SEHEMU YA 5:
Mwenendo mzima wa BM, Mwenendo mzima wa ujauzito wake na mwenendo mzima wa kujifungua kwake na ushirikishwaji wangu kwake mpaka hapo ulishanipa mashaka sana
Kama mtoto ni wangu kwanini mambo yote haya yanatokea? Kama nilihudumia ujauzito mwanzo mwisho hasira zao/zake juu yangu zinatoka wapi? Bado haitoshi kunifanya baba wa mtoto? Iwe nimetoa mahari au sijatoa madhali sikukaa mbali na mimba kwanini nitengwe hivi?
Anyway wakati wa ujauzito nilijua labda hasira za mimba sasa mbona mambo yanaendelea mpaka baada ya kujifungua?
Taa nyekundu ikazidi kuangaza ndani ya ubongo wangu, isisahaulike stress ziliendelea kuniandama vilivyo, watu wangu wa karibu, ndugu na jamaa wakashangazwa na mabadiliko..lakini kwa mbaali nikaanza kuzisikia roumours kwa watu wakisema hali hii imepelekewa na kuachwa kwangu na mwanamke huyo, watu walijuaje? Nikaanza kunote kitu kwamba inawezekana yeye ndio anayasema haya kwa watu. Hali ilikuwa mbaya sana, najifungia ndani tu kama siko kazini. Huko ndani ni mimi na mitungi tu.
Kwa mara ya kwanza ni wakati huu sikupata usingizi, nilikuwa naweza kukaa macho tu tangu giza linaingia mpaka linapotea siku ya pili. Sikuutamani usiku tena, ni angalau mchana ningekutana na watu nikapoteza mawazo lakini giza likiingia nikabaki peke yangu ilikuwa ni mawazo mwanzo mwisho, mimi na mawazo, mawazo na mimi.
Ikafikia kipindi nikafreeze nikakaa kimya nikakubali matokeo, kwamba hapa sina changu tena. Kilichobaki ikawa kupambana kurudi katika hali yangu ya kawaida. Nilipambana sana mpaka angalau nikawa sawa kidogo.
Mwaka ukaisha, bila mawasiliano yoyote as if kule sina damu yangu, yaani hata simu ya bahati mbaya haikuwepo hapo nikaamini kuna mwenye mtoto anahudumia
Siku moja akanitumia meseji anasema nyumbani kwao wanataka kujua hatima yangu na yeye maana pako kimya tu. Nikapiga akili ya haraka nikaona huo ni mtego, kwao wanasubiri mimi niseme simtaki binti yao ili ionekane mimi ndio nilimuacha na kama kuna madai kwao nisidai, mimi nikamjibu hatima yetu alishaiamua yeye BM hapo kinachofanyika ni kunitega tu.
Kuna kitu akasema sasa kukaa kwako kimya ni kama namfunga yeye(maana yake ni iwapo anataka kuolewa kwingine nitoe go ahead) hapo nikajihakikishia huyu ana mtu mwingine sasa anataka kuolewa
Nikamjibu sijamfunga kama anataka kuolewa anaweza kuolewa tu maan mimi sidai kitu kwao biashara imeisha na kiukweli sikumhitaji tena hata bure.
Akauliza kimtego na mtoto je, nikamjibu nimewapa zawadi, akasema atawaambia yote hayo. Tukamaliza hivyo
Ikumbukwe ni mwaka sasa sijawahi kumuona huyo mtoto, sio mimi wala wazazi wangu.
Kiutaratibu baada ya kujifungua alitakiwa amlete kwangu nimuone, kisha awapelekee babu zake, kama mimi na yeye tulikuwa na matatizo angewapelekea hata wazee wangu, hakufanya hivyo. Na kwao wanaona sawa wala hawakujihangaisha kumshauri juu ya hilo.
Siku tuliyoongea hayo nikafuta na namba zake moja kwa moja, miaka ikakatika nikaja kusikia alipeleka kijijini mtoto akiwa na mwaka mmoja yeye akarudi shule, nikawaza sana huyu mwanamke wa aina gani? Mtoto wa mwaka mmoja kumpeleka kijijini kisa shule mbona shule zipo tu si angesubiri? Sikujali nikaachana nao
Ikawa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu, mtoto alishakuwa na miaka minne namsikia tu. Mimi nikaendelea na mambo mengine. Nikaanza kusikia kwa watu wa karibu vitu ambavyo ni kama kuna kitu huwa wanaongea nae kinachofanana na kurudiana na huyo mwanadada. Kuna jamaa yangu mlevi siku moja alilewa katika stori akasema utarudiana tu na mama fulani? Yaani BM nikamwambia kwa mapito aliyonipitisha haitawezekana
Akasema tutaona mtoto atawaunganisha tu, kusema kweli mtoto bado nilikuwa namhitaji sio mama yake .
Watu waliamini kweli naweza kumrudia sababu walijua nampenda sana sina ujanja, hata yeye alijua hivyo. Inasemekana hata alipoenda shule alijua mimi sina ujanja wa kumove on atanikuta tu, anakuja kumaliza shule anaanza harakati anakuta mimi nilishapambisha mapenzi kwingine.
Anyway baada ya kuanza kusikia kwa watu vitu vinavyofanana na kurudiana nikaanza kujiandaa kisaikolojia nilijua ni yeye tu anayasema haya. Kweli bwana siku moja akanitumia meseji yuko njiani anataka tuje tuonane, nikamwambia kuna tatizo gani? Akasema tutaongea akifika.
