Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Mayalla acha upotoshaji. Wasukuma ni "wabaguzi" kama makabila mengine.Ushahidi upo.
1.Ubaguzi wenyewe kwa wenyewe.
Kati ya Wanyantuzu na wasukuma wengine. Wanyantuzu huwaona wengine "wajinga" kwa kuwaita "babuli bha ng'hweli" -wajinga wa magharibi(Bariadi ipo mashariki) na wasukuma wengine wapo magharibi.
2.Ni ngumu mtu wa kabila tofauti na Ntuzu kuendesha biashara na kufanikiwa Bariadi (miaka kadhaa nyuma). Hujuma na vikwazo ilikuwa kawaida.
3.Kuna msemo wa "likabila" ambao huitwa wasio wasukuma. Hadi miaka ya karibuni ilikuwa vigumu kujichanganya nao bila kuhisi "ugeni"
NB.Magufuli si msukuma bali kazaliwa na kulelewa usukumani. Ni mhamiaji haramu japo anaongea kisukuma.Ni mhutu! Ndo maana matendo na tabia ni za ki-Nkurunzinza!
 
Niongezee nikuwa naangalia data

  1. Brela: Biashara nyingi zilizopo wasukuama hawako hata karibu ya kuongoza kaangalie registration pale.
  2. CPA. Yaani certified Public Accounting wa Tanzania hadi wapare ni wengi kuliko wasukuma!
  3. Advocates: Hawa ni certified attorneys yaani hata watu wa Mara, wahaya ni wengi kuliko wasukuma
  4. Professors: Walimu wa vyuo wahaya na wachagga, na wanyaksusa wanaongoza
  5. wafanyabiashara wadodo wadogo au Machinga hadi watu wa pemba, watu wa kusini ni wengi kuliko wasukuma
  6. Viwanda: wahindi na wahamiaji wanaongoza
  7. Media: Vyombo miliki vya wahaya na wachagga ni vingi kuliko wasukuma
Kwenye siasa wasukuma ni wengi kidogo zaidi maana wana wabunge zaidi lakini huwezi kusema ni dominant!. Wasukuma au wahaya ni dominant kwenye lipi wame dominate wapi kwenye idara au sehemu gani ya uchumi. Hata kwenye kilimo ambako ndiyo wengi wapo nimeangalia kilimo cha Moshi, Tanga, Manyara kinazidi usukumani na mikoa yote, Mikoa ya Mbeya kule wanalima kuliko usukumani. Hivyo sio kweli kwamba tuna dominant kabila Tanzania hakuna. Kenya mfano kwenye siasa, biashara, utajiri kote huko ni wakikuyu kasoro elimu ni Luo
 
Mmasai akigombea ubunge Newala atapata?.
 
Hivi wewe jamaa unaona fahari gani kuzungumzia ukabila ??? Yaani kabisa unajitutumua unaleta hoja za makabila Tanzania ya leo hii.

Mijadala kama hii huwa haishi vizuri, na wewe kama mtu mwenye ufahamu nilitegemea ungekuwa ushalifahamu hili mapema.

Yaani umefungua kabisa na uzi wa kikabila kisa tu kujenga hoja za kisiasa. Sijui wasomi wetu mna matatizo gani.
 
Mkuu sifikiri kama sababu ulizoweka hapa kuhusu kutoanzishwa vijiji vya ujamaa Kilimanjaro au Bukoba ni sahihi; labda kama unajibu ili ukubaliane na unayemjibu. Kuna mtu walifungua uzi kwenye hii kitu.

Hivi kweli kila mtu akitumia sahani yake wakati wa kula ni kuwa selfish?? Mbona ndo mijini majumbani wanafanya hivo? Kuhusu viamba mbona mjini kila mtu ana kiwanja chake na kuna maeneo ya wazi kwa watu wote? Ndo ilivyo huko vijijini kwenye jamii hizo kila mtu ana kihamba chake lakini yapo maeneo ya wazi (communal land) kwa watu wote mfano kuchungia ngombe. Kama yanayofanywa mjini unayaona sio kuwa selfish basi hizi jamii kwa muktadha wa hoja yako hapo juu sio selfish.
 

Pascal Mayalla,
Kwani Magufuli ni Msukuma asili au wa kuja? Kama ni Msukuma-asili niambie asili yake wapi? Halafu nitakwambia aina ya watu wanaojiita wasukuma hata kama si wa asili.

Wasukuma-asili wengi ukikutana nao faragha na kuwauliza kama Magufuli ni Msukuma utasikia majibu mbalimbali. Kuna kitu kimoja wote wanakubaliana: HAKUNA Msukuma wa aina ya ukali, ukatili, kiburi, na ujuaji kama Magufuli.

Ni kweli Wasukuma si wabaguzi kwa asili. Na wala Si wakatili na wenye kiburi. Wengi ni wapole, wanyenyekevu, wakarimu na wenye upendo kwa watu hata wasiowajua au kukubaliana nao. Wasukuma-asili hawanaga visasi.

Hata hivyo kutokana na ukubwa wa kabila hili, kuna vikabila vidogo vya kanda ya ziwa na baadhi toka nchi jirani vilivyomezwa na kujiita "wasukuma" ili kupata unafuu wa kujichanganya na kabila kubwa. Hawa asili yao yaweza kuwa mwingine japo wanaongea Kisukuma safi na hata kufuata mila na desturi zote za wasukuma-asili.

Siwezi kusema kwa hakika aina ya Msukuma aliyo nayo Magufuli, japo kwa anayewajua vizuri Wasukuma halisi, ni vigumu kumshawishi kama Magufuli ni Msukuma-asili.

