True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

...47
Nilitazama ile njia ya kwenda kisimani, nilishtuka kumwona paka mkubwa mweusi akinikata jicho baya mno.
Sijawahi ona paka kubwa kama hili, niliwaza huku nikiyakwepa macho yake mabaya kama ya bundi, ama ndo huyu anaekamata kuku? nilipo mtupia tena macho sikuamini, yule paka hakuwepo na badala yake bonge la bundi alikua pale ananitizama!
Nilishindwa kuvumilia, nilitimua mbio ndani kwangu nikafunga mlango na kukaa kitandani, jamani yaani uchawi njenje? Hapana bwana mie kesho lazima nirudi nyumbani, niliwaza huku hofu ikiwa imenikumba.
Muda kidogo majira ya kama saa 8 mchana alikuja yunge mkubwa akiwa na kisufuria kidogo alichokuwa amekijaza viazi vitamu na maziwa mgando!
Mbona umejifungia jua kali hivi? Aliuliza yunge.
Hiki kijiji chenu mie sikiwezi, naona kesho niende nyumbani tu, huku kutishana mie sipendi kabisa, nilimwambia.
Yunge: Nani kakutisha mchumba?
Nilimsimulia kila kitu, vituko vya bibi na babu mpaka kile cha paka na bundi.
Yunge: mhh! Kabla hujamwona bundi, hukushirikiana kitu na yunge mdogo?
 
Antonnia Tayukwa njooni
 
Hii ni chai,saa moja jioni kuku hajarufi bandani,saa moja jioni anaenda mashineni kusaga,mwezi december saa moja ni giza sana huko
 
WAJUAJI WAKIJA WATAKUULUZA

Mpaka sasa huyu bwana hajafikisha masaa 24 hapo ugenini kwa Babu yake kifupi alifika saa 12 na mpaka Sasa n saa nane mchana lakini sasa

👉Ameshajua kuku huwa wanakaa WAP mchana?
👉Kaonana na msichana jion nayeye akiwa mgen lakin usiku alimfungulia geto?
👉Saa 11 asubuh unasindika mtu ambae hujui kwao n wap na vp heshima yako kwenye mji husika ipoje?
👉Inakuaje we n mgen tena mjukuu ulipewa jina lababu alafu wote wanakuacha walijua we n mgen bila hata chakula Cha mchana?
👉Hukuwah kulala na msichana Ila mpaka sasa umeshalala nae na bado una shauku ya kupata mwingine.(mkojo wa kwanza kutoka kwa Mara ya kwanza huwa unakuchukua akili kwa aliyekukojolesha)
👉Unapata ujasiri gani kutoa nguo zako na shuka la Bibi yako liende kwenye mji usioufahamu ili Hali ulishataadhirishwa na Mambo ya ushirikina?
👉Muda n mchache Mambo n mengi.



Jamani achen mihemko hapa tupite Kama kuburudika na kuongeza kitu kichwan tusiwe serious Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…