Cash Generating Unit
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 13,286
- 39,418
Kwa hyo tenga 27 Ni elfu 27.
Sasa mbona faini Ni milioni 3
Kosa la dereva hajampa mteja wake risiti ya kusafirisha mzigo
Mkuu haya maelezo yako hapa Wewe unachanganya hisia na sheria.Anayetakiwa kutoa receipt ni muuzaji au mnunuzi?
Huyo wa kwenda kwa mtendaji wa kijiji labda yule ambaye kununua labda hiyo kazi ya kununua bidhaa na kwenda kuuza ni ndiyo kazi yake mahususi lakini kwa mtu ambaye ni dereva wa Malori ya masafa marefu inakuwa si sawa.
Halafu ni kwambie kitu kwa mikoani huduma za serikali za mitaa ziko scattered kwa sana, Yani ukiwa eneo moja tena mashambani kuambiwa umtafute mtendaji ni mtihani mkubwa sana!
Usichukulie ni rahisi kumfikia mtendaji wa serikali ya kijiji kwa maeneo ya mikoani.
Elimu imetolewa sana na madereva wanajua hawatakiwi kupakia mzigo wowote ila wanaleta mazoeaFlexibility ni muhimu, watoe elimu, wanaleta uhasama na serikali
Ww sio mfanyabiashara kwa maana wafanyabiashara wote wanaelimishwa kuhusu utoaji wa RISITI. PUNGUZA UROPOKAJI.Flexibility ni muhimu, watoe elimu, wanaleta uhasama na serikali
Kwahiyo ukikodi GARI nani anapaswa kutoa risiti mwenye gari au anayesafirisha mzigo? Ww ukipanda basi TIKETI unatoa ww au MWENYE BASI NDIO ANAKUPA RISITI?Sheria ya EFD iko wazi anayetakiwa kutoa receipt ni muuzaji, wajibu wa mnunuzi ni kuidai hiyo fiscal receipt toka kwa muuzaji.
Tuanzie hapo halafu lete hoja yako maana sijakusoma vizuri.
Mteja wake ni Huyo mwenye tenga 27.Mteja wake ni yupi? Mbona sikusomi vyema ?
Sheria ya EFD iko wazi anayetakiwa kutoa receipt ni muuzaji, wajibu wa mnunuzi ni kuidai hiyo fiscal receipt toka kwa muuzaji.
Tuanzie hapo halafu lete hoja yako maana sijakusoma vizuri.
Ni chanzo cha rushwa, sidhani kama kila mtu anachajiwa, asipofika bei yao wana mchaji, just common sensr, nenda kariakoo usikie madudu ya TRA walivyokwamisha biashara. Tukubali TZ bado tuna operate kwenye informal economy, ndiyo maana rais wetu mwenye IQ kubwa aliliona jinsi chinga na mama ntilie wanavyochukuliwa vitu vyao na migambo akaleta vitambulisho,Elimu imetolewa sana na madereva wanajua hawatakiwi kupakia mzigo wowote ila wanaleta mazoea
Watu wengi humu wanaleta hisia sana badala ya kufata sheria. Wanamuonea Huruma kisa kabeba tenga 27 lakini wanasahau Dereva anajua ni Kosa kufanya hivyo.Kwahiyo ukikodi GARI nani anapaswa kutoa risiti mwenye gari au anayesafirisha mzigo? Ww ukipanda basi TIKETI unatoa ww au MWENYE BASI NDIO ANAKUPA RISITI?
Mkuu ukifanya hivyo magari yatapukutika barabarani. Madereva hawahusiki kwa lolote linalohusiana na matengenezo/tozo au malipo mbalimbali ya gari bali yanamhusu Mmiliki wake.Hili ni Kati ya masuala tata sana.
Kodi muhimu na kodi hii ipo kisheria.
Lakini upande wa pili wa shilingi kodi hizi kwenye usafiri wa mazao ya chakula utaongeza ugumu wa maisha na kushusha kipato cha wakulima wa mazao ya chakula, matunda na mboga mboga, maana madereva sasa hawatathubutu kubeba mizigo midogo kama hiyo njiani. Mazao yata waharibikia na masokoni kutakuwa na upungufu wa bidhaa kisha bei zitapanda kama ilivyo uzwa 1kg ya vitunguu kwa 10,000/- wakati wa Corona.
Lakini tujiulize, kama mwenye mgahawa anatakiwa atoe risiti ya EFD akiuza kitu cha chini ya 30,000 mfano kahawa cupuccino au juice au kuku nusu au Samosa(sambusa) kwanini mwenye kusafirisha mzigo na kutoza 70,000/- au 100,000/- asitoe risiti ya EFD?
