TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

Tunawambia hapa.. ilindeni hiyo SGR....
Wachawi washaingia kazini. Take Care..
 
TRC mmepata changamoto ila mna la kujifunza , sasa kaeni mkao wa kibiashara kuhakikisha umeme upo mda wote pamoja na ulinzi wa miundombinu .

Hujuma zipo kweli.
Kwenye ulinzi wawachukue Suma jkt wapambane na hao ngedere pori.......Hapa mfano tungekuwa na ugomvi na majirani zetu kama Kenya ama Uganda tungewasingizia wao ila hatuna ugomvi nao tunabakia kuwalaumu Ngedere
 
Ndomaana india wana treni za umeme ila nyuma ya locomotive kuna dizeli generator, naamini umeshajua kwa nini wameweka.

Kimbinyiko, shabiby, BM, Abood n.k haya mabasi ni ya vigogo wakubwa waliowahi shika madaraka makubwa ya nchi kuanzia spika, marais, wafanyabiashara wakubwa weupe kwa weusi mabasi haya na mengine yanayotamba ktk safari za dsm, moro, dom ni hatari sana kwa ustawi wa sgr hasa kwa safari za dsm moro hadi dom
 
Kidete mpk kilosa ni km 59km.
Sasa train kama lina battery kwa speed ya 160km/h linamaliza hizo km chini ya dkk 23 hivi.
Sasa battery linashidwa kitumza umeme wa dkk 23 kweli.
 
😀 😀 😀sababu umeme wa kuendesha ile engine ni kubwa sanaa huwezi uzalisha kwa kutegemea betri labda waweke na engine ya kutumia mafuta kama back up.
Hayana battery yale , battery zilizopo ni kuweka mabehewa taa isizime
 
Kwenye ulinzi wawachukue Suma jkt wapambane na hao ngedere pori.......Hapa mfano tungekuwa na ugomvi na majirani zetu kama Kenya ama Uganda tungewasingizia wao ila hatuna ugomvi nao tunabakia kuwalaumu Ngedere
Acheni ubinafsii,hivi aliyewafata bundi na ngedere ni nani
Waliyojenga reli ndiyo wamewafata hao maporini huko
Ambako ndiyo nyumbani kwao
Sasa muwafukuze waende wapi
Acheni ubinafsi nyie wanadam

Ova
 
Bundi wanasingiziwa tu
Kwani kipande cha Dar na Morogoro hawapo?
 
Kwenye ulinzi wawachukue Suma jkt wapambane na hao ngedere pori.......Hapa mfano tungekuwa na ugomvi na majirani zetu kama Kenya ama Uganda tungewasingizia wao ila hatuna ugomvi nao tunabakia kuwalaumu Ngedere
Hivi ngedere wanazurulaga usiku?
 
Waende wapi usiku wale wanatembea wakiwa wanaona usiku ni kujificha tu mara chache sana labda eneo lao liwe na uvamizi ndio utawaona kuhama usiku..
Sasa ngedere wamehusikaje kwenye uharibifu unaosemwa? Na kama wamedanganya kwa ngedere, nina sababu gani ya kuamini kuwa bundi ndo wamesababisha uharibifu?

1. Je waliwakuta bundi wamefia kwenye nyaya za umeme?
2. Wamewakuta ngedere wamefia kwenye nyaya za umeme?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…