TUHUMA: Ubadhirifu mkubwa wa ruzuku CHADEMA waripotiwa

TUHUMA: Ubadhirifu mkubwa wa ruzuku CHADEMA waripotiwa

Mimi mambo ya CHADEMA huwa yananichosha sana...Ile ni taasisi lakini mambo mengi hayaendeshwi kwa kuzingatia taratibu...sijui hata kama wafanyakazi wake wanalipwa mishahara na kodi za serikali ikiwemo ya PAYE kukatwa...na sielewi hata kama kuna wafanyakazi pale ambao michango yao inakwenda kwenye mifuko ya jamii...CHADEMA ni wazuri kuzungumzia maovu ya srikali na CCM, lakini kwao maovu ni mara mia...hakuna demokrasia ya ukweii...LOWASSA 'alichaguliwa' kuwa mgombea wa URAIS kupitia CHADEMA kwa wajumbe wa mkutano kunyoosha mikono huku kukiwa na hofu kubwa kwa yule ambaye hatanyoosha mkono...Li-CCM lina maovu mengi lakini wakati mwingine unasema ni afadhali hili zimwi ulijualo kuliko.... Uozo uliopo kupitia uteuzi wa wabunge kupitia viti maalum ndani ya CHADEMA ndiyo usiseme... i
Mwenyekiti wa ccm ambaye ni Mmiliki wa Richmond alienda Dodoma na majina Mfukoni akitaka Membe awe Rais lakini wafuasi wa Lowasa wakamkomesha kwa kumchagua Magufuli ambaye Juzi kakataa ccm wasitumie pesa za umma kufanya mkutano wao mkuu, kumbe huko nyuma walizoea kutumia pesa za Serikali kwa mkutano wa chama kisha kuitafuna Ruzuku kwa matumizi Hewa, ndani ya ccm pesa inapigwa Hatari na sasa mkuu wa Fitna, Uchakachuaji na Ndumba kaamua kuingia kwenye vibali vya sukari anapiga magendo kwa kwenda Mbele hakuna wa kuthubutu kumuuliza ccm ni shida, ccm bila January makamba leo hii kungekuwa ni Sawa na KANU ya kenya.
 
Hata Zitto,alipoomba CAG aje wakataka "awatonye".
Pesa za Ruzuku ya ccm zoote zinatumika kwenye mambo ya ajabu ajabu likiwemo kudhoofisha upinzani hata Lizabon licha ya kuishi Uvunguni mwa Lugumi mpaka sasa bado analipiwa kwa Ajili ya kuwachafua upinzani, boss wake January mzee wa fursa kwa sasa yupo busy na vibali vya sukari kasahau kazi yake ya fitna, Uchakachuaji na Ndumba kwa mda kidogo mpaka amalize kupiga Dili la sukari.
 
Eti ccm wameamua kuijiingizia pesa kwa njia haramu, sasa watatumia pesa ya Ruzuku kuagiza sukari kisha wauze wakipata faida watazitumia kuwanunua wapinzani,ccm kwa sasa ni wafanyabiashara wa sukari na kiongozi wa mchakato woote ni January makamba akimwakilisha Kinana.
 
Na Chotipembe Ntuguja.

Matumizi ya fedha za ruzuku ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaimeibua maswali mengi miongoni mwa watendaji wakuu wa chama hicho.

Chanzo chetu cha habari ndani ya CHADEMA kimedokeza kuwa kumekuwa na uhamisho mkubwa wa fedha mara tu ruzuku inapoingi kwenye akaunti. Zaidi ya shilingi milioni mia mbili zimekuwa zikihamishwa kila mwezi kwa madai kukijenga chama ila jambo la kustaajabisha ni kuwa pesa hizo huamishiwa kwenye akaunti mpya zilizofunguliwa katika benki moja ya biashara kisha kutolewa taslimu.

Kwa masikitiko makubwa mtoa taarifa huyu alisema ‘kaka ninachokuambia kwa sasa pamoja na ruzuku kuongezeka lakini nakuapia chama hakitafanya maendeleo muhimu kama ya kujenga ofisi wala kuimarisha ofisi za kanda na majimbo, kwa sasa hali ni mbaya tokea Dr. Slaa ameondoka mambo yamekuwa hovyo, taratibu za ofisi hazifuatwi na kumekuwa na matumizi holela ya fedha kwa mambo yasiyo na msingi’’.

