Ukweli ni kuwa sasa fedha inapatika mtaani hivyo kuwezesha watu wengi kulipa kodi. Kwa mfano nilipo hapa kata ya Maskati Mvomero, mwaka jana muda kama huu debe la mahindi lilinununuliwa kwa mkulima kwa Tsh 5,000 lakini Leo ni Tsh 10,000, kwa Nini mkulima asiishukiru serikali yake? Wilayani Kyerwa mwaka juzi kg ya kahawa maganda ilininuliwa kwa Tsh 950 Leo ni 1650, hapo pato la mtu mmojammoja limeongezeka na raia watatumia huduma mbalimbali na kupitia Hilo tayari serikali inakusanya Kodi ya kutosha.