango vya kodi katika uingizaji magari nchini,magari yataingia kwa wingi na Serikali itapata kodi na tozo nyingi katika ununuzi wa mafuta.(Waliondoa tozo ya 'Road licence' kutozwa kwenye magari na piki piki,na sasa Serikali inapata zaidi katika ununuzi wa mafuta bila ya mwenye chombo cha moto kuona kero!!!).

Ujasiri,na ubunifu na uelewa wa watoa maamuzi wameshindwa kufahamu kuwa 'Ruhusu wananchi wamiliki magari kwa wingi,ili upate kodi kubwa wakati wananunua 'Petrol au Dizeli'

Visingizio kuwa hatuna barabara,na kutafsiri gar sio muhimu ,dhana hii imeendelea kukwamisha vichocheo vya maendeleo,na kumfanya mwananchi kujitafutia maendeleo binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…