Tujikumbushe Kauli hii ya Rais Samia Atafanya Kazi na TLS ya Aina Gani? Hizi ni Salaam kwa Mwabu,. Swali ni is He A Bow Down Type or a Stand Firm?.

Tujikumbushe Kauli hii ya Rais Samia Atafanya Kazi na TLS ya Aina Gani? Hizi ni Salaam kwa Mwabu,. Swali ni is He A Bow Down Type or a Stand Firm?.

Wanabodi,
Wakati tukisubiri salaam za pongezi za mihimili kwa rais mpya wa TLS, sio vibaya tujikumbushe kauli hii ya Rais Samia atafanya kazi na TLS ya aina agani!

View: https://youtu.be/fZ7MWhPeyko?si=LtHTK8wfeAXMAtun
Hizi ni kama salaam kwa rais mpya wa TLS, Wakili Boniphase Mwabukusi .
Swali nI is he a bow down type or a stand firm type?.

Tusubiri time will tell, au tuanze kumfinyanga finyanga na mabandiko kama haya ili kumsaidia mtu wetu?.
Paskali.
Update
Mchango wa maana sana huu

You are a philosopher this is philosophical contribution.
Asante sana kwa hii
P

Samia ni rais wa nchi, Mwabukusi ni rais wa chama cha fani yake hivyo Mwabukusi hawezi kuwa juu ya utendaji kazi wa rais. TLS sidhani kama ilianzishwa ili ipambane na serikali, nadhani ilianzishwa ili mawakili wawe na jukwaa la kupeana mawazo kuhusu fani yao, chama hiki ni cha kitaaluma tofauti na vyama vya wafanyakazi ambavyo vina uharakati ndani yake, hivyo Mwabukusi na Samia tofauti zao suluhu yao ni mahakama na bunge, haya ni mawazo yangu si lazima yakubaliwe.
 
Mara nyingi watu firm wanalambishwa asali.

Kama Mwabu anataka kufika mbali asikubali kulambishwa asali akatema BIG G.

Namuona mbali sana kwa misimamo yake ,atazame kwa Pole Pole alivyokuwa before kulambishwa asali na sasa.
Huyu jamaa siyo muoga kumbuka alikuwa mtumishi wa ofisi ya DPP akaachia ngazi siyo mtumwa wa pesa
 
Wanabodi,
Wakati tukisubiri salaam za pongezi za mihimili kwa rais mpya wa TLS, sio vibaya tujikumbushe kauli hii ya Rais Samia atafanya kazi na TLS ya aina agani!

View: https://youtu.be/fZ7MWhPeyko?si=LtHTK8wfeAXMAtun
Hizi ni kama salaam kwa rais mpya wa TLS, Wakili Boniphase Mwabukusi .
Swali nI is he a bow down type or a stand firm type?.

Tusubiri time will tell, au tuanze kumfinyanga finyanga na mabandiko kama haya ili kumsaidia mtu wetu?.
Paskali.
Update
Mchango wa maana sana huu

You are a philosopher this is philosophical contribution.
Asante sana kwa hii
P
 
Mara baada ya mwezi mmoja anaanza kutumia maneno kama kuuburuza , kuupiga , mwingi
 
Sawa tutaona input yake itakuwaje
Kwanini mnapenda vita na wanao usema ukweli kwa asili yake? Kwani serikali haijazoea kuwa na ukweli? Inamaana mtu akiwa mkweli basi ni mwana harakati? Punguzeni roho za ubinafsi kwa sababu wanao usema ukweli ni watanzania na wao ni washiriki wazuri wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa lao
 
Ndugu Mayala nakuheshimu mno, lakini hapa umepotoka.

Mosi, TLS ni chombo cha kisheria. Kinaongozwa kwa kanuni, taratibu na miongozo wala siyo matakwa ya mtu binafsi, sera au miongozo ya chama chochote cha kisiasa, kikabila au kidini.

Pili, TLS ni chombo cha kitaaluma cha wanasheria chenye malengo makuu ya kusimamia na kulinda katiba ya nchi, utawala bora, haki za wananchi, na kuimarisha taaluma ya sheria nchini. Hivyo hata Raisi awe MALAIKA, NABII au MTUME, kama hafuati sheria na katiba ni lazima tutamvaa tu na kumbagaza kwasababu sheria imeturuhusu kufanya hivyo.

