TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

TRA yafafanua ongezeko la ushuru wa magari

Hivi mtu anaposema bei halisi ana maana gani? Hizo bei za awali hazikuwa halisi? Bora angesema thamani ya shilingi au kupanda kwa bei ya magari hayo. Na kama hakuna badiliko then kwanini kodi iongezeke?

Ni kinyume cha sheria na uvunjifu wa katiba kupandisha kodi bila idhini ya bunge. Badiliko la kodi ni lazima liidhinishwe na bunge
Nachojua kuna 'CIF value' waliyonayo kwny mfumo wa TRA kwa kila gari

Na kuna 'actual CIF'/invoice price unayonunulia gari

on average CIF za TRA zilikua juu...ss sijui saivi wanakokotoa kwa actual invoice price ama ni wamerevise tu CIF values za mfumo wao
 
Mmmh ni rafiki yangu Sana sana, hela imekata nyingine hadi nimemkopesha, maana ana miradi mitatu yote nyokoo imemmalizia hela, anajenga ghorofa, Yuko kwenye michakato ya kuoa, na kaagiza na hilo dude Japan [emoji848][emoji134][emoji134] imagine hapo! Mwana lazima presha ipande!

Kibaya zaidi mi ndo nilipendekeza achukue huo mdude, maana magari hayajui vizuri na michakato yote nimemfanyia mimi ( ndo gari lake la kwanza) jana tulikuwa wote naona hana hata habari na mimi nimekausha ndinga ndo iko njiani inafika two weeks ahead...atalaumu kinoma[emoji848][emoji848]
Kuna rafk angu majuzi kidogo afe
We subiria siku apewe assessment ya hio kodi kwenda kulipia uone
 
Tuwakomalie wabunge wabadilishe hizi kodi za enzi za ujamaa kwenye magari. Japo unasema unalinda mazingira lakini kodi kubwa hivyo kwenye mtumba una viwanda vya magari?
Gari ni kitu kinachosaidia kukuza uchumi. Ingekuwa ni amri yangu ningeweka kodi karibu na sifuri. Kwenye magari ya kazi kama pickup na fuso watu wangenunua bila ushuru hata mia, ikiwezekana nawapa na hela ya asante😀😀

Kulalamika haya mambo haitusaidii kitu. Inabidi wabunge, wanasheria nk walifanyie kazi.
Wabunge gani hao? Hawa wa tume ya mahera au wale Covid? Sasa kila mtu atafahamu kwanini uchaguzi ulitakiwa kuwa huru na wa haki ili tupate wabunge waliochaguliwa na wananchi.
 
Principal ya kuzuia dumping ,ant dumping ni takataka useless kwenye modern economic kwa sasa sababu yakichakaa ukatwa screpa
 
Bei ya dizel zambia lita ni tsh 1200 japo yanapitia Bandari kwetu plus distance ya kuyasafirisha,nguo uganda bei rahisi Hali zinapitia dar
 
Hata alichofafanua hakifanani na taarifa inayosambaa yani kaongea ongea tu utopolo ili mradi aonekane kafafanua
Kodi inatozwa kwa umri wa gari wakati inaingia TZ na siyo siku ilipoanza safari au siku ilioagizwa. Wakati inaagizwa inaweza kuwa na miaka minane na ikafika bandarini ikiwa na miaka tisa. Kodi yake itakuwa kwa umri wake wa kuingia na siyo kuagizwa.

Umeona kipeperushi kilichokua kinasambaa??? Ambacho watu "wanadai" ndo bei zilizobadilishwa?(kodi)

Tuanzie hapo. Halafu kielezee kwa hayo maelezo yake
Hapana sijakiona. Hebu tuletee tulinganishe na hicho tulicholetewa.
 
Kodi inatozwa kwa umri wa gari wakati inaingia TZ na siyo siku ilipoanza safari au siku ilioagizwa. Wakati inaagizwa inaweza kuwa na miaka minane au tisa.

Hapana sijakiona. Hebu tuletee tulinganishe na hicho tulicholetewa.
Kuna mtu amekiposti kwenye comment yangu hapo juu
 
Pata picha sasa gari yako ndio iko kwny meli kuja Bongo unakutana na hio kodi ya Tsh. 31m,gari itaishia kupigwa mnada tu.
Hizi kodi siyo mpya. Zipo siku nyingi. Mtu wa kulaumiwa siyo Mpango bali Bunge. Mtu wa kumlalamikia siyo Mpango bali Bunge.
 
Back
Top Bottom