Trump asitisha misaada yote ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine

Trump asitisha misaada yote ya kijeshi ya Marekani kwa Ukraine

Kwa kasi ya nyumbu isiyo n ufanisi ya Trump mwaka utaisha katepeta na kachuja.

Watu wake wanampiga biti Zelenski kuingia ikulu bila suti wakato mshikaji wake Musk kaingia kihuni tena na mtoto wake mdogo asiye na adabu. Na anaongea kwa dharau huku kasimama wakati raisi amekaa.
Unafiki ni sehemu ya mafanikio ya mabeberu.
 
Kwa wenzangu namimi ambao mmeshagundua iki kitu humu jukwaani mtakubaliana namimi,

% Kubwa ya watu wanaoponda maamuzi ya TRUMP juu ya maamuzi na sera zake kwa nchi yake uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana, yaani sawasawa na sifuri.

Fortunately Bwana TRUMP ni mtu ambae yuko very honest na mkweli asiependa unafiki, doesn't matter dunia nzima itapingana nae basi yeye ni mtu wa kusimamia misimamo yake kisawasawa.!!

MAGA ni sera aliokua nayo tangu kuanza kwa kampeni za Urais na wamarekani wenyewe kwa utashi wao waliamua kumkabidhi kijiti kwa mara nyingine wakiamini ni mtu sahihi kwa taifa lao cha kushangaza unakutana na mrusi wa Buza na mchina wa kakonko uko ndanindani anaanza kumpondea mtu ambae ameamua kuwa mzalendo kwa ajili ya Nchi yake.

TRUMP kaamua kuweka wazi kabisa kuwa mustakabali wake katika vita inayoendelea baina ya Ukraine na Kaka yake ambae yeye ndo alikua mfadhili mkuu ni AMANI vinginevyo iwe win-win situation. Hayupo tayari kuendelea kuliingiza taifa lake hasara zisizokua na kichwa wala miguu.

Pathetic.!!
 
Leo kwenye site ya BBC news Swahili,habari kubwa ni kusitishwa kwa misaada ya kijeshi from America to Ukraine!

Hatua hiyo ni kufuatia raisi wa Ukraine kuzozana na Mwamba trump wiki iliyopita.

Kwa maana hii Ukraine inatakiwa kutegemea zaidi msaada wa EU, hata hivyo EU haina nguvu ya kupambana na urusi.Hii itasababisha kushindwa kwa Ukraine.

Kinacho nishangaza ni kwanini Trump anaiunga mkono Urusi ?

Fikiria alivyompokea raisi wa Ukraine, Trump aliwaambia waandishi wa habari,"Mmemuona alivyo vaa? Kapendeza kweli kweli!".
Watu wengi wanadai hivyo ni vijembe.

Tusishangae siku Marekani akaweka vikwazo nchi yoyote itakayotoa msaada kwa Ukraine au hata Marekani yenyewe ikaanza kushirikiana na urusi kijeshi.

.
Screenshot_20250304-082125.png
 
Halafu deni liko pale pale bado marekani atamdai ukraine mabilion aliyotumia wakati wa vita. Na je ulaya itamsapoti mpaka aweze kumshinda mrusi? Ulaya ikiungana na ukraine dhidi ya urusi na china itaungana na urus ndo kitaumana wakati huo mmarekani amdkaa pembeni anaangalia hiyo movie,
3rd world war
 
Zile kelele za USA mifumo ndo inaendesha nchi, wenzetu wanalolifanya leo lilishapangwa miaka 20 iliyopiya na raisi ni mzimamizi tu tuziache sasa.

Tumeshajionea.
Hivi nyinyi mnao mshangaa Trump kwa kuitelekeza Ukraine nyinyi ni wageni ndani ya dunia hii?
Kwani vita ya Ukraine ndo vita ya kwanza kukimbiwa na Marekani baada ya kuona mambo yamekuwa magumu?

Marekani imesha ona kabisa kuwa hakuna uwezekano wowote wa kuishinda Urusi kwenye uwanja wa vita, hivyo anaona kuendelea kutoa pesa kwa vita ambavyo hakuna uwezekano wa kushinda ni upuuzi na ujinga.
Na haya mambo anayo fanya Trump si bahati mbaya bali ni mkakati ila Trump ni chambo tu.
 
Kwa kasi ya nyumbu isiyo n ufanisi ya Trump mwaka utaisha katepeta na kachuja.

