True story: Nimeamua kumkataa mtoto rasmi

SEHEMU YA 6:


Pili, haikuwa busara tofauti zetu wawili zimuathiri mtoto, kutengana kwetu ilitosha kabisa kuwa adhabu kwa mtoto tusimuongezee mengine tusingekuwa tunamtendea haki kabisa.



NIMEAMUA KUMKATAA MTOTO RASMI
mtoto ambaye hakuwa wako.

Kuna mzee aliwahi kuniambia kuwa watu "wastaarabu na wapole ndio wanaongoza kulea shahawa zisizo zao".
 
Ni kweli mzee tatizo lilikuwepo nafikiri ndio lilinitibia tatizo unalozungumzia

"A man is monogamous by societal but Polygamous by Nature"

Utakuja kuwa huru kutoka kwenye vifungo vyako siku utakapo gundua kuwa unaisaliti asili ya jinsia yako.
 
"A man is monogamous by societal but Polygamous by Nature"

Utakuja kuwa huru kutoka kwenye vifungo vyako siku utakapo gundua kuwa unaisaliti asili ya jinsia yako.
Lilishaisha likaibua shida nyingine

Yaani ujinga wa mwanamke mmoja unasababisha wengine waishi na mimi kwa tabu sana

Kuna wanawake hapa watashadadia aliyofanya mwenzao hawajui pengine wanawachukia wanaume kwa ushenzi waliofanyiwa bila kujua sababu inaweza kuwa wanawake wenzao

Ogopa kuangukia kwa mwanaume mwenye historia zake huko atokako
 
mtoto ambaye hakuwa wako.

Kuna mzee aliwahi kuniambia kuwa watu "wastaarabu na wapole ndio wanaongoza kulea shahawa zisizo zao".
Sina upole wa namna hiyo
Mashaka juu ya mtoto sio wangu nilishakuwa nayo kitambo, lakini kutumia jina langu inanimilikisha moja kwa moja

Mimi naamini watoto ni baraka, hata ukipata mwanamke huko ametelekezewa mdirect kwangu nitamlea lakini asije kutokea mtu akasema ni mwanae baadae nitajifunzia uchawi kwake
 
mtoto ambaye hakuwa wako.

Kuna mzee aliwahi kuniambia kuwa watu "wastaarabu na wapole ndio wanaongoza kulea shahawa zisizo zao".
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Mkuu tuendelee comment utajibu baadae
 
Ukiona red flags mapema jitahidi kuuzuia moyo wako kuendelea kupokea shida, Fanya kukimbia tena kaa mbali sana na aina hiyo ya mtu.

Wala hakuna sababu ya kujiweka karibu naye ikiwa hata mtoto siyo wako kibaiologia.

Epuka kuwa kimbilio la Waasherati

Kasome Methali 5


 
akini kutumia jina langu inanimilikisha moja kwa moja

Kitu ninachotaka nikushauri ewe mwanaume mwenzangu ni kuwa "Women are the Maters when it comes to Manipulation"

Alikfanikiwa kukushika akili kwa kutumia jina lako kwenye jina la mtoto asiye wako, hata amekufanya usahau kuwa DNA haitoweza kusaidia kujua ukweli.
 
Mimi naamini watoto ni baraka, hata ukipata mwanamke huko ametelekezewa mdirect kwangu nitamlea lakini asije kutokea mtu akasema ni mwanae baadae nitajifunzia uchawi kwake
Sina uhakika na unacho kimaanisha hapa.

Utayari wako wa kulea mbegu za wanaume wenzako unaonyesha ni jinsi gani unahitaji msaada wa kuhakikisha unarudi kwenye lengo la kuzaliwa kwako kwenye familia yenu ambalo kimsingi ni kuendeleza uzao wa ukoo wa Mfukuza Ndoto,

Na sasa umeamua kujikita kenye kukuza na kuendeleza mbegu za uzao wa koo nyingine, tena unafanya hivyo kwa kujivunia zaidi.
 
SEHEMU YA 7:


Talaka ikatolewa baada ya siku 45, maisha yakaendelea na mwanamke huyu mwingine, nikahisi kuutua mzigo maana wakati alipokuwa ananibembeleza turudiane nikigoma anasema yeye ndo mke hata nifanyeje, ananitumia na picha ya cheti cha ndoa
Ikawa inaniudhi sana, kwamba mtu hakutaki lakini anataka tu kukukwamisha hasa kwa wivu tu kwa mwanamke mwenzie, hili la kunikwamisha kweli lilikuwa linaniwazisha mimi umri unaenda nahitaji kupikiwa kufuliwa na kuitwa baba lakini kuna mtu tu yuko somewhere ameamua kushikilia maisha yako
Nilikuwa naogopa sana kama nitashinda kesi yangu ya madai ya talaka ningefangaje na yeye najua hanitaki anataka kukwamisha tu na akishajua sasa sina cha kufanya tena ndio angeninyoosha vilivyo.

