Trump anataka Marekani, China na Urusi zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi. Pia anapenda Urusi irudishwe kwenye G7

Trump anataka Marekani, China na Urusi zipunguze nusu ya bajeti zao za ulinzi. Pia anapenda Urusi irudishwe kwenye G7

Nenda kwanza kajifunze kuhusu sweatshops, hujui mengi.
Habari za kuokoteza kwenye mitandao na kuanzisha thread za ubishi inawaponza sana vijana wengi wa kitanzania. Wengi wanakuwa hawana deep understanding ya mambo ya dunia kwa sababu watanzania hatuna utamaduni wa kusoma na pia elimu yetu ni ya kukariri majibu lakini wanakimbilia kubishana vitu wasivyovijua.
 
Hawa jamaa USA huwa Wana kawaida hiyo,wakiwazidi wengine hukaa kimya,wakizidiwa hutaka ulinganifu.
Sijisemei kama porojo Nina mifano hai,
Mfano miaka ya 80 USA walipoona wamezidiwa na Urusi kwenye makombora ya masafa marefu wakataka uwepo mkataba wa kupunguza silaha Kali duniani.
Walipoona Urusi imeyumba kiuchumi na kusambaratika kwa USSR wakaanza kuunda Tena silaha Kali,Urusi alipowakumbusha wakamwambia kama anaweza na yeye anaweza kutengeneza,Sasa Urusi na china wamekua na nguvu Leo wanataka wapunguze bajeti za ulinzi.
Kwa kifupi Hawa jamaa ni wajanjawajanja.
Mna ufinyu wa fikra sana,
Putin ni mtawala wa Russia kwa miaka 25 sasa ambapo Marekani imeshabadilisha Marais Watano kuanziw Bill Clinton, Bush, Obama, Biden mpaka Trump, Marekani kuna vyama viwili vinavyopokezana madaraka kila mara. Masuala ya Marekani lazima yawe na mabadiliko mara nyingi tofauti na Russia au China ambao sera zinakuwa zimeganda kwa mtawala mmoja wa muda mrefu au chama kimoja.
 
Pia kiteknolojia na kiuchumi walipoona Japan imeizidi Marekani miaka ya 1980 wakaingia naye mkataba ulioitwa Plaza Accord na baada ya hapo Japan ikapoteana.

Unaposema Japan imepoteana unamaanisha ni wakati Japan ni taifa la uchumi namba tatu kwa ukubwa duniani ikiwa ni ukubwa wa eneo theluthi ya Tanzania tu?
 
Unaposema Japan imepoteana unamaanisha ni wakati Japan ni taifa la uchumi namba tatu kwa ukubwa duniani ikiwa ni ukubwa wa eneo theluthi ya Tanzania tu?
Kasome vizuri Plaza Accord na -ve effefts zake kwa Japan tangu wakati huo kufika sasa.

Unajua ambacho Marekani aliifanyia Japan?

20250216_112806.jpg
 
Kwa kifupi Trump ni rafiki wa Putin sana, na haoni sababu ya nchi zao kuingia vitani ndio mana anaomna poo kwenye bajeti zao.
Si unaona anasema Russia irudishwe G7? Kama nawaona nchi za West walivyonuna kama wamekula ndimu
 
Wameona kuna matumizi mabaya ya pesa ndiyo maana DOGE inataka efficiency kwenye matumizi ya pesa za Marekani. Kibunda kinatumika hovyo

Marekani ina deni la USD 36 billion, deni ni kubwa kuliko hata GDP ya nchi. Na kila baada ya siku 100 kwa wastani Marekani inaongeza deni la USD 1 trillion!

Kufikia hatua hii lazima nchi ilemewe na ndio maana wameanza kwa kupunguza unnecessary expenditures na kufanya review ya misaada yote wanayotoa.
Misaada ya Marekani ni 1% tu ya bajeti yao na chini ya 1% ya GDP yao. Hizo kelele za Musk na Trump kuhusu misaada ni siasa tu. Bajeti kubwa ya Marekani ni kwenye Medicaid na social security.
 
