Wengine wamekusifu kwamba you're article is very philosophical. Mimi naku - challenge kwa sababu hueleweki wewe ni wa MOTO au BARIDI. Mimi nilichoona kwenye article yako ni falsafa laghai, ya ujanja janja wa kucheza na maandishi na potofu kabisa kwa 90%..
Mtu makini akisoma kwa utulivu andiko lako, atatambua moja kwa moja kuwa wewe ni walewale watu wa kumsifu Mfalme/malkia hata kama anatembea uchi barabarani badala ya ku - shout na kumwambia; "...
Helloooo mfalme/malkia uko uchi.." badala yake mtapaza sauti zenu na kusema "...
Helloooo mfalme/malkia umependeza kweli..". Huu ni UNAFIKI..!
Nita highlight kila hoja yenye upogo na kukueleza kwanini Iko hivyo. Na ukiweza unaweza kujibu, la huwezi chukua kisha kaa kimya hukohuko uliko utafakari..
Twende kazi👇
Hakuna mkate mgumu kwa chai.
Mwabukusi akiangalia macho ya Rais Samia kwa utulivu, hakika atapata utulivu wa nafsi.
Kwa hiyo mnajiandaa kumnunua/kumhonga (kuuyeyusha mkate kwa chai ya moto?) Halafu Ili iweje? Tuendelee kuishi ktk impunity?
Hebu fafanua una maana gani hapa..
Mwabukusi itampasa atoke kwenye mode ya kuwa mwanaharakati( fight & flight mode) ili mapigo yake ya moyo yaendane sawa na mapigo ya moyo ya Rais Samia na serikali yake.
Hii dhana ya "uanaharakati" (activism) toka kwako tena na watu kama
Pascal Mayalla mnaelewa hata maana na utendajikazi wake kweli ktk jamii huru inayozingatia utawala bora na wa haki?
I don't see anything tangible in you. Nakuona ni kama mtu mwenye ufahamu na uelewa fulani lakini ukiu - misuse big time matumizi yake kwa hila au kwa nia ovu..!
2024 na 2025 tunakwenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Sisi watanzania kwa ujumla tunapaswa kuhakikisha mapigo yetu ya moyo yanakwenda sawa na mapigo ya moyo ya Rais Samia na serikali yake( coherence).
Wewe na sio Watanzania wote, please..!!
Unataka mapigo yetu ya moyo yaende sawa na huyu mama ambaye ni a big failure president? Really?
No. Tumsaidie by telling her the naked truth, kwa kumkosoa na kumkemea Ili akikubali, then awe the good president Ili tuanze kumpongeza...
Kwa kauli na matendo yake yeye kama Rais na chama chake - CCM it's open that, wamejiandaa kuharibu na kuvuruga chaguzi zote kama walivyofanya miaka yote. Yet unataka mapigo ya mioyo yetu yawe cohesive na yake..?
You're absolutely insane ndugu Mr/Ms Adverse Effect..!!
Ni wazi pasi na shaka kuwa moyo wa Rais Samia umejaa upendo kwetu sote na kwa watanzania kwa ujumla ila lazima tutambue Rais Samia yeye peke yake bila ya sisi sote kumsapoti kwa pamoja hatofika mbali au atafika akiwa amechoka. TUMSAIDIE!
Hapa at least umekiri jambo muhimu sana. Yes, she's a human being. She's not perfect. Anahitaji kusaidiwa.
Shida Moja mliyonayo nyie watu wake akiwemo huyu mzee
Pascal Mayalla hamjui ni msaada gani muhimu anaostahili kupewa huyu mama..!!!
Mnadhani kuwa kwa kumsifu kwa sifa za kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa ndiko kumsaidia?
Tunawaambia wazi kuwa, huku si kumsaidia bali kumpoteza na kumdidimiza chini kabisa..
Kumsaidia Rais ni kufanya hivi:
1. Kumwambia ukweli anapokosea yeye binafsi au wasaidizi wake na serikali yote kwa jumla anayoingoza.
Mfano tumwambie ukweli kuwa, kwa kulea sheria mbovu, kulea wasaidizi wake wezi na mafisadi na wasiozingatia na kuheshimu utawala bora unaozingatia sheria na Katiba, yeye Rais kukataa kurekebisha mifumo ya utawala kwa kufanya major constitutional amendments, yeye Rais kukataa kuendeleza mchakato wa kuandika katiba mpya shirikishi ili imsaidie ku - facilitate michakato ya kimaendeleo ktk nchi nk, basi afahamu kuwa hiyo ni shida na ni changamoto kwa nchi na taifa zima..