Lakini kwa kufaulu kwangu kumshinda mahakamani na talaka kutolewa sasa nikajiona maisha yanasogea kwa ahueni ya hali ya juu
Hapa ikaibuka changamoto nyingine, yule mwanamke niliyempata akawa ana-miss fire mara kwa mara, nina hamu na mtoto na kila akidaka ngoma inatokea kusikojulikana
Hapa ilifuata stori ambayo haina umuhimu sana katika mjadala huu lakini kwa ufupi ndio nikajua yoote ya tangu kabla na mpaka nilipoletewa zawadi nikazikataa, yote yalielezewa lakini sikuyatilia maanani kwa kuwa sikwenda huko physically nilisimuliwa tu.

Hapa sasa nikiwa na akili zangu timamu nikaanza kuishi nae kwa tahadhari sana, kuna wakati akanitumia akaunti ya benki anasema ni kwa ajili ya mtoto nikipata chochote niwe natuma huko, yaani amekaa amepanga mwenyewe akaamua kufanya hivyo bila kujadili na mimi, bila kujua kama kuna akaunti nyingine au vipi
Nilimjibu kwa ufupi tu "Watoto hawalelewi hivyo" hakujibu chochote tena
Nilishapigwa pesa ya kulea mimba sikuwa tayari kupigwa mara nyingine.
Tangu hapo kuna baadhi ya matukio alihitaji nichangie chochote basi hata kama ni elfu kumi tu aliipata kwa mbinde mno, sikumuamini tena.

Nataka hii stori imalizike haraka...
Niseme tu mimi ni muoga sana wa kutelekeza mtoto, hili sikutaka kabisa lije linitokee, so mpaka hapo bado nafsi yangu haikuridhika kwamba yule sio mwanangu, kuna wakati nikikaa akili inaniambia ni mwanangu.
Kikapita kitambo kidogo sina mawasiliano nao, nae kama kawaida akanyamaza tu.
Kimyaa, zaidi ya mwaka.

Kwahiyo mwaka 2019 mwishoni nikiwa humu nikapitia uzi wa mzee Iringa Native
Niliusoma kwa makini sana, ukanigusa, nikajihisi yanakwenda kunikuta hayo, ni uzi uliokuja kupigilia msumari ile dhana yangu ya kutokuwa na rekodi ya kukataa mtoto

Watu wanaweza kufikiri kwanini pamoja na yote hayo bado kuna wakati niliamini mtoto ni wangu, kuna vitu vingi pengine kwa kuruka makusudi au kwa kuvisahau viliendelea ambavyo vilikuwa vinanirudisha kwenye mstari sometimes.

Kuna wakati nikawa nahisi huenda ni kichaa cha mwanamke tu wacha nijishushe kwa faida ya mtoto mfano tukiwa poa namuuliza hivi mambo unayofanya mbona ni kama mimi sio baba wa huyo mtoto? Anajibu kama humtaki sema na akikua nitamwambia ulimkataa, acha kufikiria vitu usivyo na uhakika navyo?[emoji2307][emoji2307] Katika mazingira haya narudi tena kujaribu kuwa karibu na mtoto.

Kwahiyo uzi wa Iringa Native ukaamsha ari mpya maana nilikaa kimya kitambo sana ukizingatia tayari nilikuwa na mtoto ambaye ukimtazama huulizi, hata ukimuacha mtaani japo ni mdogo sana lakini watamleta kwangu... Sikuwa na munkari tena na watoto wenye mashaka mashaka ..
Nikapanga kumtafuta tena..

NIMEAMUA KUMKATAA MTOTO RASMI
 
Duh!! Mambo yanazidi kupamba moto!! Nafwatilia kwa ukaribu kabisa...
 
Reactions: T11
Nashuka na uziiiii nasubiri episode ya 7
 
Reactions: T11
Sio uchawi tuuu.. ni kumlima gharama za hatari ulizomlea mtoto.. ili aruke
 
Reactions: T11
sijutii kuufuatilia huu uzi, nikiwa mkubwa ntautoa na wangu coz unafanana na huu 4 sure..
 
Reactions: T11
Hayo nayo yataka moyo mkii..ila kitanda hichoo hakizai kharaaam..😄😄
 
Reactions: T11
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…