hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,678
- 27,653
Fedheha aliyokutana nayo Ramaphosa ni nzito mno
Kama ya Zelenky ama zaidi. Yote haya ni kwasababu Afrika tumekubali kujiuza kwa ubinafsi wetu. Bilashaka haya yanatupata kwasababu baba zetu walipanda mbegu za ubinafsi. Waliishia kufia madarakani badala ya kujenga utaifa na uzalendo. Ona sasa Ramaphosa anavyodhalilika mbele ya Trump na dunia. Trump akiwapigania ndugu zake weupe na wengine amewapa hifadhi kutokea South Afrika. Ila sisi tunaua ama kuwafunga ndugu zetu weusi wanaokimbia taabu katika nchi zao. South Afrika imechoma ndugu weusi na Afrika ilikaa kimya, lakini ilivyogusa weupe, wazungu wamechachamaa, sasa Ramaphosa ameenda kuwalamba miguu ili wamfungulie vikwazo vya kibiashara. Anyway ngoja pia yamkute maana Ramaphosa naye alikuwa amejawa kibri akitoa maneno mazito mbele ya Marekani na akisema atatembea na Brics, sasa Brics wamepoteana kila mmoja amekuwa bize na kijiondoa na kamba za tariffs. Huku Putin naye akiwa bize kujinasua kwenye vita na kufungua uhusiano wa kibiashara na Marekani. Hivyo kila nchi inaangalia mambo yake ya kimaslahi. Kwahiyo basi Afrika tunahitaji mfumo wa kiuchumi kulingana na mazingira yetu na sio mifumo ya kukopa ambayo kwa kipindi kirefu imetufanya watumwa wa kiuchumi na kisiasa. Pasipo hivyo tutaendelea kujieleza mbele ya weupe kama Ramaphosa anavyojieleza mbele ya Trump kama mtoto wa shule kwa mwalimu wake.
Ila sijui kama tutatoboa kwa wingi wa ubinafsi huu tulionao. Mungu atusaidie.