Huu ndiyo mwelekeo wa Adv. Boniface Mwabukusi na TLS ya Sasa anayoiongoza. Sasa hebu sema Kuna ubaya gani kwake kuchukua uelekeo huo huu?
Siasa za harakati na siasa za kupambana kwa hulka na tabia ya Rais wetu Samia hazitakuwa na mashiko Wala tija katika chaguzi zijazo.
Nani anapambana na nani hapa?
Mfano ni upi hasa wa mapambano unaoweza kuutoa hapa Mr/Ms
Adverse Effect Ili pengine utaeleweka na kuungwa mkono?
Au unaandika tu kwa kutumia mapenzi ya hisia, yasiyo na uhalisia..?
Hivi watu wanaposema kwa mfano;
"...
hapana, hapa Rais na serikali yako mmekosea badala yake ingekuwa vyema mngefanya hivi au vile..";
au
"...hapana, hapa Rais, serikali na Bunge kwenye mkataba huu mmekosea, ni mbaya na madhara yake kwa nchi ni 1, 2, 3..."
Je, ndo kusema kwamba mtazamo na ufahamu wako huu, kumbe huku ndiko kufanya siasa za harakati na kupambana? Really? Mimi naamini, kama ni hivi basi haya ni mapambano mazuri sana yenye lengo zuri kabisa la kukomesha uhalifu wa kisheria na utawala bora!
Kama wewe na mwenzako
Pascal Mayalla na wengine wenye fikra za dizaini yenu ndivyo mnavyoelewa, basi ninyi ni BURE KABISA, mmepotea na hamna msaada wowote kwa nchi na taifa hili huku nyie kwa "ujinga" wenu mikijidhania kuwa mnalisaidia taifa na viongozi wake ukweli ukiwa ni kinyume chake.!!
Miaka 60 ya uhuru kama nchi tumepambana na umasikini tumeshindwa, tumepambana na ujinga tumeshindwa halikadhalika kwenye maradhi, rushwa, ufisadi n.k.
Eleza ni kwanini unadhani tumeshindwa? Je, ni kwa sababu ya wanaharakati? Wepi hao na kwa namna gani wamefanya tushindwe..?
Sote kwa pamoja tunapaswa kubonyeza button ya switch off fight and flight mode na kuwasha button ya utulivu na uamsho mode ili kuweza ku match na kuongea lugha moja
badala ya lugha gongana.
Ndugu
Adverse Effect, button ya utulivu, uamsho mode ni hii: HAKI, HAKI, HAKI na HAKI ikitawala tunakuwa na AMANI na AMANI ikitawala watu watakuwa na furaha na upendo, hakuna ugomvi na kulaumiana tena.
Wapuuze watu kama kina
kavulata ambao wanadai na kuamini kuwa duniani hakuna haki. Ni waongo na hawajui wasemalo na wanachokiamini. Mungu anasema:
"..
.Haki huinua taifa na watu waovu watawalapo, watu huugua/huumia..."
Na Mungu anaposema akatokea binadamu akapinga, huyo ni mjinga na baba yake huyo ni Ibilisi. Hapo Mungu amesema. Na kwa hiyo HAKI duniani inaweza kuwepo kama hatutaruhusu waovu watutawale..!
Kwa kuwa tumejifunza kwamba hakuna faida kubwa kwenye kupambana basi hatuna budi kubadilisha gea angani.
Badilisha gia huko huko angani kwa kuanza kuusema ukweli.
Waambieni watawala ukweli kwa lugha yoyote wanayoweza kuielewa. Mwabukusi anaweza kazi hii..
Ushauri wangu kwa Rais wa TLS Mwabukusi, wanazuoni wote kwa ujumla na wananchi tuacheni KUPAMBANA sababu kupambana hakujawahi kutusaidia na kutufikisha tunapotarajia au tunapotaka.
Kwa mwelekeo na mission ya Adv. Boniface Mwabukusi na TLS anayoingoza sasa, dhana ya "kupambana" (makabiliano ya ugomvi usiojenga) ni ni tafsiri yako wewe ndugu
Adverse Effect na kwa 109% hiyo yako ni tafsiri potofu...!
Nimekuambia huko👆juu na nakuambia tena hapa kuwa, kukemea viongozi wezi na mafisadi, viongozi wavunja sheria, viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya (abuse of powers) kuonea na kunyanyasa watu wengine, viongozi wavunja taratibu na katiba, viongozi wanaonajisi utawala bora wa kuzingatia kanuni, sheria na Katiba nk haya si mapambano hasi kama unavyotafsiri wewe Bali haya ni mapambano chanya mazuri yenye nia ya kujenga utawala bora na kuleta ukombozi kwa watu wote..
