Kwani wewe ni punguani au huna kumbukumbu?
Hivi unajua hakuna nchi iliyoisaidia Ukraine mwanzoni?
Unafahamu kuwa mwanzoni kabisa Putin alituma kikosi ambacho ni top elites akijigamba kuwa atakuwa amekamilisha operation ya kuiondoa Serikali ya Zelewisk ndani ya siku 2?
Unajua kilichotokea ndani ya hizo siku 2? Ukraine bila ya msaada wa nchi yoyote, ilikiangamiza kikosi maalum cha Urusi, na kuwafanta wachache waliobakia kukimbia Kiev na kwenda Mashariki mwa Ukraine ambako kuna majimbo ambayo wakazi wake ni watuwa asili ya Urusi. Baada ya mafanikio ya Ukraine ya kuweza kuizuia Urusi kufanikisha kuiangusha Setikali ya Ukraine, ndipo taratibu Marekani ikatangaza kuisaidia Ukraine kwa vifaa. Na wataalam wa masuala ya vita akatamka wazi kuwa hawakutarajia Ukraine ingeweza kushindana na Urusi, wakasema wanaamini kuwa uwezo wa kijeshi wa Urusi waliokuwa wanaujua, ni dhahiri ulikuwa exagerated. Ndiyo maana hata utrkaji wa maeneo ya Ukraine, mpaka sasa, unaofanywa na Urusi, ni wa kujikongoja. Kiwastani Urusi inayateka maeneo ya Ukraine kwa wastani wa square kilometers 4 kwa siku.
Ilikuwa Battle of Hostomel.
Urusi ilichukua special forces yake ya anga VDV wakafanya helicopter assault wakatua kwenye airbase wakapigana vikali na Ukraine. Baadae wakateka airbase ila Ukraine ikafanya counter attack kubwa kwa vifaru na rocket launchers. Ukrainians waliofanya hivyo ni 72nd Mechanized Brigade wakapigana na special forces ya Urusi.
Hapo Urusi siku ya kwanza ilikuwa inataka iteke Hostomel na Antonov pale ili wafanye airlift ya silaha na wanajeshi waje wa-link na kutoa supply kwa main drive inayoenda kuteka Kiev.
Wakati huo Ukraine wanajipanga kwenye Battle of Kiev, mkuu wa majeshi ya Ukraine wa sasa kipindi cha uvamizi alikuwa mkuu wa majeshi ya ardhini. General Oleksandr Syrskyi aliongoza defensive lines na coordination kuzuia Russia kuteka mji mkuu wa Kiev.
Russia walikuja wakidhani watatumia siku tatu kwahiyo hawakuwa na provisions za kudumu muda mrefu. Battle of Kiev ilitumia kama wiki tu Warusi wakaona hawawezi hiyo approach wakarudi nyuma walikotokea Belarus.
Ndio pale sasa NATO ikaanza kutoa misaada, ndio zile Javelins zikaja tukaona misururu ya vifaru vya Urusi imepigwa barabarani wiki zilizofuatia.
Baada ya kufeli hiyo njia ndipo Urusi wakabidi warudi kule kule Donbass walikozoea tangu 2014. Wakapate afadhari maana kuna waasi waliokuwa wanawafadhiri, pia ni wanapakana nao.
Ndipo NATO ikaanza kuleta defensive weapons. Sasa Madulo yeye yani ungeanza kubandika maharagwe jikoni wakati shambulizi linaanza, kabla hayajaiva yeye ashatekwa.
Urusi walitamani siku tatu, wana mwaka wa nne wanaelekea kasoro siku kama 50. Marekani katumia masaa machache mtu umeingia guest kujifurahisha, ile unatoka ashatekwa mtu vita imeisha.