Tufanye nini na hizi clip zinazopotosha Historia ya Tanzania?

Saigi...
Si rahisi kunipuuza.

Ingekuwa wepesi wewe ungefanya hilo.

Hujaweza kufanya hilo uko hapa unajadiliana na Mohamed Said.

Huijui historia ya Waislam na juhudi zao za kutafuta elimu.

Waislam chini ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) walikuwa wanajenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968.

Serikali ikapiga marufuku EAMWS na kumkamata Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na kufukuzwa Tanganyika.

Serikali ikaunda BAKWATA na kuipa mali zote za EAMWS.

Historia ya Waislam katika kujenga taasisi za elimu ni historia ndefu iliyojaa mengi ya kuhuzunisha.

Hapa hapatoshi mimi kukueleza yote ili nifute hiyo fikra uliyonayo kuwa sisi ni wavivu na walalamishi.

Tungekuwa wavivu tusingeweza kunyanyua silaha dhidi ya Wajerumani wala kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katika miaka ya 1970 Organisation of Islamic Conference (OIC) ilitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania.

Nyerere alikataa kutoa kibali chuo hicho kikajengwa Mbale, Uganda.

Usikimbilie kuwatukana Waislam ilhali wewe huna moja ulijualo katika historia yao.
 
Mudi, nilikupa tu mfano wa makosa makubwa mengi katika hiyo makala. But mi sijaona la kuhangaika nalo. Mi kuna mambo nasema hayana haja ya kuumiza kichwa na kulalamika lalamika kila wakati.
Mtu...
Nitashukuru kama utanitambulisha kwa jina langu sawasawa.
 
Huyu mohamef said mambo yake ni ya udini tu. Mwenyewe ni mdini. Wenyewe watanzania tunajielewa. Mtu alete uchonganishi wake wa kila aina hua tunamsare au ikibidi tunamzima kama koroboi.
 
Mohamed, huyu alikuwa ananijibu mimi. Lakini naona kama hamna tofauti maana kila mmoja wenu anavutia shuka upande wake.
Tukianza kuchambua mambo ya EAMWS (ambayo ilianzishwa na ilifadhiliwa kwa kiasi kikubwa na washia ambao masunni wengi wanaona kama makafir) hatutamaliza. Hadithi ya kushindwa kujenga chuo kikuu chenu Chang'ombe hali kadhalika.
Unazungumzia msaada wa ujenzi wa Chuo Kikuu ambao ulikuwa ufanywe na OIC lakini unapata kigugumizi kuzungumzia hatua ya mvatican kukabidhi Chuo cha Tanesco kwa waislamu.
Pamoja na yote haya nakubaliana na wewe kuwa maneno aliyotumia mwandishi kuhusu waislamu hayafai na hayana ukweli.

Amandla...
 
Huyu mohamef said mambo yake ni ya udini tu. Mwenyewe ni mdini. Wenyewe watanzania tunajielewa. Mtu alete uchonganishi wake wa kila aina hua tunamsare au ikibidi tunamzima kama koroboi.
Kmb...
Vitisho huwa hatari zaidi kwa anaetishia kuliko yule anaetishwa.

Zuia ulimi wako.

Singependa kukuonya zaidi kuhusu kunizima kama kibatari.

Umeropoka tu kwa ujinga au ghadhabu.

Ni kosa la jinai kutishia maisha ya mtu.

Mambo yangu si Uislam maana huna ujasiri wa kutamka unajificha nyuma ya neno "udini."

Nimeandika historia ya wazee wangu walivyounda African Association 1929 hadi kufikia kuunda TANU 1954.

Huu si udini.
 
Fundi,
Watu wawili tu ndiyo waliotafiti historia hiyo.

Katika watafiti hawa wawili wewe si mmoja wao: Dr. Mayanja Kiwanuka (1973) na Mohamed Said (1989).

Paper hizi zipo Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.

Hapa ndipo ilipo tofaiti yangu na wengi.
 
Nyerere alitaifisha vyuo na shula za Kikristo. Miaka imepita je nini kilitokea mpaka leo kinachozuia Waislam wasijenge shule na vyuo vyao kama Wakristo? Tuacheni kulia lia na historia ambayo iliathiri wote. Wengine waka move on. Wengine wakabaki wanalalamika mpaka leo. Nchi imekaa miaka 10 na Rais Mwislamu, Miaka 10 tena na Rais Mwislamu. Now miaka mitano itaenda na mingine 10. Tujengeni Vyuo na Shule. Misikiti tumejenga barabara yote kwenda mikoani. Hatukukatazwa. Ila shule hatutaki tunalalamika kila uchwao. Tumekuwa ni WALALAMISHI MIAKA NENDA RUDI. KAMA WAAFRIKA WANAVYOWALAUMU WAARABU NA WAZUNGU KWA BIASHARA YA UTUMWA NA UKOLONI..MIAKA ZAIDI YA 50 WAPO HURU BADO MASKINI.
 
Nimefupisha kama nawe unavyofupisha jina langu la Mtu Asiyejulikana.
Mtu Asiyejulikana,
Ungeniambia niandike jina lako kamili ningefanya hivyo.