Tatizo unaamini kila propaganda za CCP na MAGA. China wanapika takwimu, makadirio ya wataalamu wengi wanaoifuatilia China ni kwamba bajeti yao halisi ya ulinzi ni mara mbili ya ile ambayo serikali huwa wanaisema. Pia fahamu kwamba ukiwa huna barabara za lami ukijenga utaonekana zaidi kuliko mwenye lami ambaye anahitaji kurekebisha mashimo tu.
HSR ya California imekamilka ?

Mimi sio CCP wala MAGA
 
Anasema anataka kumwambia Xi na Putin kuwa mabilioni wanayotumia kwenye bajeti za ulinzi na kuunda mabomu ya nyuklia yanaweza kutumika katika matumizi mengine mazuri

Kweli leo Marekani yenye bajeti kubwa ya kijeshi, ulinzi na muuzaji mkubwa wa silaha duniani imekuwa ya kusema hivi?

By the way ni kama Marekani imeanza kuyumba
Chekecha akili trump siyo zuzu kiasi hicho unachofikilia wewe.
 
Misaada ya Marekani ni 1% tu ya bajeti yao na chini ya 1% ya GDP yao. Hizo kelele za Musk na Trump kuhusu misaada ni siasa tu. Bajeti kubwa ya Marekani ni kwenye Medicaid na social security.
Hawezi kukuelewa
 
Na yale maswali mwishoni mwa uzi yamelenga ulichoandika. Marekani naona sasa kalemewa

Kwa kuongezea Marekani anataka kulegeza uhusiano kati ya China na Urusi na BRICS hasa anaposema angependa Urusi irudi kwenye G7

Marekani ameshaona haiwezi kushindana na Urusi na China. Anataka kufanya separation anafikiri akimrubuni Urusi kwenye G7 ataweza kudeal na China peke yake

Ila kwa sasa ukaribu uliopo kati ya China na Urusi na jinsi wanavyojua ujanja wa Marekani hawawezi kuingia huo mtego
Inabidi upambane kweli ili uendene na hilo jina lako la XI...hahahaa
 
Misaada ya Marekani ni 1% tu ya bajeti yao na chini ya 1% ya GDP yao. Hizo kelele za Musk na Trump kuhusu misaada ni siasa tu. Bajeti kubwa ya Marekani ni kwenye Medicaid na social security.
Hata kama ingekuwa asilimia 0 wanatoa ya nini kwani nyinyi hamna akili na mikono ya kuendeleza nchi zenu?
 
Hata kama ingekuwa asilimia 0 wanatoa ya nini kwani nyinyi hamna akili na mikono ya kuendeleza nchi zenu?
Ili ukipata Ebola, Marburg, Zika, Kaswende n.k usipande ndege kuwapelekea kwao.
 
Misaada ya Marekani ni 1% tu ya bajeti yao na chini ya 1% ya GDP yao. Hizo kelele za Musk na Trump kuhusu misaada ni siasa tu. Bajeti kubwa ya Marekani ni kwenye Medicaid na social security.
Mapato ya Marekani ni madogo kuliko matumizi yake. Ndio maana inalazimika kukopa ili ifikie malengo ya bajeti

Mara ya mwisho Marekani kuwa na surplus budget ni 2001, kuanzia 2002 mpaka sasa ni mwendo wa deficit budget na kukopa
 
Mapato ya Marekani ni madogo kuliko matumizi yake. Ndio maana inalazimika kukopa ili ifikie malengo ya bajeti

Mara ya mwisho Marekani kuwa na surplus budget ni 2001, kuanzia 2002 ni mwendo wa deficit budget na kukopa
Nani kakuambia kuwa na surplus budget ni jambo la maana sana kwenye kila uchumi?? Surplus budget inayotokana na utozaji kodi au kubana matumizi muhimu sio kitu cha maana sana kwenye uchumi.
 
Nani kakuambia kuwa na surplus budget ni jambo la maana sana kwenye kila uchumi??
Unaelewa maana ya kiuchumi kuwa na deficit budget? Taifa lazima likope kutoka vyanzo vingine

Hiyo inaongeza deni la taifa ndio maana kila mwaka deni la Marekani linakua kwa kasi sana

Kwa hiyo kuwa na deni kubwa la taifa ni jambo la maana kwenye uchumi sio?
 
Back
Top Bottom