Hapa madereva waongee na matajiri wao watembee na EFD na hii pesa ya mizigo ya juu kwa juu wapawe commission kubwa nje ya mishahara yao ili kuwaongezea kipato na kupunguza ugumu wa maisha.
Au
Njia ya pili ambayo mmiliki wa gari si lazima ahusishwe au ajue gari yake ilibeba mzigo wa juu kwa juu.
Kuwe na maafisa wa TRA ambao si wala rushwa wakikutana na mzigo kama huo wanakata kodi halali (yenye uwiano sahihi) kwa huo mzigo, wanatoa risiti ya EFD na gari inaendelea safari.
Kurahisisha zoezi hili na kuepuka udanganyifu wa madereva kuhusu bei walitoza kusafirisha mizigo inabidi TRA waweke vituo vidogo kama check-points au mfano wa vile vya maliasili barabarani kila Kijiji au umbali flani ambapo hapo wenye mizigo na madereva watapakilia hii mizigo na mbele ya hao afisa wa forodha.
TRA inaweza kuweka hata mawakala kwenye vituo hivi kupunguza gharama za kuajiri watu wengi.
Hakuna haja ya ku- centralize kila kitu.
Hivi vituo pia vinaweza kuwa kama vile masoko ya madini Kika wilaya.
Mkulima kazi yako kutoa mzigo wa mazao shamba na gari ndogo kisha kufikisha kwenye vituo hivi. Iwepo na miundombinu ya kusaidia baadhi ya mazao haya yasiharibike yakirubiria usafiri.
Serikali isihusike kabisa kupanga bei ya usafiri wa hii mizigo, hiyo iwe mapatano ya mwenye mzigo na dereva.
Nafikiri haya ndiyo mawazo yangu ambayo si lazima niwe sahihi.
Mkuu ndo mana nilisema Wewe unachanganya hisia na sheria . Chunga sana Hili jambo litakukost siku mojaMimi naona kama kuna wachangiaji huenda kuna jambo hatujalielewa vizuri.
1. Kuna tofauti ya dereva ambaye kazi zake ni kubeba hayo mazao ya kilimo toka mashambani na,
Mfano madereva wa Canters na mafuso ya makabichi toka Lushoto, viazi toka mbeya nyanya toka Moshi au Iringa , matunda toka Mheza n.k
2. Kisha kuna madereva wa masafa marefu waendesha semi trailers ambao wengine huenda kuvuka boda na kwenda nchi jirani .
Hawa mara nyingi husafirisha bidhaa za viwandani nyingine toka ng’ambo (durable goods kwa kiasi fulani) sababu Safari yao huwachukua muda mrefu sometimes.
Sasa aina ya dereva anaeongelewa ni wa aina ya kundi la 2. Hapo juu.
Huyo mara nyingi anapita barabara kuu tu hata watendaji wa vijijini huko ndani hawajui.
Amekutana na wachuuzi wadogowadogo jioni wamemwangukia anunue nyanya zao akawahurumia akanunua, alipowadai risiti wakamwambia hatuijui unaongelea kitu gani huku wakimwangukia anunue bidhaa zao , hapo ungekuwa wewe ungefanyaje?
Mzee hata bidhaa ya buku1 kama hujatoa risit unaadhibiwa alieiba simu na nguo wote si wezi tu?? Sheria haiangalii hvo[emoji28][emoji28]
Kwa nini kapigwa faini?Unachanganya mada,unachoeleza hakihusiani na nilichoandika,tafadhali soma tena vizuri.
Hapa sisi hatumuongelei mkulima anayekuuzia tenga mia za nyanya ndo akupe risiti , no Sio jukumu lake hiloHiyo ni kwa ambaye tayari ana vigezo vya kuwa na mashine ya EFD na tayari anayo.
Kumbuka sheria ya EFD inahusu wale wenye mauzo ya kuanzia milioni 10-14 unless uniambia sheria imebadilishwa kwamba kila muuzaji wa thamani yoyote kwa Mwaka hata 1000,000 anatakiwa kuwa na EFD mashine.
Tuwe makini ktk kujadili ili tusipotoshe watu.
Mkuu ndo mana nilisema Wewe unachanganya hisia na sheria . Chunga sana Hili jambo litakukost siku moja
Sasa TRA wakikumata huna risiti utawaambia niliwaonea Huruma wale wa kulima?????? Seriously Kabisa??????? Mkuu step up achana na hisia.