Chanzo kingine kilitudokeza kuwa ‘pesa zinazohamishwa baada ya kutolewa benki taslimu ni malipo kwa mwanasiasa mkongwe aliyehama kutoka CCM na Kuja CHADEMA kwa mujibu wa makubaliano’’, ameendelea ndugu yangu mwenyekiti amekuwa ‘mbogo’ hataki kuulizwa kuhusu suala hili na ametamka yeyote atakayeendeleza mjadala atatimuliwa’’.

‘Mimi na vijana wenzangu tuliacha kazi, nilikuwa afisa wa serikali nikajitosa kugombea ubunge Mkoa wa mbeya nilitumia pesa zangu zote mbona silipwi? sababu kura nilizo pata zimesaidia kuongeza ruzuku japo nilikosa ubunge’

Aidha katika hatua nyingine kumekuwa na matumizi makubwa katika mikutano ya chadema huku ikiambatana na hafla kubwa kwenye mahoteli makubwa baada ya mikutano, ndugu yangu mkutano wa juzi pale Mwanza Gold Crest chama kililipa zaidi ya milioni mia mbili hamsini kwa ajili ya vyakula na vinywaji kwa siku mbili ukiachilia mbali posho za wajumbe’’ alidokeza mtoa habari wetu ndani ya chama. Wanatuhumiwa baadhi ya vigogo kuungana na watoa huduma kupandisha gharama ili kujinufaisha ‘ten percent’.

Malalamiko mengine yamejikita kwenye ubaguzi wa dhahiri kwa baadhi ya viongozi ambao hawakuunga mkono suala la mwenyekiti kuwapa ujumbe wa kamati kuu waliokuwa mawaziri wakuu wa awamu ya tatu na nne, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa.

‘Ndugu yangu sasa hivi mwenyekiti hana maamuzi na baadhi ya viongozi wameshaambiwa wasichukuwe fomu kugombea nyadhifa kwenye uchaguzi ndani ya chama unaotarajiwa kufanyika mwaka 2018.

‘Ninachokwambia baadhi ya viongozi wapo sababu ni wabunge lakini kulekea uchaguzi mkuu 2020 mtasikia mengi, kuna fukuto kubwa sana na mwenyekiti kwa sasa amefanya shingo ngumu’’

Baada ya mazunguzo haya mwandishi alimtafuta Mwenyekiti wa Taifa ambaye alipokea simu baada ya kuombwa miadi alijibu ‘I am busy’ yaani kabanwa na shughuli, mara ya pili alivyoulizwa tuhuma hizi alimwambia mwandishi aende kwa katibu mkuu ambaye alisema ‘no comment’’ baadaye akajibu anashughuli nyingi ikiwamo safari ya nje ya nchi hivyo hakusema zaidi.

Maswali yangu kutokana na habari hii.

Je ni nani wanalipwa mamilioni haya?

Ni makubaliano gani ya siri baina ya uongozi na watu bila ya maamuzi ya vikao?

Je waliokosa ubunge nao wanalipwa fidia hii?
Lizabon bado upo Uvunguni nyumbani kwa Lugumi? Kitwanga anataka pesa zake maana anasema imetafuna pesa bila kufanya kazi ya maana kumtetea vya kutosha.
 
Mapato na matumizi ya ccm hayapo kwa CAG wala hatafahamiki ndiyo maana Magufuli kawagomea kuwapa pesa za Serikali kwa Ajili ya kuendeshea mkutano mkuu wa ccm, pesa yote ya Ruzuku, miladi Michango ya wanachama na pesa Toka chama cha china yoote imeliwa na wajanja na pengine Wewe ni mmojawapo maana inaelekea unaogopa kitu.
Mkuu funza mbona sikuelewi? Mimi nimekuwa gamba tena wa kula hela za CCM? Ntake radhi aisee huwezi nitusi namna hii
 
Lizabon toka Uvunguni kwa Lugumi mzee kitwanga haji tena leo kukudai.mtafute January wakupe pesa za Ruzuku ya ccm uagizie Sukari.
 
