TRA inazalisha mabilionea wengi kupitia wafanyakazi wake

Kuna kahasira kalikochanganyikana na wivu hapa hahaha.
 
Kuna dogo kashusha apartment kibao kisasa
 
inategemea na kitengo mkuu kuna watu wapo TRA ila wanateseka
Kweli inategemea na kitengo. Kwa mtu ambae hajawahi kufanya hapo TRA hawezi kuelewa hili. Kuna ma HR na watu wa Planning hapo TRA wana maisha ya kawaida sana. Maisha ya kutegemea posho na mshahara huwezi kuwa na ukwasi anaosemea mtoa mada.
Pesa zipo kwenye baadhi ya vitengo vyenye madili ya hela.
 
kuna mmoja ndo zake pale **********. yeye anapigaga tik-tak mishindoyake kufuta milioni 10 kwa ajili ya milion 3 haon tabu. wanazipiga kwa kweli
 
Maisha sio marahisi hivyo
Yangekua marahisi hivyo mbona karibia kila mtu ana-maisha mazuri

Miaka 26 huna familia, unamshahara above 2m, Saccos ya ofisi inakukopesha mara 20 sijui 25 ya mshahara wako kwa makato ya 5 years makato ni kidogo kidogo. Hapo kuna overtime, kazi za nje ya mikoa pengine kuna allowance za mafuta, makazi na bonus za hapa na pale.

Ugumu wa maisha unatoka wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…