Trump kamshtukiza Rais Ramaphosa ndani ya Oval Office

Trump kamshtukiza Rais Ramaphosa ndani ya Oval Office

Anyway ngoja pia yamkute maana Ramaphosa naye alikuwa amejawa kibri akitoa maneno mazito mbele ya Marekani na akisema atatembea na Brics, sasa Brics wamepoteana
Nani alikwambia BRICS wamepoteana? Na ni lini Rama alisema atatembea na BRICS?
 
yalikuwa yameingia doa baada ya Ramaphosa kukaribia zaidi China, Urusi (kupitia BRICS)
BRICS wala haihusiani hapo mkuu

S.A imekuwa mwanachama wa BRICS tangu S.A ikiwa na uhusiano mzuri na Marekani.

Sehemu kuu ya mazungumzo imehusu hasa wakulima walowezi Boers na hapa ndipo Marekani na S.A walipotibuana
​
 
Sio kwa China na Russia.

Hawezi kumuita raisi au kiongozi yeyote mkubwa wa China au Russia akamfanyia huo utoto wake

By the way yeye ndiye anajikomba kwenda China halafu wala hawana mpango wa kumkaribisha
​

View: https://x.com/business/status/1923572723290128385?t=3ZdxuoVY2p0Lq-Qj21i_8w&s=19


Trump au Marekani ni kwenda nao kibabe kama China na Russia zinavyofanya​

Ila ni tabia mbaya kuwakaribisha viongozi wa mataifa mengine ofisini mwako halafu unawadhalilisha.

Viongozi wenye akili hawatokubali kwenda huko Oval Office.
 
Kama anatetemeka vile! Kuongea na raisi wa dunia sio mchezo
Hiyo ni raisi wenu wa dunia kwa mataifa dhaifu

Trump alimwalika Xi kwenye kuapishwa kwake Xi akampotezea.

Wenzenu wameshajiwekea standards za kulinda utu na heshima zao
​


View: https://x.com/AJEnglish/status/1867381748658549006?t=xJKWxgy2oEfiM8KgY750dw&s=19

 
Ila ni tabia mbaya kuwakaribisha viongozi wa mataifa mengine ofisini mwako halafu unawadhalilisha.

Viongozi wenye akili hawatokubali kwenda huko Oval Office.
Trump has the maturity of an adolescent boy he really is a 72 year old child​
 
Viongozi wa Afrika hamkutakiwa kwenda Marekani kujipendekeza, nchi kama za Afrika zina kila aina ya utajiri, ila wanashindwa kufikiria ni watumiaje huo utajiri !
Wenye akili watumiaje wanapigwa vita wasio na akili ndo wako kwenye viti
 
Nimemwones huruma aisee.

Sioni kabisa haja ya marais kwenda kumwona mtu kama Trump hapo ofisini kwake.

Hata waziri mkuu wa Canada alipoenda naye aliishia kuwa mdogo tu.
Mbona Netanyahu lilikua lina ujasiri mbele ya trump na linaongea kwa kuliamini sana. Halina hata chembe ya hofu.
Au wanajuana?
 
Ramaphosa kilaza kweli, sitaki kuamini kwamba hakutegemea kuulizwa habari za Julius Malema.
Alionyesha utulivu sana bila kupaniki hata Trump alipojaribu kumbana... tofauti na Zelensky kipindi kile.

Ila alifanya vyema sana kuongozana kwenye hiyo ziara na waziri wake wa kilimo ambaye ni mzungu hii kidogo ilimsaidia.
 
Ila ni tabia mbaya kuwakaribisha viongozi wa mataifa mengine ofisini mwako halafu unawadhalilisha.

Viongozi wenye akili hawatokubali kwenda huko Oval Office.
Mbaya mno.

Ila jamaa anafanya kile wafuasi wake wa MAGA wanachopenda kukiona.
 
Kwa hiyo, ameenda kutuliza hali hiyo: kurejesha ushirikiano wa kibiashara, kuvutia wawekezaji, na kuzuia vikwazo vya moja kwa moja au visivyo rasmi.
Sawa Mkuu,
 
Hahahaaa.

Niliposikia anaenda kuonana na Trump ikulu ya Marekani, nikasema huyo anaenda kufanya nini huko?

Hakuona jinsi vile Zelenskyy alivyofanyiwa.

Haya, leo naye yamemkuta kiaina 🤣.
===============
Donald Trump amemshambulia ghafla Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, wakati wa mkutano katika Ikulu ya White House kwa kuonesha video ambazo alidai zinahusiana na tuhuma za mauaji ya halaiki nchini Afrika Kusini.

Rais huyo wa Marekani alikuwa akimkaribisha kiongozi huyo wa Afrika Kusini, ambaye alikaa kimya wakati video hizo zikipigwa. Baadaye, Bw. Ramaphosa alisema:
"Ningependa kujua mahali hapo ni wapi kwa sababu hizi video sijawahi kuziona."

