TRA yakusanya Trilioni 22 mwaka wa fedha 2021/22, Nauliza tena Nani kama Samia?

TRA yakusanya Trilioni 22 mwaka wa fedha 2021/22, Nauliza tena Nani kama Samia?

Huoni impacts au una shida mahala? Kipi huoni kama impacts?

Bajeti ya Serikali inapopangwa huo inaonyesha makusanyo na wapi zitatumika,kwa hiyo ni wajibu wako kufuatilia kama fedha zilitumika kama ilivyokusudiwa..

Kwangu mimi ni sahihi kwa sababu Kwa mujibu wa Bunge, serikali uliganikiwa kutekeleza bajeti yake kwa 95%..
Hapa dar es salaam hakuna hata kipande cha kilometa moja cha barabara mpya inayojengwa toka samia kuchukua nchi ....kama kipo nitajiwe ni kipi
 
Hauna taarifa sahihi. Rais Samia hakukuta fedha yeyote. Yake mambwembwe ya TASK FORCE na fedha za Plea bargain kutoka kwa walioitwa "mafusadi" zilikuwa zinawanufaisha Magufuli na watu wake. Miradi yote mikubwa alikuwa anajenga kwa kukopa toka mabenki. ya ndani na nje, huku akiwadanganya wananchi kuwa ni fedha za ndani.

Alichofanya Samia ni ku restructure miradi mikubwa ili imalizike kwa muda wa mbali bila kuleta stress kwenye makusanyo na matumizi. Ndiyo maana tunaona anaweza kuongeza mshahara wa watumishi wa umma na kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo.
Huyu CHAWA ajengewe haraka sanamu lake la UNAFKI kwenye kiburi la Mwamba JPM kule Chato.

Rais Samia hakukuta fedha yoyote [emoji736] wala si fedha yeyote [emoji777].

Je alitoa wapi pesa za kusafiria kwenda nchi za nnje kutafuta wawekezaji, kulipa mishahara na posho wafanyakazi/aliendeshaje nchi?
 
Huoni impacts au una shida mahala? Kipi huoni kama impacts?

Bajeti ya Serikali inapopangwa huo inaonyesha makusanyo na wapi zitatumika,kwa hiyo ni wajibu wako kufuatilia kama fedha zilitumika kama ilivyokusudiwa..

Kwangu mimi ni sahihi kwa sababu Kwa mujibu wa Bunge, serikali uliganikiwa kutekeleza bajeti yake kwa 95%..
Kwa mujibu wa bunge lipi?. Bunge la ndiyo mzee ndilo kwa mujibu wa bunge?.
 
TRA ieleze pia kati ya hayo makusanyo serikali imelipia kiasi gani kupitia wakandarasi walioingiza malighafi za ujenzi wa reli,bwawa la Mwalimu Nyerere,kodi kutokana na manunuzi ya wakandarasi kutokana na fedha ya mkopo wa COVID 19 ambao ulijenga madarasa na vituo vya afya nchi nzima...tunaweza kutoa sifa kama hizi halafu wananchi wasione impact ya makusanyo kwa sababu sehemu kubwa ya fedha imetokana na fedha za serikali yenyewe.

Wewe hujaona impact?
 
Hayo ni makusanyo kidogo sana kutokana na kodi walizoanzisha za kuwakamua wa tanzania ambazo ni kandamizi .pamoja na hivyo,kwa nini hatuoni mwendelezo wa miradi mikubwa kama sgr na bwawa la umeme (nyerere).kwa makusanyo hayo angalau yangeonesha matumaini ya hii miradi ya kimikakati.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huoni umeenda site?
 
point kubwa kabisa hii! huwezi kujisifu unakusanya kodi huku miradi mingi imesinzia hizo pesa zinaenda wapi. tujue tuanze kusifia serikali

Taja mradi uliosinzia. Badili mindset yako kupinga kila kitu sio akili
 
nyie ni watu wakusifia makusanyo wengine tunataka kujua makusanyo hayo yamefanya nini

Kuna websites na kurasa za mitandao ya kijamii. Kuna report ya bajeti ya mwaka wa fedha ulioisha kasome huko.
 