Tatu, any law society in the world, by its nature is a de facto political organisation, because law in itself is a political phenomenon. Utofauti tu ni kwamba sisi wanasheria hatugombanii nafasi za kisiasa wala kutumia ilani za vyama, bali tunafanya Political, Social and Economic Commentary/Scrutiny on daily undertakings of the Government ili kuhakikisha serikali inafuata kanuni za utawala bora, haki za raia na kuheshimu katiba.

Nne, kuendelea kupambana na wanasheria na kudhoofia taaluma kwa kupitia vyombo vya dola ni kujipiga risasi mguuni. Jambo ambalo wengi hamlifahamu ni kwamba mabadiliko mengi ya kisiasa na kiuchumi hapa nchini Tanzania yameletwa na wanasheria na siyo vyama vya siasa.

WANASHERIA WAZALENDO, wenye ujasiri ambao walihatarisha uhai wao walisamami kidete kuhakikisha Tanganyika/Tanzania inafika hapa ilipo leo. Yote haya uyaonayo kama THE BILL OF RIGHTS, MULTI-PARTY DEMOCRACY, LAW REFORM COMMISSION, THE UNION OF TANZANIA are a result of machinations of our by gone Brilliant Lawyers.

Wakina Mzee Nyalali, Lugakingira, Makame, Makani, Mwalusanya, Chipeta, Samata, Mwakasendo, wangekuwa wanataka kumfurahisha Mzee Nyerere kama ambavyo wengi wenu mnataka TLS ifanye nadhani leo hii tungekuwa na nchi ya ajabu mno hapa Afrika Mashariki.

Raisi Samia aamue kusuka au kunyoa. Vita dhidi ya wanasheria inaweza kuonekana ni jambo zuri mno, lakini ukiiharibu taaluma na kuwafundisha wanasheria wa Tanzania michezo ya rushwa, vitisho na uzandiki, atakayeumia ni watanzania wote siyo TLS.

NB: Hata Raisi Samia mwenyewe amekalia hicho kiti chake cha Uraisi vizuri bila shida kwasababu kuna wanasheria wazalendo hapa nchini ambao walishauri apewe nchi kwa kufuata katiba, hata kama mfumo ulikuwa umeshamkataa na ulikuwa radhi kutumia mbinu yoyote ile asipate Uraisi mwaka 2021.

Hivyo akidhani kwamba sisi TLS tunapambana na Personality then she'll be dead wrong kwasababu hata yeye siku mfumo dume unashika hatamu, hasahasa kuelekea 2025, watakaomlinda na kumetetea kwa kufuata katiba ni sisi TLS na wanasheria wenye UZALENDO NA MAADILI.

Hebu wacheni hizi mambo zenu za kujipendekeza kwa watawala.
 
Wengine wamekusifu kwamba you're article is very philosophical. Mimi naku - challenge kwa sababu hueleweki wewe ni wa MOTO au BARIDI. Mimi nilichoona kwenye article yako ni falsafa laghai, ya ujanja janja wa kucheza na maandishi na potofu kabisa kwa 90%..

Mtu makini akisoma kwa utulivu andiko lako, atatambua moja kwa moja kuwa wewe ni walewale watu wa kumsifu Mfalme/malkia hata kama anatembea uchi barabarani badala ya ku - shout na kumwambia; "...Helloooo mfalme/malkia uko uchi.." badala yake mtapaza sauti zenu na kusema "...Helloooo mfalme/malkia umependeza kweli..". Huu ni UNAFIKI..!

Nita highlight kila hoja yenye upogo na kukueleza kwanini Iko hivyo. Na ukiweza unaweza kujibu, la huwezi chukua kisha kaa kimya hukohuko uliko utafakari..

Twende kazi👇
Hakuna mkate mgumu kwa chai.
Mwabukusi akiangalia macho ya Rais Samia kwa utulivu, hakika atapata utulivu wa nafsi.
Kwa hiyo mnajiandaa kumnunua/kumhonga (kuuyeyusha mkate kwa chai ya moto?) Halafu Ili iweje? Tuendelee kuishi ktk impunity?

Hebu fafanua una maana gani hapa..
Mwabukusi itampasa atoke kwenye mode ya kuwa mwanaharakati( fight & flight mode) ili mapigo yake ya moyo yaendane sawa na mapigo ya moyo ya Rais Samia na serikali yake.
Hii dhana ya "uanaharakati" (activism) toka kwako tena na watu kama Pascal Mayalla mnaelewa hata maana na utendajikazi wake kweli ktk jamii huru inayozingatia utawala bora na wa haki?