View: https://x.com/JoeyMannarinoUS/status/1925235398243909955

Trump has no idea genocide ni nini? Hiyo ni minor issue but anaikuza
 
Africa tunatia huruma Sana, ila hakuna jinsi ni lazima Tuende kuomba misaada Kwa wenye Akili ili tuweze kuishi
 
Kama ilivyo desturi yetu hapa alivyo fanya muriro kukana wale walikuwa sio polisi wake kisutu.
Sasa rais rmaphosa kaleta maneno ya ukarimu sijui south afrika hakuna ubaguzi na wazungu wapo shwari.
Kaletewa tu video na picha ambazo zilikuwa mtandaoni mda.
Kabaki kimya.

Sasa zile kauli za viongozi mfano hapa tz tutawakumbusha mkiwa mnasemaga ukweli kwa kuandika vitabu ambavyo wengi hawa visomi.
 
Maoni yangu juu ya tukio hilo kati ya Rais Donald Trump na Rais Cyril Ramaphosa ni haya yafuatayo:

1. Siasa za Maonyesho na Msukumo wa Ndani wa Trump

Trump ana historia ya kutumia matukio yenye hisia kali ili kuvutia wafuasi wake wa mrengo wa kulia. Kwa kuonyesha video ya madai ya “mauaji ya wakulima weupe,” alionekana kulenga kuimarisha ajenda yake ya kisiasa ndani ya Marekani, hasa kwa wapiga kura wanaoamini kuwa kuna ubaguzi dhidi ya wazungu duniani.

2. Utulivu na Ukomavu wa Ramaphosa

Ramaphosa aliitikia kwa ustaarabu na ukomavu wa kisiasa. Badala ya kujibizana kwa jazba, alielekeza mjadala kwenye ukweli na juhudi za serikali yake kupambana na uhalifu bila kujali rangi. Hii iliimarisha taswira yake kimataifa kama kiongozi mwenye busara.

Rais Ramaphosa alijibu kwa utulivu, akisema kuwa video hiyo haionyeshi sera rasmi za serikali ya Afrika Kusini na kwamba vurugu zinazotokea nchini humo zinawaathiri raia wote, hasa watu weusi. Alisisitiza kuwa hakuna mauaji ya kimbari yanayofanyika dhidi ya wazungu na kwamba serikali yake inajitahidi kupambana na uhalifu kwa ujumla

3. Hatari ya Taarifa za Upotoshaji

Video iliyotumika na Trump ni mfano wa jinsi propaganda zinavyoweza kuathiri diplomasia. Kutumia video zenye kauli za wachochezi kama za Malema bila muktadha mpana kunaweza kuleta tafsiri potofu na kuharibu uhusiano wa kimataifa.

4. Uhusiano wa Biashara na Diplomasi

Licha ya mvutano huo, Ramaphosa bado aliwasilisha ombi la ushirikiano wa kibiashara — hatua ya kiakili inayotilia mkazo maendeleo ya Afrika Kusini badala ya kuanguka kwenye mtego wa ubishani wa kisiasa.

5. Ujumbe kwa Afrika

Kwa viongozi wengine Afrika, tukio hili linafundisha umuhimu wa kuwa na taarifa sahihi, busara katika mazungumzo ya kimataifa, na umuhimu wa kutetea nchi kwa hoja — si kwa hasira.

Kwa kifupi: Trump alitumia tukio hilo kwa maslahi ya ndani ya siasa za Marekani, huku Ramaphosa alisimama kama kiongozi anayetanguliza maslahi ya taifa lake na ukweli wa mambo.

Je Ramaphosa amejidharirisha?

Hapana, Ramaphosa hajajidharirisha — kinyume chake, ameonesha ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na diplomasia.

Hapa ndiyo sababu kuu:

1. Aliendelea kuwa mtulivu licha ya kushambuliwa kwa kejeli

Trump alitumia mbinu ya ghafla (ambush) kwa kuonyesha video yenye madai mazito mbele ya kamera. Badala ya Ramaphosa kuonyesha hasira au kukasirika, alijibu kwa utulivu na busara — akikanusha madai hayo kwa hoja na si jazba. Huu ni ukomavu wa hali ya juu.

2. Hakuruhusu tukio hilo kumvuta kwenye mjadala wa kihisia

Ramaphosa angeweza kulipiza kisiasa, lakini alichagua kuelekeza mazungumzo kwenye ajenda ya maendeleo na biashara. Hii ni hatua ya kiongozi anayejua kipaumbele cha taifa lake.

3. Alilinda heshima ya nchi yake mbele ya dunia

Katika jukwaa la kimataifa, kutodharirika si lazima kumaanishe kujibu mapigo kwa nguvu, bali ni kujua lini unapaswa kuwa mtulivu ili kuepusha taswira hasi ya nchi. Ramaphosa aliwaonyesha viongozi wa dunia kuwa Afrika haipaswi kutishwa au kuhamasishwa kwa propaganda.

Kwa hivyo:

Ramaphosa amecheza karata zake vyema — amejenga heshima kimataifa badala ya kujiangusha kwa kurushiana maneno. Na katika siasa za kimataifa, hilo ni jambo la msingi
Wabongo wanadhani ramaphosa amejidhalilisha hilo sio kweli ramaphosa amepata platform nzuri ya kufuta propaganda
 
Back
Top Bottom