Nikamwambia haiwezekani akasema tuache tofauti zetu bhana turudiane tutunze mtoto. Halafu anaongea kirahisi tu kwa kuwa alijua mimi ni wake tu nampenda sana. Hakujua mambo yalibadilika kutoka mapenzi mpaka chuki.
Mpaka wakati huoa alikuwa ndio binadamu namchukia kuliko wote, yeye hakujua hilo
Kiukweli nilimgomea.
Alipofika akapitiliza chuo alichokuwa anasoma akadai anafuata cheti chake, mimi nikajiuliza huyu cheti alishachukua ni cheti gani amefuata? Nikanyamaza
Jioni hiyo ananipigia simu anajichekesha chekesha kisha akanipa mama mmoja niongee nae, nikaongea nao kidogo nikakata.
Huyu mama tangu akiwa anasoma walikuwa wanaitana mama wa hiyari, huyu mama ilifikia hatua akihitaji kitu ananipigia mimi niko mjini yeye bush namuagizia.
Kuna dhana nyingi zinatembea hapa, inawezekana huyu mama ndio aliwezesha mchongo mzima wa mimi kukamatika kirahisi, na sasa baada ya akili yangu kurudi sawa kwa kuona sielewi tena somo basi BM alirudi kujieleza ili mama afanye mambo tena..hizi ni dhana tu sina hakika ila zenye mantiki mbele ya safari.
Yaani ni kwamba BM alinipenda, alipofika miji ya watu akazuzuka hakunitaka tena, lakini kule nasikia alikuja kuachwa kwa fedheha ndio akanikumbuka mimi wakati tayari nimeshabumburuka nateleza tu kama kambale[emoji1][emoji1][emoji1]
Kuhusu mtoto hata kama sio wangu alijua ntaamini tu maana jina anatumia langu.
Alipotoka huko moja kwa moja akataka tuonane, mizimu ya kwetu ikacheza kama Pele nikagoma[emoji23][emoji23][emoji23](mimi niligoma tu kwa sababu zangu kumbe ningekubali nilikuwa nakwisha, haya niliyajua baadae)
Sababu ya kugoma nilimwambia wewe mtu wa ajabu una mtoto miaka minne sijawahi kumuona na unaona kawaida tu badala yake unataka tuonane mimi na wewe.
Akanibembeleza sana nikamwambia kama unataka kuonana na mimi uje na mtoto, maana yangu nataka kumuona mtoto sio wewe, akakubali
Safari hii hakuwa jeuri sana kila kitu anakubali tu.
Kesho yake akaja na mtoto sikutaka kuonana naye nyumbani kwangu nilimwita tu somewhere(Mizimu iliendelea kucheza part yake[emoji1][emoji1]nasikia ningempeleka home nilikuwa narudi kulekulee kwenye kukamatwa) Baada ya miaka minne ndio wanandoa wanakutana[emoji2307]
Naita wanandoa kwa sababu hatukuwa tumevunja ndoa kisheria lakini kimsingi hakukuwa na ndoa.
Akaja na zawadi fulani za vijijini ni aina ya chakula sitaitaja ilikuwa kwenye kapu.
Kuhusu kwanini tumeonana hapo na sio kwangu kuna namna nilimpiga kiswahili.
Baada ya kutulia umakini wangu wote ulikuwa kwa mtoto, nikamtazamaa, kusema kweli hakuna nilichofanana nae hata kimoja, wakati nakuja kuonana naye nilishaongea na bi mkubwa akasema ukiona hamfanani angalia kitu fulani, kweli wazazi ni wazazi aisee, ndio maana BM n wazazi wake walikimbiza mtoto walijua wazazi wangi wakimuona tu watajua wamepigw au hawajapigwa.
Sisi vijana unaweza kubambikiwa mtoto, sio mama yako, akimshika mtoto tu anajua kila kitu na ndio ilikuwa maana nzima ya kupeleka mtoto kwa babu na bibi zake tangu enzi na ndio sababu kupigana hakukuwepo sana hata ukipigwa ujue wamekutunzia siri kwa sababu maalum sio kwamba hawajajua.
Nilimcheki yule dogo hakufanana na mimi, nikajipa imani wacha nisimhukumu, mradi mama yake anasema mtoto ni wangu acha niwe mtulivu nikiamini kufanana sio ishu sana, basi bwana baada ya stori mbili tatu nikaona mtu anaenda kwa magoti ananiomba nimsamehe ulikuwa ujana utoto tu kama vipi tumalize tofauti zetu tulee mtoto.
Hapa utajiuliza ulikuwa utoto tu upi? Kunijibu dry? Kunitoroshea mtoto? Kunichukulia poapoa? Hapana hapa unapata jibu kwamba utoto wenyewe ulikuwa kupigisha nje. Na sasa kaachwa
Nilimwangalia tu sikumjibu nikamuinua, akajua yameisha si sinaga ujanja kwake.
Tukaendelea na maongezi baadae tukaagana, akataka kunipa ile zawadi kikapuni nikagoma[emoji23][emoji23][emoji23] mizimu ilichukua nafasi yake tena, sijui kwanini mwanzo ilinitelekeza, kuna sababu nilimpa ikabidi arudishe kwa dada yake
Inasemekana ningepokea ile zawadi sasa ndio nilikuwa namalizwa kabisa, sijui ni kweli maana haya naambiwa tu baadae kabisa tena na mtu mwingine kabisa sema mi sio mtu wa maimani inawezekana aliyasema kwa interest zake tu maana nae nina stori nae
Tunaendelea kuweka kumbukumbu
NIMEAMUA KUMKATAA MTOTO RASMI!