TRA yadaiwa kuvamia Waturuki na kufunga Ofisi jioni ya Leo (Desemba 14, 2020)

Kuna jamaa mmoja alikuja kutembea kwetu kama mtalii mnyonge. Akaona fursa, akatafuta mkopo, akawekeza na sasa ana kampuni kubwa inayo ajiri watu wengi tu na ni mlipa kodi mzuri. Lakini ilimchukua muda na kujinyima sana mpaka kufika alipo sasa. Nadhani angekuja wakati huu angeisharudi kwao zamani sana. Na ndugu zetu wangeendelea kusota bila ajira. Wako wengi tu kama hao ambao wanaona fursa ambazo sisi hatuzioni na wana uwezo wa kuzitumia vizuri. Tusiwakatishe tamaa.

Amandla...
 
Kwanini wasilipe kodi?
Yawapasa kulipa kodi haraka sana kwa maslahi mapana ya taifa letu.
 
TRA wangalie namna bora ya kurecover wanachodai bila kuathiri utendaji wa anayedaiwa.

Hii imekuwa kama vita, hakuna vita, private sector should be encouraged.

Serikali haiwezi kuajiri graduates wote?? Hivyo it is very wise to deal wisely na wajasiriamali ambao wanaisaidia serikali kuajiri graduates.

Hii sio sawa.
 
Unapofuka kituo cha uwekezaji, unaeleza aina ya biashara na mtaji unaokuja nao. Vigezo vinayoonyesha wewe umejiandaa au ni tapeli. Kwa taarifa yako kampuni kama hizi ni za Watanzania wajanja wanaotafuta wawekezaji ama kuwauzia au kuingia nao ubia. Kosa lolote kabla ya muwekezaji kukamilisha taratibu zenu ni lako muanzilishi sio waturuki ambao hawajatambiliwa kisheria. Ati amekutwa mtanzania anayelinda mali Waturuki wako kwao, wanasubiri Mkopo unaofanywa na local bank😂😂 kukitokea queries, bank inasubiri walioko uturuki😃😃
 
Samahani nakutukana. Wewe huna akili kabisa na utakuwa masikini wewe na kizazi chako milele kwa akili hizo
 
Wewe hujui wakikopa kwenye Bank zetu, bank zinafanya biashara kubwa na kuingiza faida kubwa???

Hivi CCM kuwa kilaza na sifa ya kujiunga na CCM??
Yaani hao wawekelezaji wanataka mkopo waupate hapa hapa nyumbani, ndo maana wanyonge tunapigwa riba kubwa hata na benki za umma kama CRDB na NMB.
 
Kwa akili yako unadhani wawekezaji wanawekeza na hela zao za mfukoni????

Enyi watanzania ni nani aliyewaroga??? Hivi ujamaa ndo umewafanya muwe na akili za kipumbavu namna hii????

Kwa taarifa yako, duniani, hakuna kuwekeza ni genuine anayetoa hela yake mfukoni na anawekeza. Kwa practice ya Duniani almost kila mfanyabiashara anakopa Bank na kuwekeza. Kwa duniani Bank ni sehemu ya kufanya biashara ya hela, kukopesha na sio sehemu ya kuweka fedha. Amka kilaza wewe
 
Hapa sasa kosa lako.
Ingawa hoja yako ya msingi kuhusu TRA kuwa waelewa na flexible kea wafanya biashara upo sahihi sana.
Sawa linaweza kuwa kosa ni langu kuchelewesha kukabidhi barua ya kuwa nimefunga biashara,

ILa TRA ipo kwaajili ya nani? Hivi TRA huwa wanapita kwenye maduka kwaajili ya inspection maana wana physical adress, contacts za wafanyabiashara, TRA wanapaswa kuwatembelea wafanyabiashara na kuwajulia status za biashara zao kwa ufanisi mkubwa, basi pawe na team za kuzunguka mtaani na kukagua maendeleo na kupokea kero za wafanyabishara ingeleta feedback nzuri na kuongeza pato, na kwa kufanya hivyo wangejua pia biashara zilifungwa na zinazoendeshwa kihuni, zilizofungwa watawapigia simu kuwaita wahusika nakufanya nao mazungumzo kujua wapilo kwenye hali gani
 
Tax payers bill of rights ndiyo suluhisho la haya yote.

Mungu akulinde sana Lissu huko uliko.
 
Hapo unaingilia uhuru wa watu, mtu akichangia wewe waache waongee wanavyojisikia hapa ni uwanja wa hoja ukileta siasa ukileta hoja makinikia ni wewe tu as long hujavunja sheria, mtu anunue bundle bado mpangie achangiaje nini meku
 
Me bado nawalalamikia TRA kuongeza kodi ya leseni ya udereva toka 40,000 hadi 70,000 (75%). Mtu mzima nimetoka home na elfu 50, nikijua nalipa elfu 40 nabakiwa na hela ya kula, nakutana na bili ya elfu 70. Hivi TRA wanaona kila dereva ni tajiri eenh? Hawajui wengine tunategemea hizo leseni tupate mkate wa siku?

Mnatukamua kila sehemu hadi tutatoka damu badala ya maziwa
 
They dont care.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…