Watu wake wanampiga biti Zelenski kuingia ikulu bila suti wakato mshikaji wake Musk kaingia kihuni tena na mtoto wake mdogo asiye na adabu. Na anaongea kwa dharau huku kasimama wakati raisi amekaa.
Unafiki ni sehemu ya mafanikio ya mabeberu.
Zelenskyy ni mkuu wa nchi na alikuwa ikulu kwa shughuli rasmi ya kimataifa.

Alipaswa kufuata code na etiquette husika.

Jifunze kutofautisha mada.
 
Zelenskyy ni mkuu wa nchi na alikuwa ikulu kwa shughuli rasmi ya kimataifa.

Alipaswa kufuata code na etiquette husika.

Jifunze kutofautisha mada.
Kwa nini leo wakati yeye amekuwa hivyo muda wote na sababu inajulikana.
Lingechukuliwa ni kama vazi la kitamaduni tu kama mkuu wa nchi ya Papua new Guinea angevaa sketi
 
Fikiria alivyompokea raisi wa Ukraine, Trump aliwaambia waandishi wa habari,"Mmemuona alivyo vaa? Kapendeza kweli kweli!".
Watu wengi wanadai hivyo ni vijembe.
Aliyeanza kumchokoza mwenzie ni Zelenskyy mwenyewe - kwa kufunga safari kutoka Ukreni na kwenda kumpigia kampeni Kamala Harris dhidi ya Trump.

Kwa maneno mengine alikuwa anautangazia umma kwamba Trump hafai hata jino moja.

Kwa mantiki hiyo, Trump naye anamjibu - inakuwaje mtu asiyefaa leo awe bora?

Zelenskyy ni kibaraka, na daima anaburuzwa na mabwana zake wanaompangia nini afanye, lipi aachane nalo.

Jamaa anashikiwa akili, hana maamuzi yake mwenyewe.
 
Kuna doube-standards kama lengo ni American First Policy, ambayo imeanza kwa kuzuia misaada kwa ajili ya nchi na mashrika mengi ya kigeni ; mbona haigusi Israel! Ambayo ni receipient namba moja wa misaada ya nje ya US?
 
Hivi nyinyi mnao mshangaa Trump kwa kuitelekeza Ukraine nyinyi ni wageni ndani ya dunia hii?
Kwani vita ya Ukraine ndo vita ya kwanza kukimbiwa na Marekani baada ya kuona mambo yamekuwa magumu?

Marekani imesha ona kabisa kuwa hakuna uwezekano wowote wa kuishinda Urusi kwenye uwanja wa vita, hivyo anaona kuendelea kutoa pesa kwa vita ambavyo hakuna uwezekano wa kushinda ni upuuzi na ujinga.
Na haya mambo anayo fanya Trump si bahati mbaya bali ni mkakati ila Trump ni chambo tu.
Vijana wa siku hizi wanachojua ni mpira na kubeti... historia hata ya nchi yao hawajui hivyo unawatazama tu na kusikitika
 
Kuna doube-standards kama lengo ni American First Policy, ambayo imeanza kwa kuzuia misaada kwa ajili ya nchi na mashrika mengi ya kigeni ; mbona haigusi Israel! Ambayo ni receipient namba moja wa misaada ya nje ya US?
Muulize Trump
 
Wivu, wizi na unafiki ndio umemjaa Trump. Hayo yote yanakuja baada ya Zelensky kukataa deal la Trump kutaka kufyeka rasimali za Ukraine kwa sharti la kumsaidia.
Unaijua gharama ya kifaru kimoja cha Abrams wewe?

Trump hafanyi hizo biashara kichaa za kugawa silaha kama njugu.

Mbaya zaidi sehemu kubwa ya misaada ya Ukreni ilikuwa ikiishia kwenye soko tusi (black market) na kisha kuingia mikononi mwa magaidi.

Zelenskyy na genge la NATO limefaidi sana mabilioni ya Marekani.

Trump anapodai wazitapike kwa gharama yoyote, kwa nini kumwona mjinga au mbabe?

Mabilioni hayo yangeleta maendeleo kiasi gani Marekani?

Mbaya zaidi, hakuna dalili yoyote ya vita kuisha hivi karibuni na wahuni wa Ukreni bado wanadai kupewa misaada mingine!

Nasemaje? Trump ashikilie hapo hapo hadi kieleweke.
 
Back
Top Bottom