True story: Nimeamua kumkataa mtoto rasmi

Si kuna sehem alisema kua anahisi yawezekana mwanzo alifanyiwa mambo kidogo
Kuna mengine nayajibia kwenye comments na watu hawasomi
Lakini hili la imani lisipewe nguvu sana

Hili zigo la uzembe niko radhi kulibeba
Cha msingi tunaweka kumbukumbu na tunafundisha wengine
 
SEHEMU YA 8:

Kabla sijaendelea mbele kuna kitu nilisahau kukisema, ili kukazia hoja yangu kwamba mtoto sio wangu.
Tunajua kufanana kwa mtoto na mzazi sio lazima lakini je, inawezekana mtoto asifanane na wazazi wote wawili? Yaani hafanani na baba wala mama[emoji1][emoji1][emoji1] hapa nikajua kuna mtu wa tatu ndiye kafanana nae.

Tuendelee tulipoishia, Baada ya kupitia uzi wa Mzee Iringa Native akitafuta wanae na akionesha majuto ya hali ya juu ikaanza kama kunigusa gusa hivi, wakati nasoma ilikuwa 2019 december nikajiambia nitaanza mwaka kwa kuwatafuta hawa watu ili kama vipi niendelee kuhudumia mtoto.
Nikatafuta namba zake maana nilishazifuta kabisa, nikazipata nikampigia
Tukaongea tukaelewana, yaani yeye hanaga mpango na mimi hata nikikaa kimya miaka kibao, nikirudi ananipokea tu
Nikagundua huyu ananipokea ili anipige hela lakini masuala ya mtoto kuna mtu(Baba Mtoto) wanashauriana naye

Kufupisha tu stori baada ya kuwa nimejirudi na sasa nawasiliana nao vizuri nikamwambia nahitaji huyo dogo aje anitembelee nyumbani ili kujenga mazingira ya kujuana na nduguze nikapigwa chenga nyingiii baadae akakubali likizo atakuja kwa muda mfupi, lakini pia nikamwambia anatakiwa afike mpaka kwetu maana babu zake wananidai sana.

Kwa bahati nzuri au mbaya korona ikatuvamia hiyo 2020 mwanzoni, wakafunga shule, haraka nikamwambia kwa kuwa wana likizo ndefu sana naona nimchukie, nilipigwa chenga kali sana nikaambiwa sijui kachukuliwa na nani kwenda wapi sijui
Anyway nilichojua hapa nimekataliwa tu..sasa mimi baba yake nakataliwaje

Tutaendelea
 
[emoji23][emoji23][emoji23] jamani pooleee. Pole sana. Ndo huwa ilivyo. Mapenz ni upofu sikulaumu
 
Noma sana, huyu kiumbe alizaliwa maalum (special) kukutesa
 

Kwanini now watu wa JF mkianza kusimulia kitu mnaweka robo robo??

inakata stimu sana
 
SEHEMU YA MWISHO:


Naona niifupishe maana japo lengo halikuwa kuomba ushauri lakini naona kuna haja ya kuomba ushauri baada sasa ya kujivua rasmi.
Mwaka jana baada ya kupigwa chenga kwa lugha nyingi mara bibi yake amemchukua mara sijui yuko wapi nikakausha, siku moja nikampa somo zito juu ya umuhimu wa mtoto kuwajua nduguze ikiwemo kuwajua babu na bibi yake wa upande wangu, na kweli wazee walikuwa wananidai sana kwamba kama anatumia jina langu maana yake ni wangu kwahiyo wanataka awapelekee wamjumlishe kati ya wajukuu zao maana hawajamtilia maanani bado kati ya wajukuu walionao.
Hapo akakubali na akasema bwanaee kamchukue mi nimechoka
Nikamuuliza amechoka nini akasema amechoka kupiga chenga.
Inavyoonekana upande wao ni kama walikuwa wanakaza, nikimdai ilikuwa lazima aombe kwao wamkubalie sasa akawa amechoka huku namdai kule mpaka awaombe, kweli nikapanga weekend moja nimchukue lakini kutokana na shughuli zangu nikashindwa nikamwambia akipata muda ampeleke home mwenyewe.