Tukome kupambana na umasikini tuongelee na kujadili UTAJIRI tuliyokuwa nao.
Eleza utakomaje kupambana na umasikini...........
Na eleza utajadilije UTAJIRI bila kwanza kumfukuza adui umasikini kwa njia zilizo wazi, shirikishi katk taifa/nchi
Tukome kupambana na ujinga badala yake tujadili maboresho ya Elimu na kubadilisha mitaala ya elimu kuendana na wakati.
I think something is missing katika hoja zako. Mfano;
Hebu eleza basi, hivi mtu atakomaje kupambana na ujinga. Njia gani atumie kuondoa huo ujinga wake..?
Na eleza basi, ni kwa vipi elimu na viambata vyake itaboreshwa katikati ya viongozi/serikali inayopuuza HAKI, inayopuuza na kutojali utawala bora na katikati ya serikali yenye viongozi wezi na mafisadi wenye kuiba fedha yote iliyopaswa kwenda kwa watu/wananchi ili iboreshe elimu yao na viambata vyake?
Tukome kupambana na maradhi, tujadili kuboresha AFYA zetu na miumdombinu ya afya.
How?
Katikati ya serikali corrupt? Really?
Ndugu, utakuwa unatwanga maji kwenye kinu chako..
Kabla ya kufikiri haya kwanza, lipo Moja la kufanya ndipo uende kwenye hatua ya kufanya na kuboresha..
Jambo hilo ni: Tengeneza mifumo thabiti ya kikanuni, kisheria na kikatiba itakayooziba au kupunguza kwa 95% mianya ya utapanyaji rasrimali kama fedha, madini, misitu, ardhi na rasrimali watu ambazo ndizo nyenzo za kuboresha haya afya, elimu, barabara, umeme nk
Tusipambane na Rushwa, dhuluma bali tuhubiri na kuongelea HAKI.
Bado swali langu ni lilelile: HOW?
Haki itatoka wapi iwapo dhuluma na rushwa ndiyo inayotawala ktk jamii?
Au hujui au umesahau kuwa dhuluma na rushwa ni kikwazo cha haki? Kipi kianze kutoka kwanza? Bila shaka ni dhuluma na rushwa. Kisha panda HAKI na iendelee kuipalilia. Swali kubwa bado ni HOW..?
Na kwanini unadhani Adv. Boniface Mwabukusi na TLS unawaona kuwa ni kikwazo kupambana na rushwa, dhiluma? Kwa namna gani ni kikwazo..?
Tusipambane kuipinga DP world bali tujadili na kuweka wazi jinsi DP world itanufaishaje Taifa Sasa na vizazi vijavyo.
Wenzio huko serikalini wanajua hili?
Unatambua kuwa uwepo wa kitu au jambo baya tayari moja kwa moja inakuwa ni kikwazo? Uwepo wa DP WORLD kwa namna tu alivyoingia moja kwa moja ni tatizo..
Njia ya kufanya Ili ku - harmonize mambo ni kumwambia:
DP WORLD tunakuhitaji, ila umeingilia mlango wa nyuma usiorihusiwa. Toka kwanza kisha ingia kwa upya, tupatane upya kisha ufanye kazi na sisi kwa upya. Ni hivyo tu..!
Tusipambane na wajomba zetu wa Oman na wa Dubai sababu mjomba ndio mama bali tuangalie na kutazama kwa jinsi ya kunufaika kutoka kwa wajomba zetu.
Hatuna shida na wajomba sisi. Lakini wanapokuja kwa hila Ili kutuibia, ujomba wa namna hiyo hauna maana yoyote kwetu. Ni lazima tupambane na ujomba wa namna hiyo. Au wewe huamini kuwa mjomba anaweza kukubakia mwanao? Huamini kuwa mjomba anaweza kukuibia kila kilicho chako?
Basi shauri lako na ukiwa hivi Utakuwa na kiwango cha chini sana cha awareness katika maisha na kuishi kwako. Na ukiwa hivi, utaliwa sana ktk dunia hii..!
All in all hongera sana Rais Mwabukusi.
Ni vyema kuwa umemwa - aknowledge, lakini katikati ya andiko lako kuna kuuma na kupuliza kwingi. Kuna kujichanganya mwenyewe (self contradict) kwingi...
Hujulikani wewe ni wa Baridi au wa moto. Nimeona uvuguvugu mwingi katika mawazo na hoja zako. Lakini kumbuka hili Bwana wa mbingu na nchi asema hivi, walio vuguvugu watatapikwa tu..!
Amua Leo, uwe wa moto au baridi.
Asante, na kila kheri...