Nakutaka radhi.

Ufupisho wa jina langu Mohamed ni Moh siyo Mudi.
 
Mohamed, seriously? Wewe na Kiwanuka ndio pekee yenu mliotafiti historia hizi? Na maandiko yote ya historia hizo yanapatikana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam peke yake? Mimi sio authority wa historia ya nchi yangu kama ambavyo wewe nawe sio authority wa historia hiyo. Ulichoandika ni historia ya jamaa zako na ambayo sehemu kubwa ni anecdotal ( nilisimuliwa na mjomba wangu, aliniambia fulani, nilimuona kwenye picha, nimepiga picha nae n.k.) na sio factual ( mtu mwingine anaweza kuthibitisha kwa kutumia vyanzo vingine) ndio maana pamoja na umbumbu wangu naweza kuonyesha mapungufu ya simulizi zako. Hapana, Mohamed. Wadanganye wengine sio mimi.

Amandla...
 
Ngawethu
 
Fundi...
Ikiwa yuko mtu mwingine aliyetafiti historia ya BAKWATA tuwekee jina lake hapa tumfahamu.

Kataroge Mayanja Kiwanuka , "The Politics of Islam in Bukoba District," Dissertation University of Dar es Salaam (1973).

Mohamed Said, "Islam and Politics in Tanzania," (1989), Al Haq International Karachi.

Mimi sina haja ya.kusema lolote kuhusu ujuzi wangu katika historia ya Tanzania.

Hayo mengine nabakia kimya wengine wakipenda watazungumza ila ninaloweza kukufahamisha na ni rahisi kwako kuelewa ni kuwa waandishi wa "Nyerere Biography," wameninukuu sana kuhusu Julius Nyerere katika kitabu chao.

Sijui kama umesoma kitabu hicho.

Hapa ndipo ilipo tofauti kubwa sana baina yangu na watu wengi wanaodhani kuwa wanaweza kushindana nami katika historia ya uhuru wa Tanganyika au historia ya Nyerere.

Mimi ndiyo mtafiti pekee ukimtoa John Iliffe katika miaka ya 1960 aliyebahatika kufunuliwa Nyaraka za Sykes.

Nimetumia nyaraka hizi katika miaka ya 1980 kuandika historia ya TANU.

Naamini unatambua kuwa Kleist Sykes yumo ndani ya Dictionary of African Biography (DAB).

Hii ndiyo tofauti baina yako na mimi.


Moja ya Nyaraka za Sykes katika Maktaba yangu​

''Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli toka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU.

Stakabadhi ya hundi ya posta toka kwa Ally Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru;

Nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa.

Barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa.

Barua ya mwaka 1963 toka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho.''

(Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...(2002) Phoenix Publishers, Nairobi.

 
Mohammed, tunarudia yale yale ya siku zote. Wewe kuwa na nyaraka za Sykes kunakufanya bingwa wa historia yake na sio ya Tanganyika hata ya uislamu. Hali kadhalika, historia ya Bakwata ni sehemu ndogo sana ya historia ya Uislamu wa Tanganyika. Article ya Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography uliiandika wewe na haimfanyi kuwa alikuwa na mchango zaidi ya watoto wake katika upatikanaji. Yeye na wakina Matola waliridhika kabisa na TAA kuwa chama cha jamii na sio cha siasa. Wanae ndio walichangia kukibadilisha muelekeo.
Dictionary ni dictionary na mara zote haiendi deep kwenye jambo lolote. Kutajwa Kleist Sykes mle ndani hakumaanishi kuwa yeye ndie alikuwa zaidi ya watu wengine.
Aidha, hizi barua na risiti hazina maana yeyote kama haziunganishwi na tukio muhimu katika historia yetu. Zaidi ya hapo ni kama mtu kuwa na photo album ya picha ulizopiga na mtu maarufu. Tunafurahi kuona sura za wazee wetu na miandiko yao lakini hamna kitu zaidi ya hapo.

Amandla...
 
Fundi...
Hakuna shida ndugu yangu.

Muhimu ni kuwa historia hii haikuwako kabisa.

Mimi ndiye niliyeirejesha na imepokelewa vyema kabisa kote vyuoni inakosomeshwa African History.

Hayakuishia hapo.

Nikapata kazi nyingi za kuandika historia na vitabu nilivyoandika vikachapwa na Oxford University Press, Nairobi na New York.

Vitabu vingine vimechapwa na wachapaji wa Tanzania na Kenya.

Ikiwa hayo kwako si lolote ndipo nimetanguliza kusema hakuna shida ndugu yangu.

Miaka 25 bado kitabu cha Abdul Sykes kinajadiliwa.

"Nyerere Biography" (2020) umekisikia popote kinajadiliwa?

Mimi ndiye ninaekitaja hapa peke yangu.
 
Mzee Mohamed Said, Wewe ni unaandika historia ya Uhuru wa Tanganyika au unaandika Historia ya Waislam katika harakati za Uhuru wa Tanganyika?
Mpasuaji...
Nimeandika kitabu kinaitwa: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…