Huyu BM sasa alikuwa amehama mkoa ule amehamia mkoa ambao wazazi wangu wapo ingawa wilaya tofauti, kwahiyo kutoka alipo mpaka kwetu ni masaa machache tu. Akakubali atampeleka akipata muda.

Sasa mwaka jana mwishoni akataka mtoto ahame alipo ambapo ni karibu na mimi ahamie kwake, na mimi ndio nilipendekeza hivyo baada ya kumdai sana kwanini hataki kukaa na mtoto, sio vizuri mtoto ana wazazi wote vijana tu halafu anakaa na mama mdogo sijui. Nimamwambia kufika mwisho wa mwaka jana asipomchukua namchukua hata kwa nguvu hapo akaogopa
Yeye hoja yake ni mtoto hawezi kukaa na mwanamke mwingine nikamwambia ntampeleka kwa bibi yake bado ana nguvu za kumlea, akaogopa akasema atakaa naye yeye. Kwa kuwa mimi ndio nilikuwa karibu na anapoishi mtoto akaniomba nifuatilie uhamisho shuleni, kweli nikafuatilia mtoto akatangulia uhamisho ukafuata..
Kabla sijakamilisha uhamisho akaanza visababu eti mtoto hataki kuishi huko aliko anataka abaki, nikamwambia amdanganye kama anaenda kusalimia tu atarudi, akakomaa nikamwambia hataki tu kukaa na mtoto ikabidi akomae akae nae.

Sijakaa sawa akaanza visababu ooh shule aliyopo sio nzuri imekaa pabaya kwa sababu kutoka nyumbani mpaka shule inabidi avuke barabara anahofia atagongwa nikamwambia watoto wengine wanavukaje akasema huyu mgeni nikamwambia atazoea kama wenzie. Akakosa cha kusema
Akaibuka na hoja nyingine hii shule hawajui kufundisha nikamwambia mhamishie shule nyingine akasema anataka shule fulani ina gari la kuchukua na kurudisha watoto kwahiyo tutakuwa tume-solve tatizo la hatari ya kugongwa na magari lakini pia atapata elimu nzuri halafu anataka mtoto ajue kizungu.

Hapa wafuatiliaji wafahamu kwamba pamekuwa na mjadala kabla mimi na huyo mwanamke juu ya namna ya kuwapatia elimu watoto, Tangu siku za nyuma nilishamwambia si kwa kukosa pesa au kwa kutojua umuhimu wa elimu lakini mimi binafsi sipendelei mtoto asome boarding katika ngazi ya shule hizi za chini iwe awali au shule ya msingi, sitaki mtoto asome shule za kishua hata kama sio boarding katika ngazi hizi za elimu
Nikitoa hoja kwamba mtoto atasoma changanyikeni huku chini halafu atasoma shule hizo za kishua ukubwani kama ni kizungu hakihitaji mtu kuanzia awali anaweza kukijua vizuri kabisa hata akikutana nacho chuo tu hata asipoenda chuo anaweza kujua kizungu.
Nikampa mfano wa wasanii wetu hawa wengine hata form four hawajafika lakini kwa kujua wanahitaji kujitanua kimataifa walijifunza na wanazungumza vizuri tu

Kwahiyo suala la kizungu halihitaji miaka bali nia na nilimueleza sio kwa mtoto wake tu bali watoto wangu wote watasoma kwa utaratibu huo.

Pamoja na hoja zangu zote hakuelewa, kama nilivyosema kabla yeye akiamua ameamua, habari ya ubaba haina maana kwake.
Juzi tumebishana sana nikamwambia mbona sasa ubaba wangu uko kwenye suala la hela tu lakini sina maamuzi yeyote ina maana hiyo mimba ulijitia mwenyewe? Akanijibu ndio maana unaambiwa mtoto ni wa mwanamke

Shuuubamiiiit!!!! Nikapanda jazba nikamwambia sababu ya mimi kila mara kujishusha ni kwa sababu mtoto anatumia jina langu bila hivyo nisingekuwa na habari, anachotakiwa kufanya ni kubadili hilo jina hatakuja kunisikia tena
Akaniuliza kwahiyo nakataa mtoto? Kwa mara ya kwanza nikamjibu ndio namkataa fanya nilivyokwambia sitakusumbua tena, akajibu sawa.
Nikakata simu, baadae nikapiga kuna jambo sikumalizana nae, hakupokea tena.