I don't see anything tangible in you. Nakuona ni kama mtu mwenye ufahamu na uelewa fulani lakini ukiu - misuse big time matumizi yake kwa hila au kwa nia ovu..!
2024 na 2025 tunakwenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Sisi watanzania kwa ujumla tunapaswa kuhakikisha mapigo yetu ya moyo yanakwenda sawa na mapigo ya moyo ya Rais Samia na serikali yake( coherence).
Wewe na sio Watanzania wote, please..!!

Unataka mapigo yetu ya moyo yaende sawa na huyu mama ambaye ni a big failure president? Really?

No. Tumsaidie by telling her the naked truth, kwa kumkosoa na kumkemea Ili akikubali, then awe the good president Ili tuanze kumpongeza...

Kwa kauli na matendo yake yeye kama Rais na chama chake - CCM it's open that, wamejiandaa kuharibu na kuvuruga chaguzi zote kama walivyofanya miaka yote. Yet unataka mapigo ya mioyo yetu yawe cohesive na yake..?

You're absolutely insane ndugu Mr/Ms Adverse Effect..!!
Ni wazi pasi na shaka kuwa moyo wa Rais Samia umejaa upendo kwetu sote na kwa watanzania kwa ujumla ila lazima tutambue Rais Samia yeye peke yake bila ya sisi sote kumsapoti kwa pamoja hatofika mbali au atafika akiwa amechoka. TUMSAIDIE!
Hapa at least umekiri jambo muhimu sana. Yes, she's a human being. She's not perfect. Anahitaji kusaidiwa.

Shida Moja mliyonayo nyie watu wake akiwemo huyu mzee Pascal Mayalla hamjui ni msaada gani muhimu anaostahili kupewa huyu mama..!!!

Mnadhani kuwa kwa kumsifu kwa sifa za kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa ndiko kumsaidia?

Tunawaambia wazi kuwa, huku si kumsaidia bali kumpoteza na kumdidimiza chini kabisa..

Kumsaidia Rais ni kufanya hivi:

1. Kumwambia ukweli anapokosea yeye binafsi au wasaidizi wake na serikali yote kwa jumla anayoingoza.

Mfano tumwambie ukweli kuwa, kwa kulea sheria mbovu, kulea wasaidizi wake wezi na mafisadi na wasiozingatia na kuheshimu utawala bora unaozingatia sheria na Katiba, yeye Rais kukataa kurekebisha mifumo ya utawala kwa kufanya major constitutional amendments, yeye Rais kukataa kuendeleza mchakato wa kuandika katiba mpya shirikishi ili imsaidie ku - facilitate michakato ya kimaendeleo ktk nchi nk, basi afahamu kuwa hiyo ni shida na ni changamoto kwa nchi na taifa zima..

Huu ndiyo mwelekeo wa Adv. Boniface Mwabukusi na TLS ya Sasa anayoiongoza. Sasa hebu sema Kuna ubaya gani kwake kuchukua uelekeo huo huu?
Siasa za harakati na siasa za kupambana kwa hulka na tabia ya Rais wetu Samia hazitakuwa na mashiko Wala tija katika chaguzi zijazo.
Nani anapambana na nani hapa?

Mfano ni upi hasa wa mapambano unaoweza kuutoa hapa Mr/Ms Adverse Effect Ili pengine utaeleweka na kuungwa mkono?

Au unaandika tu kwa kutumia mapenzi ya hisia, yasiyo na uhalisia..?

Hivi watu wanaposema kwa mfano;

"...hapana, hapa Rais na serikali yako mmekosea badala yake ingekuwa vyema mngefanya hivi au vile..";

au

"...hapana, hapa Rais, serikali na Bunge kwenye mkataba huu mmekosea, ni mbaya na madhara yake kwa nchi ni 1, 2, 3.
.."

Je, ndo kusema kwamba mtazamo na ufahamu wako huu, kumbe huku ndiko kufanya siasa za harakati na kupambana? Really? Mimi naamini, kama ni hivi basi haya ni mapambano mazuri sana yenye lengo zuri kabisa la kukomesha uhalifu wa kisheria na utawala bora!

