Sisi hatuna ugeni. Vitu vyote vinavyofanywa na kusimamiwa na Serikali hii ya kwetu huwa havina perfection hata siku moja. Hiyo ndiyo kawaida ya miradi yote ya Serikali. Kukiwa na perfection ndiyo itakuwa ajabu.
Tulianzisha viwanda, viliishia wapi? Tulianzisha mashirika ya usafirishaji kwa kila.mkoa, yaliishia wapi? TANESCO utendaji kazi wake upoje? Hospitali zetu za umma, zipoje?
Watu wazoee tu, hiyo SGR itakuwa inakwenda hivyo hivyo, cha kuombea isipate hitilafu ya kuleta maafa. Hiyo kukwamakwama itakuwa ndiyo utendaji wake wa kawaida.