Hapa unajiuliza kama ningekuwa baba wa mtoto mbona nikisusa hajishughulishi yaani ni fasta tu anakata mawasiliano?

Nikajiambia sitajihusisha tena na huyo mtoto.
Kwahiyo wadau wa jamii forum kwa heshima na taadhima napenda kusema NIMEAMUA RASMI KUMKATAA MTOTO, wakati nafikiria kuandika huu uzi nilijawa na hofu nitasimangwa kwa kukataa mtoto, nilijipanga hasa kushawishi nieleweke kwanini nakataa mtoto, kwa bahati nzuri kabla sijamaliza uzi wananzengo wote wanaelewa kwanini nakataa na wengine wametambua kabisa namna gani nilibambikwa tu.
Kwahiyo kazi yangu imekuwa nyepesi.

TAMATISHO:
Kama nilivyosema hapo juu sikuwa na mpango wa kuomba ushauri lakini nimepata wazo la kuomba ushauri wenu wa kisheria juu ya haya;

1) CHETI CHA NDOA: Mahakama ilitoa talaka, nina hati ya talaka lakini kiutaratibu cheti cha ndoa kinabaki kwa mwenye ndoa, ni hati tu inajulisha ndoa imevunjika
Sasa mwenzangu nilipomjulisha nimeshavunja ndoa afuate hati yake ya talaka ikibidi achane kile cheti akajibu kwa nyodo hawezi kuchana kinamsaidia kwenye mambo mengi ikiwemo kuombea stahiki fulani fulani kazini
Lakini pia kilimsaidia kuhama mkoa mmoja kwenda mwingine, na kwa mbwembwe anakutumia na kapicha ka cheti whatsapp
Jambo hili linanikera naona ananitumia kwa faida yake je, naweza kumchukulia hatua za kisheria kwa kutumia cheti ambacho ndoa yake haipo? Hata nisipomchukulia hatua hawezi kuja kusumbua kughushi masuala yoyote hapo baadae wakati shuhuda nikiwa sipo?

2) JINA: Huyu mwanadada siku zote ni jeuri najua nimemwambia abadili jina la huyo mtoto kuondoa jina langu, na mimi sitaki tena atumie jina langu.
Nikibaini bado anatumia nimchukulie hatua gani kisheria?

MWISHO

NIMEAMUA KUMKATAA MTOTO RASMI!
 
Kutumia cheti cha ndoa ambayo imeshavunjwa kujipatia manufaa hapo kuna elements za jinai.

Kwenye issue ya kusajili talaka Rita, ni bora ukatafuta mwanasheria aliye karibu nawe akusaidie.
 
Ni kweli , mi na mwana anapitia hayo kipindi hichi story zinafanana kwenye swala la mtoto na tabia ya demu wake (japo wote wapo mkoa mmoja) anakamuliwa tu matumizi bora we unauhakika wa kipato...naye mwanzoni alikuwa na machale sahv ndo kapotea kabisa hashikiki..

Naona story yako umenikumbusha mwana, Inahuzunisha Sana !
 
Cha
Chai
 
Samahani mkuu naomba unisaidie unaangalia nn ili kujua mtt ni wako au umepigwa ikitokea hujafanana nae? Maana naona umelisema juu juu, utakua umenisaidia sana mkuu.
 
Kutumia cheti cha ndoa ambayo imeshavunjwa kujipatia manufaa hapo kuna elements za jinai.

Kwenye issue ya kusajili talaka Rita, ni bora ukatafuta mwanasheria aliye karibu nawe akusaidie.
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…