Kama wewe na mwenzako Pascal Mayalla na wengine wenye fikra za dizaini yenu ndivyo mnavyoelewa, basi ninyi ni BURE KABISA, mmepotea na hamna msaada wowote kwa nchi na taifa hili huku nyie kwa "ujinga" wenu mikijidhania kuwa mnalisaidia taifa na viongozi wake ukweli ukiwa ni kinyume chake.!!
Miaka 60 ya uhuru kama nchi tumepambana na umasikini tumeshindwa, tumepambana na ujinga tumeshindwa halikadhalika kwenye maradhi, rushwa, ufisadi n.k.
Eleza ni kwanini unadhani tumeshindwa? Je, ni kwa sababu ya wanaharakati? Wepi hao na kwa namna gani wamefanya tushindwe..?
Sote kwa pamoja tunapaswa kubonyeza button ya switch off fight and flight mode na kuwasha button ya utulivu na uamsho mode ili kuweza ku match na kuongea lugha moja
badala ya lugha gongana.
Ndugu Adverse Effect, button ya utulivu, uamsho mode ni hii: HAKI, HAKI, HAKI na HAKI ikitawala tunakuwa na AMANI na AMANI ikitawala watu watakuwa na furaha na upendo, hakuna ugomvi na kulaumiana tena.

Wapuuze watu kama kina kavulata ambao wanadai na kuamini kuwa duniani hakuna haki. Ni waongo na hawajui wasemalo na wanachokiamini. Mungu anasema:

"...Haki huinua taifa na watu waovu watawalapo, watu huugua/huumia..."

Na Mungu anaposema akatokea binadamu akapinga, huyo ni mjinga na baba yake huyo ni Ibilisi. Hapo Mungu amesema. Na kwa hiyo HAKI duniani inaweza kuwepo kama hatutaruhusu waovu watutawale..!
Kwa kuwa tumejifunza kwamba hakuna faida kubwa kwenye kupambana basi hatuna budi kubadilisha gea angani.
Badilisha gia huko huko angani kwa kuanza kuusema ukweli.

Waambieni watawala ukweli kwa lugha yoyote wanayoweza kuielewa. Mwabukusi anaweza kazi hii..
Ushauri wangu kwa Rais wa TLS Mwabukusi, wanazuoni wote kwa ujumla na wananchi tuacheni KUPAMBANA sababu kupambana hakujawahi kutusaidia na kutufikisha tunapotarajia au tunapotaka.
Kwa mwelekeo na mission ya Adv. Boniface Mwabukusi na TLS anayoingoza sasa, dhana ya "kupambana" (makabiliano ya ugomvi usiojenga) ni ni tafsiri yako wewe ndugu Adverse Effect na kwa 109% hiyo yako ni tafsiri potofu...!

Nimekuambia huko👆juu na nakuambia tena hapa kuwa, kukemea viongozi wezi na mafisadi, viongozi wavunja sheria, viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya (abuse of powers) kuonea na kunyanyasa watu wengine, viongozi wavunja taratibu na katiba, viongozi wanaonajisi utawala bora wa kuzingatia kanuni, sheria na Katiba nk haya si mapambano hasi kama unavyotafsiri wewe Bali haya ni mapambano chanya mazuri yenye nia ya kujenga utawala bora na kuleta ukombozi kwa watu wote..
Tukome kupambana na umasikini tuongelee na kujadili UTAJIRI tuliyokuwa nao.
Eleza utakomaje kupambana na umasikini...........

Na eleza utajadilije UTAJIRI bila kwanza kumfukuza adui umasikini kwa njia zilizo wazi, shirikishi katk taifa/nchi
Tukome kupambana na ujinga badala yake tujadili maboresho ya Elimu na kubadilisha mitaala ya elimu kuendana na wakati.
I think something is missing katika hoja zako. Mfano;

Hebu eleza basi, hivi mtu atakomaje kupambana na ujinga. Njia gani atumie kuondoa huo ujinga wake..?

Na eleza basi, ni kwa vipi elimu na viambata vyake itaboreshwa katikati ya viongozi/serikali inayopuuza HAKI, inayopuuza na kutojali utawala bora na katikati ya serikali yenye viongozi wezi na mafisadi wenye kuiba fedha yote iliyopaswa kwenda kwa watu/wananchi ili iboreshe elimu yao na viambata vyake?
Tukome kupambana na maradhi, tujadili kuboresha AFYA zetu na miumdombinu ya afya.
How?

