TRA yakusanya Trilioni 22 mwaka wa fedha 2021/22, Nauliza tena Nani kama Samia?

nyie ni watu wakusifia makusanyo wengine tunataka kujua makusanyo hayo yamefanya nini
 
Yaani ukielewa logic ya Economics huwezi uliza hayo maswali yako kwa sababu matumizi ya pesa za mikopo kwenye purchases ni sehemu ya hayo makusanyo..

Hizo pesa zimeingizwa kwenye mzunguko na hivyo kuchochea uchumi zaidi..
 
Ashukuru magufuri alijaribu kutengeneza miundo minu ameikuta nchi iko mahali pazuri aliyepokea toka mzee wa msoga aliikuta bot chungu hakina hela
Hauna taarifa sahihi. Rais Samia hakukuta fedha yeyote. Yale mambwembwe ya TASK FORCE na fedha za Plea bargain kutoka kwa walioitwa "mafisadi" zilikuwa zinawanufaisha Magufuli na watu wake. Miradi yote mikubwa alikuwa anajenga kwa kukopa toka mabenki. ya ndani na nje, huku akiwadanganya wananchi kuwa ni fedha za ndani.

Alichofanya Samia ni ku restructure miradi mikubwa ili imalizike kwa muda wa mbali bila kuleta stress kwenye makusanyo na matumizi. Ndiyo maana tunaona anaweza kuongeza mshahara wa watumishi wa umma na kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo.
 
Ukweli ni kuwa sasa fedha inapatika mtaani hivyo kuwezesha watu wengi kulipa kodi. Kwa mfano nilipo hapa kata ya Maskati Mvomero, mwaka jana muda kama huu debe la mahindi lilinununuliwa kwa mkulima kwa Tsh 5,000 lakini Leo ni Tsh 10,000, kwa Nini mkulima asiishukiru serikali yake? Wilayani Kyerwa mwaka juzi kg ya kahawa maganda ilininuliwa kwa Tsh 950 Leo ni 1650, hapo pato la mtu mmojammoja limeongezeka na raia watatumia huduma mbalimbali na kupitia Hilo tayari serikali inakusanya Kodi ya kutosha.
 
Ndio shida ya wahuni ata kutunga uongo awajui.

TRA imekusunya 99.2% ya budget yao; kwenye mikopo maza amepitiliza ata iliyopangwa kwenye budget.

Halafu waziri juzi tu ametuambia budget imefikiwa 78% kuna short fall ya 22% imesababishwa na nini kama source zote za budget makusanyo ni karibu na 100%.

In the mean time nchi imeongezewa risk ya ku default from low to moderate, imeshushwa uchumi wa kati na kupata non-concessional loans za miradi isiyofadhiliwa na WB imekuwa shida.

Ni sawa na kusema mshahara wako kwa mwezi sh million kumi lakini kila siku unaomba hela ya mafuta nyumba ya jirani; ni kujiongopea mwenyewe.

Watanzania wamewazidi uwezo wa kufikiri propagandist wa ‘bi-tozo; hadithi zao ni za kujitekenya na kucheka wenyewe not consistent with other economic variables.

You do know waziri wa fedha alielezea shortfall ya budget ikiletwa hapa hiyo speech ndio utaona kiwango cha upuuzi wa huyo Kidata.
 
Huyu ni mwajiriwa kodi za wananchi ndio zinamlipa mshara, hela ya matibabu,malazi , usafiri na kiinua mgongo akistaafu iweje iwe siri?
Mnaanza nongwa za kijinga badala ya kuwa wabunifu katika kutafuta riziki, fursa nyingi zimeshaachiwa.
 
Wakijibu nitag
 
Ndio hayo makusanyo ndo yanaenda kugharamikia ma v8 na kuwalipa mapdeiem ila kwenye miradi sijaona impact yake
 
Chuki imekuzidi
 
Ni ngumu Sana kufanya maandishi kuonekana hela
 
Ashukuru magufuri alijaribu kutengeneza miundo minu ameikuta nchi iko mahali pazuri aliyepokea toka mzee wa msoga aliikuta bot chungu hakina hela
Malaika wako wa Chato angekuwa na chungu kilichojaa hela angeenda kukopa credit suisse bank na kuiingiza nchi kwenye dhahma za kulipa mideni mikubwa kibiashara? Yule ni muharibifu wa nchi ndio maana alikuwa akitegemea kukwapua pesa za watu na na tax force yake.
 
This Lady Samia is too smart. Every sector now is moving and contributing to the national economy. The true meaning of balanced development.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…