Mkuu funza mbona sikuelewi? Mimi nimekuwa gamba tena wa kula hela za CCM? Ntake radhi aisee huwezi nitusi namna hii
mkuu hujanielewa mie sijakutisi kama nimeteleza nisamehe lakini pengine nimechanganya bahasha pole mkuu, usikonde komaa tuwape vidonge hao ccm sukari mpaka waache kuiba Ruzuku na kumjengea nyumba ole sendeka.
 
Msiyaseme ya chama chetu pendwa!! Huwa hakifanyi makosa. Kimejaa malaika wengi, Lowassa, Mbowe, sumaye.

Hawana tuhuma wala kashfa yoyote.
Mmiliki wa Richmond ni Kikwete na boss wa infosys Kitwanga ni mshirika wa Lugumi, Mwakyembe ni mkuu wa mabehewa chakavu, January ni mkuu wa Madili, fitna, Uchakachuaji,Ndumba nk, Dau wa NSSF ni mkuu wa Siri ya ufisadi wa NSSF juu ya daraja nk , Membe ni mfujaji wa pesa za NIDA na mabilioni ya marehemu Gadafi, hao ni baadhi ya ccm ambao hawapendi Dili kubwa, wao wamepiga vidili hivyo tu hawataki kusikia mtu anapewa vibali vya sukari bila kuacha 10% kwa January ambaye huwagawia ganji zao baadae.
 
Unajua ruzuku ya chama ni kiasi gani kwa mwezi?kama inatoka mil 200,hiyo ni significant loss kiasi kwamba kwa pesa inayobaki chama hakiwezi kuwalipa watumishi wake!Hizi ni shobo tu na propaganda!CAG angekuwa ameshaliona hili!
Hata kama ni kiasi kidogo wameshindwa kujenga hata jengo lenye gorofa moja wakubwa? wanakuwa kama wawekezaji wa kupita ambao hawana shida na kuwekeza katika majengo ni aibu kwa kweli
 
Lumumba timu mko vizuri haswa duh
Poleni kama mnataka kuzima nguvu ya CHADEMA kwa mfumo huo mmefeli sana tumeziba masikio
Mkubwa swala si uzushi unataka kuniambia kuwa ruzuku wanayopewa haitoshi hata kujenga office yao ndogo au utasema sio malengo yao kuwa na ofice
 
Kwasasa tunajenga chama kwanza, Vipi kuna lingine?
Kujenga chama kunaendana na kuwekeza mkuu kuwekeza sio tu katika watu pia katika vitu kama officer ( kwa maana ya majengo ya chama) ili uweze kueleweka kwa watu makini. ukiondoa siasa za kijanja za kuchumia tumbo unajua kabisa kuwekeza ni muhimu
Mfano timu zetu kubwa zinashindwa kuendelea kwa sababu hata viwanja hawana majengo yenye mazingira mazuri hawana kuhaminikia kunakuwa kudogo, miaka 20 bado ni wachanga mnapanga sio sawa sana mkubwa
 
Umeleta ripoti ukiwa kama nani? na kutoka kwa nani ?na ili iwe nini?na utanaka tuchangie nini?bahati mbaya hatuna akili za Lumumba,nenda mkahadithiane nyumbani kwenu huko
Jikite kwenye hoja,acha hasira.
 
Eti ccm wameamua kuijiingizia pesa kwa njia haramu, sasa watatumia pesa ya Ruzuku kuagiza sukari kisha wauze wakipata faida watazitumia kuwanunua wapinzani,ccm kwa sasa ni wafanyabiashara wa sukari na kiongozi wa mchakato woote ni January makamba akimwakilisha Kinana.
Dogo mbona umeumia sana au wewe ni Komu?
 
Watafuna Ruzuku ya ccm ndiyo wameandaa Huu uzushi ili watu wasahau kuwakumbusha jinsi pesa za miladi ya ccm Viwanja wa soka parking na Michango ya wanachama zinavyoliwa kifisadi.
Yoyote yule anaye fisadi jasho la watanzania achukuliwe hatua, kwenye Mali za Umma tuwe wamoja kulipinga. Fisadi hana dini, kabila, wala chama.
 
Back
Top Bottom