TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

Kwa kweli kama ulikuwa na mpango wa kuagiza gari inabidi utulie kidogo, vuta pumzi kwanza then sikilizia upepo wa kusi ukivuma kwanza, otherwise kaisari anaweza akaipiga gari mnada pale bandarini.
Acha tuu
Shida ni gari iko kwenye meli tyr kwa hesabu za zamani ushabajeti
 
Nachojua kuna 'CIF value' waliyonayo kwny mfumo wa TRA kwa kila gari

Na kuna 'actual CIF'/invoice price unayonunulia gari

on average CIF za TRA zilikua juu...ss sijui saivi wanakokotoa kwa actual invoice price ama ni wamerevise tu CIF values za mfumo wao
 
Kuna rafk angu majuzi kidogo afe
We subiria siku apewe assessment ya hio kodi kwenda kulipia uone
 
Wabunge gani hao? Hawa wa tume ya mahera au wale Covid? Sasa kila mtu atafahamu kwanini uchaguzi ulitakiwa kuwa huru na wa haki ili tupate wabunge waliochaguliwa na wananchi.
 
Principal ya kuzuia dumping ,ant dumping ni takataka useless kwenye modern economic kwa sasa sababu yakichakaa ukatwa screpa
 
Bei ya dizel zambia lita ni tsh 1200 japo yanapitia Bandari kwetu plus distance ya kuyasafirisha,nguo uganda bei rahisi Hali zinapitia dar
 
Hata alichofafanua hakifanani na taarifa inayosambaa yani kaongea ongea tu utopolo ili mradi aonekane kafafanua
Kodi inatozwa kwa umri wa gari wakati inaingia TZ na siyo siku ilipoanza safari au siku ilioagizwa. Wakati inaagizwa inaweza kuwa na miaka minane na ikafika bandarini ikiwa na miaka tisa. Kodi yake itakuwa kwa umri wake wa kuingia na siyo kuagizwa.

Umeona kipeperushi kilichokua kinasambaa??? Ambacho watu "wanadai" ndo bei zilizobadilishwa?(kodi)

Tuanzie hapo. Halafu kielezee kwa hayo maelezo yake
Hapana sijakiona. Hebu tuletee tulinganishe na hicho tulicholetewa.
 
Kodi inatozwa kwa umri wa gari wakati inaingia TZ na siyo siku ilipoanza safari au siku ilioagizwa. Wakati inaagizwa inaweza kuwa na miaka minane au tisa.

Hapana sijakiona. Hebu tuletee tulinganishe na hicho tulicholetewa.
Kuna mtu amekiposti kwenye comment yangu hapo juu
 
Pata picha sasa gari yako ndio iko kwny meli kuja Bongo unakutana na hio kodi ya Tsh. 31m,gari itaishia kupigwa mnada tu.
Hizi kodi siyo mpya. Zipo siku nyingi. Mtu wa kulaumiwa siyo Mpango bali Bunge. Mtu wa kumlalamikia siyo Mpango bali Bunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…