Jambo muhimu kwa raia ni ajira, mfumuko wa bei na ukuaji uchumi sio ongezeko la kodi.
 
Ndio hayo makusanyo ndo yanaenda kugharamikia ma v8 na kuwalipa mapdeiem ila kwenye miradi sijaona impact yake
Huwezi ona sababu ya kilema cha chuki ulichonacho..

Baki hivyo hivyo usione kitu ndio vizuri.. Mpumbavu unamuacha na upumbavu wake.
 
Kama watanzania watakuwa hawana maendeleo na kuishi kimaskini makusanyo hayo ni ujinga tu. Hakuna tofauti na kushangilia goli la kujifunga mwenyewe
 
TRA ieleze pia kati ya hayo makusanyo serikali imelipia kiasi gani kupitia wakandarasi walioingiza malighafi za ujenzi wa reli,bwawa la Mwalimu Nyerere,kodi kutokana na manunuzi ya wakandarasi kutokana na fedha ya mkopo wa COVID 19 ambao ulijenga madarasa na vituo vya afya nchi nzima...tunaweza kutoa sifa kama hizi halafu wananchi wasione impact ya makusanyo kwa sababu sehemu kubwa ya fedha imetokana na fedha za serikali yenyewe.
Hakuna kitu hapo , BAJETI 2022/2023 41 TRL , Makisanyo ya kodi TRIL 22 , Ifike mahali Serilikali ibuni vyanzo vipya vya ukusanyaji wa kodi , kwanini makampuni makubwa baadhi yao hayalipi cooperate taxes ?????Misamaha ya kodi ipunguzwe , ifike ,mahali nchi hii lazima ijetegemee maana hao wahisani wanakuja na masharti magumu kiasi kwamba huwezi kufanya naye fair negotiations ,(win win situation situation )naye akataka kuwekeza nchini .Wake up Tanzania tuna feli wapi?????????????/
 
Na jee deni la TRA kama VAT returns kwa VAT registered company's ni kiasi gani?
Maana usikute madeni yao nao ni ya kutisha kwa vile hawana desturi ya kurudisha fedha hizo
 
Kama watanzania watakuwa hawana maendeleo na kuishi kimaskini makusanyo hayo ni ujinga tu. Hakuna tofauti na kushangilia goli la kujifunga mwenyewe
Afrika bado Sana serikali kufanya maendeleo kwa mtu mmoja mmoja
 
Serikali haigawi pesa kwa watu, maendeleo ni nini kwa tafsiri yako?
1. Ajira na mishahara ya watumishi
2. Maji
3. Afya na Madawa
4. Barabara na miundo mbinu yake
5. Umeme
6. Elimu
7. Mikopo kwa vijana
8. Kusaidia kilimo na fursa zake za masoko
9. Scholarship za kitafiti na kielimu
10. Kusaidia wafanya biashara na wajasiriamali kujenga masoko na kutoa fursa kwao za kufanya biashara
11. Kujenga uwezo wa ndani kiviwanda,kibajeti na kuepuka mikopo tegemezi ya wahisani na taasisi zao nk.

Siwezi na sijasema tunataka fedha mifukoni ila huduma hizo serikali iziboreshe sana na iepukane na matamko yasiyo na tija kwa wananchi ikiwemo matumizi makubwa ya fedha kwa viongozi.
 
Nchi ngumu hii, tupunguze pambio, maana walamba asali walisema Magufuli aliua Uchumi na Biashara.Kwaiyo kwa makusanyo aya tuseme Mama kaimarisha Uchumi ulioharibiwa ndani ya miaka 5 kwa mwaka mmoja.
Huyu Kidata si ndiyo alivuliwa adhi ya ubalozi na leo ndiyo kapandidha makusanyo!!!!!
 
Back
Top Bottom