Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dar es Salaam yawasili Moshi ikiwa na abiria 294, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM

Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dar es Salaam yawasili Moshi ikiwa na abiria 294, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM

Treni hiyo imewasili ikiwa na abiria 294 ambao wameipongeza serikali kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM baada ya usafiri huo kusimama kwa takribani miaka 21.

Source ITV habari!
Hiyo miaka 21,ni nani aliyekuwa ameusimamisha?
Sumu umemnywesha mwenyewe. Sasa hivi unampa maziwa ya kumtibu, unataka upongezwe!
 
Mabehewa 20 × abiria 80 = abiria 1600
Capacity 1600 - waliosafiri 294 = loss (1306 × nauli per person)

Tusikate tamaa tutangulize uzalendo tusafiri kwa reli yetu hata kama ni narrow gauge
Mkuu sidhani kama hao ndio wasafiri waliotoka Dar hao ni waliowasili Moshi. Kuna walioshukia Korogwe, Mombo Hedaru nk. Hivyo uwe unafikiria kidogo kabla ya kuandika.
 
Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dsm imewasili mjini Moshi saa 5 asubuhi na kupokelewa na maelfu ya wakazi wa Moshi.

Treni hiyo imewasili ikiwa na abiria 294 ambao wameipongeza serikali kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM baada ya usafiri huo kusimama kwa takribani miaka 21. Pia abiria wamesema usafiri wa treni ni wa uhakika na hakuna mambo ya kuchimba dawa au kula magengeni kama ilivyo kwenye mabasi.

Baadhi ya abiria wameomba kwa kipindi hiki cha sikukuu wawekewe miti ya Krismas na zile taa zake kwenye kila behewa.

Source ITV habari!
Mawazo mengine bana eti treni iwekewe miti ya Christmas, unadhani Wasabato na Waislam wanapionaje jambo hilo.

Stupid
 
Halafu kumbukumbu zikifutika vichwani utasikia eti Kaskazini tunabaguliwa katika awamu hii.
Hivi kaskazini inajumuisha mikoa mingapi? Na ndani ya mikoa hiyo kuna makabila mangapi?

Mana hoja nyingine zinazojengwa na upinzani sijui huwa wanazipanga wakiwa wamelewa au ndio uwezo wao wa kufiliri umegomea hapo?
 
Hii Treni ilihujumiwa na ccm na sasa wanajifanya kuifufua halafu wanataka wasifiwe hahaa mabingwa wa kutengeneza tatizo halafu kuja kulitatua kwa mbwembwe.
Ufipa mpaka leo hamna ofisi mmepanga kwenye kiosk kile. Shughulikieni shida zenu kwanza.
 
Huwezi kupongezwa kwa kusahihisha makosa uliyosababisha wewe.

Walioua reli ni watanzania na serikali yao hii hii chini ya CCM.

Kufufua bila kuwachukulia hatua yoyote ni kazi bure.

hii time BOMB huyu JPM akitoka kwisheni maana hakuna reference ya ya kumuogopesha aliyaharibu awali.

Kama mnataka reli hii isiharibiwe tena na basi JPM awepo bila kujali AWAMU na iwe strategy ya maendeleo na tukiomba Mola asiingilie kati kwenye afya yake.
 
Mabehewa 20 × abiria 80 = abiria 1600
Capacity 1600 - waliosafiri 294 = loss (1306 × nauli per person)

Tusikate tamaa tutangulize uzalendo tusafiri kwa reli yetu hata kama ni narrow gauge
Behewa zilizotoka Dar zilikua 9, kati ya hizo 1 ilikua ya mizigo, hivyo behewa za abiria zilikua 8, treni imetoka dar almost full, kuna watu wanaremka njiani na kupanda, na wale wanaokwenda Tanga huwa wanateremkia korogwe, pia kuzidi kukuelewesha, treni ni kama dalalada kila kituo inashusha na kupakia abiria na mizigo, abiria wa hivyo ni wengi sana njiani, mwisho ondoa fikra potofu huyo aliyetoa taarifa kuwa treni imefika Moshi na abiria 294 inawezekana ni kweli kwani sio ajabu hata mabasi yanayoingia Moshi kukuta yakiwa na abiria chini ya 20 wengi wakiwa wameteremka vituo vya njiani ikiwemo mwanga, himo, chekereni, nk nk nk. Taarifa za uhakika nilizonazo hadi muda huu ni kuwa treni toka Dar-Moshi ni almost full hadi Jan 1, sasa nyinyi endeleeni kujidanganya na taarifa fake za mtandaoni ila ukipata muda tembelea vituo vya treni moshi/dar ili uthibitishe ninayokuambia usisubiri taarifa pitofu za mamluki wa wamiliki wa mabasi ambao ndio adui namba 1 wa hii treni
 
Tehe tehe,pinga pinga hamkosi la kusema
Treni ipo fully booked mpaka 31 dec
Hakuna mchagga atakusikiliza wewe wakati anafika moshi kwa 15,000
Waendao moshi miezi ya december ilikua ni kilio na kusaga meno,hayo masaa ulioyataja ndio walikua wanayatumia kulala ubungo kusubiri basi lije halafu nauli ilikua 90,000
Kaka kunywa unachokunywa nakuja kulipa.
 
Hizo zote ni njama za kiprotoko ya chama ili kaskazini iunge juhudi
Treni ya kwanza ya abiria kutoka Dsm imewasili mjini Moshi saa 5 asubuhi na kupokelewa na maelfu ya wakazi wa Moshi.

Treni hiyo imewasili ikiwa na abiria 294 ambao wameipongeza serikali kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM baada ya usafiri huo kusimama kwa takribani miaka 21. Pia abiria wamesema usafiri wa treni ni wa uhakika na hakuna mambo ya kuchimba dawa au kula magengeni kama ilivyo kwenye mabasi.

Baadhi ya abiria wameomba kwa kipindi hiki cha sikukuu wawekewe miti ya Krismas na zile taa zake kwenye kila behewa.

Source ITV habari!
 
afadhali maana wachaga walikuwa wananisumbua sana kuazima prado langu kila desemba, bora wapande treni.
Konyo koza wee una prado?nitakuumbua wewe na kile ki paso chako cha red.wee jifanye tuu mjuaji kama sijakuanika hapa
 
Ukweli hata kama ni mchungu lazima usemwe ukiwa ndani ya ccm wewe kazi yako ni kupiga vigelegele tu.
Njoo na wewe ndani ya ccm kwani vigelegele vyako ni muhimu, unachangia huu uzi kwa kujilazimisha kwelikweli, pole sana.
 
Back
Top Bottom