Trump Waarabu wanamcheza kama wazungu wanavyowacheza viongozi wa Afrika

Miimi nimeuliza hizo ndege zilizompokea zilikuwa za Qatar au za jeshi la Marekani wenyewe? Maana US ana military base Qatar pale na trump aliwatembelea wanajeshi walioko hapo.
By the way kila kitu kinawezekana trump anafanya vitu vingi ambavyo watangulizi wake ilikuwa mwiko. Mimi nilichopenda ni pale anasifia nyumba ya Sheikh sijui ndiye waziri mkuu, nice house very nice house very beautifu... this is the meaning of perfection... jamani msije sema nimenukuu neno kwa neno lakini alisema hivyo.
 
Wandengereko waanze kuswali na viatu
 
Kiongozi kwa upande wangu sikuweka tu video kama pambo na kwenye post husika nikaandika alichofanya ni ‘news worthy’.

News worthy kwa sababu ndege ya raisi wa marekani ni out of the ordinary, kwa jinsi Air Force one inavyitakiwa kulindwa; ni breach of security kuruhusu ndege ya taifa lolote kupaa karibu yake.

Air force 1 inalindwa wewe kuifikia ni mission. Achana na hayo mambo.

Kwa sababu nahitaji msaada wako kwa mambo yetu mengine.

Lakini Air Force 1 alichofanya Trump ni serious compromise. What it does ina expose weakness ya US security.
 
Mpaka amalize kipindi chake tutashuhudia mengi.
 
Mpaka amalize kipindi chake tutashuhudia mengi.
Tatizo sio yeye ni weak security ya US na katiba yao.

Ni sawa na raisi wetu wa Tanzania kwa katiba yetu.

Upuuzi huo auwezakani popote kwenye developed nation nje ya US.

Sasa wazungu ni watu wakujifunza.

Kufanya kosa sio kosa, Iła kurudia kosa ni kosa.

Mambo anayofanya Trump, as far as developed nations goes; only possible in US.
 
Hakuna kipengele cha katiba kilichovunjwa na Trump.

Executive orders zote alizo signs, mamlaka hayo yapo kwenye katiba.

Hayo mengine ni madai tu ya wapinzani wake ambao hata afanye nini watadai kavunja katiba.
 
Hehehehe una maono ama mitazamo mifupi sana kaka.
Sio waarabu wote waoga laa hasha.
Kuna nchi za kiarabu zinajinyenyekesha kwa USA ili zilinde tawala zao mfano Saudi Arabia na Jordan,hizi nchi viongozi wao hawakubaliki na raia wao kwa asilimia kubwa,kama hawa viongozi wa hizi nchi hawatopata kujikomba kwa USA na kupata ulinzi basi wangepoteza uongozi muda sana.
Ila unapoitaja Qatar,Oman unataja mataifa makini sana na ya kijanja.
Unadhani kwani hayo mataifa hayajui kilichomkuta Saddam Hussein!??
Hao ni watu wa win win situation,huku watambembeleza Trump ila Wana agenda za siri,Hamas inalelewa na Qatar, Houthi inalelewa na Iran na Qatar, harakati zozote unazoziona za axis of resistance kifedha zinalelewa na Qatar na kijeshi zinalelewa na Iran.
Mwaka jana Qatar aliwakaribisha Iran kwenye maonesho ya silaha,tegemea siku zijazo Iran itakua ikiunda silaha pamoja na Qatar.
Pigia mahesabu hapo unapata picha gani.
Unadhani hao hawana akili kuwa silaha za USA sio za kuzitegemea!?
Ikatokea siku Westerners wakamgeuka Qatar kama walivyomgeuka Saddam tayari Qatar atakua na usaidizi wa kijeshi wa Iran.
Usitizamie mambo kiufupi aisee.
 
Hakuna kipengele cha katiba kilichovunjwa na Trump.

Executive orders zote alizo signs, mamlaka hayo yapo kwenye katiba.

Hayo mengine ni madai tu ya wapinzani wake ambao hata afanye nini watadai kavunja katiba.
Kwa viongozi wa kizungu ambao ni controversial learn to set limit on your support hata kama maamuzi yao hayakugusi wewe.

Ili mradi kuna wengine wanaumia na maamuzi yake unnecessary, hakuna maamuzi ya Trump yanayokupa wewe advantage. Ila yanawaumiza watu wanao tafuta advantage.

You don’t gain nothing for advocating Trump policies.
 
Saudia na USA ni kitu kimoja tambua saudia ana maadui wengi ambao wanaungwa na urusi
 
Wewe jamaa lugha ya malkia huielewi.
 
Kwa wale ambao mnashangaa ndege za kivita kuila escort Air Force One, hii hapa video kutoka wiki tatu zilizopita ambaoo ndege hizo hizo [hii ilikuwa ni Saudi Arabia] zikiisindika/ zikiikaribisha ndege ya waziri mkuu wa India, Narendra Modi, alipozuru nchi hiyo.

Waarabu wa Mashariki ya Kati huwa wana utamaduni huo.

Kwa hiyo wala si Trump pekee aliyepata hiyo treatment.


View: https://youtu.be/2g7sNvv7eTo?si=my1RTKYltRl4zl1g
 
Wanaswali sana tu, as long as Viatu ni visafi, misikiti kibao ya sunna nishaona watu wanaswali na Viatu.
Yoda anashangaa.

Uislam ulianza ukiwa mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyoanza.

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«بَدَأَ الْإِسْلَامُ غَرِيبًا، وَسَيَعُودُ كَمَا بَدَأَ غَرِيبًا، فَطُوبَى لِلْغُرَبَاءِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 145]

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Ulianza Uislamu ukiwa ni mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyo anza, basi shangwe kwa wale wanaoonekana kuwa ni wageni".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 145]


Allah atufishe katika Tawheed na Sunnah, Aamiin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…