Labda niseme hivi: Magufuli ama kawainua au kawahatibia kabisa Wasukuma-asili. Wengi wanaowajua vizuri kama wanyenyekevu wapole, na wakarimu, watakuwa wamebadilishwa kabisa kimtazamo na Magufuli huyu. Lakini pia wale waliodhani
 
Ndugu Jorojik, Thank you very much kwa ukweli ulituwekea hapa. Ndugu Pascal anaendelea kujivunjia hadhi na heshima, japokuwa ni mwandishi mzuri na mwenye maono mazuri ya kisiasa, lakini naona amejiunga na kundi linalosemekana lina mipango ya kutuletea siasa za kiKENYA nchini kwetu.

Ndugu Pascal yumo kwenye siasa za kidini na kikabila, hili jambo limenishtusha na kunisonesha sana, i was a great follower of his writings, but now am very disappointed.

Ninamuombea mungu amrudishe kwenye fikra za kizalendo na amuepushe na ukabila na udini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu Pascal, I truly hope unasome post zote katika uzi huu.

JEE huoni kama umetukosea sana Watanzania kwa kuutukuza ukabila na udini?

JEE huoni kama kuna wengi hapa JF walikuwa wapenzi wa michango yako mizuri na post zako nyingi zilizokuwa na mafunzo, ukweli na upendo.

I believe you need to sit down na kutafakari na ujirekebishe.

Ndugu Ukabila hauna maendeleo wala faida, nadhani hakuna anayefaidika kwa ukabila , it has never put any food in your plate nor supported your family.

Ndugu tuangalie yaliyotokea Somalia, hii ni nchi yenye watu wa Lugha Moja, dini moja tena madhehebu moja, lakini kilichoiteketeza somalia ni ukabila.

Tusisahau yaliyotokea Rwanda, Burindi, Kenya, Central Africa Republic, Myanmar na yanayo endelea leo India, bila kusahau Iraq na Syria.

Jee utafurahia hayo yakitokea Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli Pascal huwa ananisikitisha kwa posts zake za kikabila na ukanda. Sijui anajaribu kuleta ujumbe gani kwa Taifa?! Wacha tuangalie.
 
Mkuu Facts First usemayo ni facts na hao Wasukuma unaowazungumzia wewe ndio Msukuma mimi, ila karibu pande hizi
P
 


Kusambaa kwa Wachaga ni kufanya biashara na si wengi kubali. Wasukuma wameenea kila mahala hadi Zambia. Wasukuma ni matajiri wa rasilimali mfano, ngòmbe, ardhi kwa maana ya kilimo, madini, uvuvi na chakula. Nenda Zanzibar ni wakulima wazuri wa mpunga. Wachaga mtu mmoja akiwa na uwezo familia nzima inaishia kwake. Wakati wasukuma kila mtoto katika familia uwezeshwa kuwa na mifugo na mashamba yake. Wasukuma si watu wa kujionesha na kujitangaza, pia majina yao ni mengi hayajirudii kama ya wachaga mfano Lyimo, Urassa, Chuwa na kadhalika. Hivyo majina haya kuwa common ni rahisi kujua hapa kuna mchaga ndo maana unahisi wachaga wengi. Wachaga wanakisiwa kuwa 1.2 Million wakati wasukuma ni kati ya Million 8 hadi 10. Familia za kisukuma si masikini kama unavyodhani bali wanapenda kuishi maisha ya kimila zaidi si modern life. Wakiamua kuuza mifugo yao nadhani utatambua ni kiasi gani wanauchumi mzuri. Wengi ni wafanya biashara za madini mikoa inayokaliwa na wasukuma wana madini mengi mbali na uvuvi. Ardhi kubwa. Ni tofauti na uchagani kuna shida ya ardhi familia moja wanakusanyika katika plot moja, hii ni tofauti na usukumani kila mtoto anapewa ardhi na mifugo yake.
 
kwenye hotuba moja ya Julius alisema nchi hii ukizingatia vigezo vya sifa juna hatari nafasi zote za serikali kushikwa na wachaga na wahaya, halafu uone moto wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kwa vipi Pasco kijiji kijengewe Airport??
Sio airdrome nasema airport ili zitue ndege gani, kwa bdgt ipi ikaidhinishwa lini na bunge lipi??
Mwl Nyerere hakufanya hivyo, nyumba tuu yakuishi alijengewa na jeshi tena wa lazima!!
That was a true Tanzanian, man of people.
Yako mengi watu wanaogopa watu waiojulikana!!
Mzee wa kiti moto back to your real sence!!
 
Kusema ukweli Mimi ni mkabila 100%,Ni mzalendo 100%.
Kukiwa na nafasi 10 za ndani ya nchi nitaanza na kabila langu,nitafuata wale wa ukanda wangu,ila nitakikisha wote wana sifa.
Kukiwa na nafasi 10 za kimataifa nitaanza na Watanzania Kisha watafuata wa nchi jirani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikia mahali Mchungaji Gwajima amehojiwa kwa kuhamasisha ukabila. Sheria yetu ya uchaguzi inakataza kabisa watu kuhutubia kwa kilugha katika mikutano ya kampeni za uchaguzi, hicho nilichoeleza hapo ni kitu ambacho nimekishuhudia kikifanyika, maofisa wa NEC wakiwepo, OCD na polisi wake wakiwepo, and nothing was done about this na kuna watu wanadhani baadhi ya watu kuhutubia kwa lugha za Kisukuma wameanza leo. Hili ni bandiko la mwezi May, 2009, miaka 11 iliyopita!. Sasa leo Gwajima anapoyasisitiza haya kosa lake ni lipi?.

Naendelea kusisitiza Wasukuma sii miongoni mwa makabila yenye ukabila m-baya

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…