TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

TRA, inakuwaje ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari lenyewe?

Bei ya gari huangaliwa ikiwa mpya.... then mahesabu ya depriciation hufuata... HATA UKIPEWA BURE, KODI UTALIPA... Gari ya mwaka gani? Brand gani? Ikiwa mpya inauzwa shilingi ngapi? Bei ya sasa ni shilingi ngapi? CC ngapi?
Hueleweki
 
Kama wanaona magari ni anasa mbona wao (wanasiasa wa Ccm) hawaachi kutumia hizo anasa?
Hapo ndipo mnakoseaga kila sehemu mnaingiza michadema na miccm yenu. Ushawahi ona Mbunge Wa upinzani anatetea hili? Wote ni wachumia tumbo tu kwa taarifa yako hawakuwazii wewe,wanawawazia mademu zao,familia zao tu. Wewe wanakutumia kama mtaji Wa kufanikisha azma yao
 
Magari mengi sana ya ulaya washamba waliojazana hapo tra wanaya-overrate kwenye kikotoo cha depreciation yanafika hadi huko
Sio kweli,umeongea kishabiki sana. Hakuna gari la million 15 lenye ushuru wa million 60.

Kikawaida yaan layman ushuru huwa sawa na CIF,mfano kama gari ni million 5 bas we andaa tu million 5 ya ushuru
 
Nimetumia kikokotoo cha TRA nimechoka kabisa, ushuru wa kuingiza gari ni mkubwa kuliko bei ya gari yenyewe
Magari maarufu yana kodi kubwa mfano Crown, Rav 4, Noah , Land Cruiser. Kuna magari ambayo sio maarufu kodi zake ni nafuu kidogo, hususan brand za kizungu.

Sent from my POT-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Hili suala linaumiza wengi sana. Nchi zingine kuingiza magari ni bei chee tofauti na tanzania....

Cha ajabu halizungumzwi bungeni, hapo ndio wanaponiacha hoi. Yanajali maisha yao na watoto wao, wengine waendelee kuteseka. Mkuu wengine wameshindwa kukomboa gari zao pale bandarini ushuru mkubwa sana.
 
State of demand and appropriate task, overfull demand- discarage customers, walisema tuna barabara chache kwahiyo wakiweka ushuru wa chini mtanunua sana magari,
Tatizo tunakimbia tatizo badala ya kulitatua. Kuzuia importation ya magarai kwa ku impose kodi kubwa ikiwa hamna kiwanda hata kimoja kinachozalisha magari nakuwa sielewi umuhimu wa hio protectionism policy!

Wangeweka road tolls kwa barabara maalumu wangepata hela nyingi tu ya kuboresha miundombinu ya barabara. Ungekuta gari ni nyingi ila road tolls zingeendeleza kupanua barabara.

Watengeneze autobahns za inter regions na za mjini ambazo zinalipiwa. Unataka fast track ya kwenda mjini. Lipia 5k checkpoint unapasuka hukai foleni hata kidogo. Unataka fast track ya kwenda mkoani lipia 10k checkpoint kwa gari below 3tonnes. Above lipa 30k. Kanuni ni kupasuka tu speed inayotakiwa sio chini ya 160km/h humo. Ukizingua fine au otherwise pita standard trac zenye matuta na speed limiter za enzi za ujima 50kph!

Badala ya kutumia masaa 8 kwenda Moshi watu wapasuke 4 hours, huko speed limit ni 160kph no bumps, ila walipishe hela kidogo kuitumia njia special kama hio. Ama kama huna hela utatumia standard road ndefu yenye kona nyingi na ma bumps.

Tatizo hamna ubunifu katika mambo ya kodi. Imagine ile sh.50 tunayoichangia kwenye kila litre ya mafuta kuna mtu analalamika?
 
Wanafanya hivyo ku-avoid tanzania kuwa dumping place
Kama ni hivyo mbona kwa mfano gari la 2005 ushuru wake mkubwa kuliko la 2004 (same make, model, cc, etc)!
 
Back
Top Bottom