Katikati ya serikali corrupt? Really?

Ndugu, utakuwa unatwanga maji kwenye kinu chako..

Kabla ya kufikiri haya kwanza, lipo Moja la kufanya ndipo uende kwenye hatua ya kufanya na kuboresha..

Jambo hilo ni: Tengeneza mifumo thabiti ya kikanuni, kisheria na kikatiba itakayooziba au kupunguza kwa 95% mianya ya utapanyaji rasrimali kama fedha, madini, misitu, ardhi na rasrimali watu ambazo ndizo nyenzo za kuboresha haya afya, elimu, barabara, umeme nk
Tusipambane na Rushwa, dhuluma bali tuhubiri na kuongelea HAKI.
Bado swali langu ni lilelile: HOW?

Haki itatoka wapi iwapo dhuluma na rushwa ndiyo inayotawala ktk jamii?

Au hujui au umesahau kuwa dhuluma na rushwa ni kikwazo cha haki? Kipi kianze kutoka kwanza? Bila shaka ni dhuluma na rushwa. Kisha panda HAKI na iendelee kuipalilia. Swali kubwa bado ni HOW..?

Na kwanini unadhani Adv. Boniface Mwabukusi na TLS unawaona kuwa ni kikwazo kupambana na rushwa, dhiluma? Kwa namna gani ni kikwazo..?
Tusipambane kuipinga DP world bali tujadili na kuweka wazi jinsi DP world itanufaishaje Taifa Sasa na vizazi vijavyo.
Wenzio huko serikalini wanajua hili?

Unatambua kuwa uwepo wa kitu au jambo baya tayari moja kwa moja inakuwa ni kikwazo? Uwepo wa DP WORLD kwa namna tu alivyoingia moja kwa moja ni tatizo..

Njia ya kufanya Ili ku - harmonize mambo ni kumwambia: DP WORLD tunakuhitaji, ila umeingilia mlango wa nyuma usiorihusiwa. Toka kwanza kisha ingia kwa upya, tupatane upya kisha ufanye kazi na sisi kwa upya. Ni hivyo tu..!
Tusipambane na wajomba zetu wa Oman na wa Dubai sababu mjomba ndio mama bali tuangalie na kutazama kwa jinsi ya kunufaika kutoka kwa wajomba zetu.
Hatuna shida na wajomba sisi. Lakini wanapokuja kwa hila Ili kutuibia, ujomba wa namna hiyo hauna maana yoyote kwetu. Ni lazima tupambane na ujomba wa namna hiyo. Au wewe huamini kuwa mjomba anaweza kukubakia mwanao? Huamini kuwa mjomba anaweza kukuibia kila kilicho chako?

Basi shauri lako na ukiwa hivi Utakuwa na kiwango cha chini sana cha awareness katika maisha na kuishi kwako. Na ukiwa hivi, utaliwa sana ktk dunia hii..!
All in all hongera sana Rais Mwabukusi.
Ni vyema kuwa umemwa - aknowledge, lakini katikati ya andiko lako kuna kuuma na kupuliza kwingi. Kuna kujichanganya mwenyewe (self contradict) kwingi...

Hujulikani wewe ni wa Baridi au wa moto. Nimeona uvuguvugu mwingi katika mawazo na hoja zako. Lakini kumbuka hili Bwana wa mbingu na nchi asema hivi, walio vuguvugu watatapikwa tu..!

Amua Leo, uwe wa moto au baridi.

Asante, na kila kheri...
 
Mwabukusi kaonyesha udhaifu wake akiwa kiongozi wa taasisi ya kisheria. Kwa bahati mbaya kwake waliowahi kuiongoza TLS wameacha viwango vya kiutendaji na vimekuwa ni deni kwake.

Nilimsikia akihutubia akiwa kazungukwa na wanasheria, anatumia maneno ya mtaani yasiyoendana na nafasi yake kwa sasa.

Pia suala la DPW kushindwa kwake kesi aliyofungua kupinga uwekezaji inaacha doa kwa mtu makini mwenye kuupima uwezo wa Rais wa Taasisi ya kisheria.

Jazba zake na ile 'superiority complex' aliyonayo ni ufa mwingine wenye kuweza kutumiwa na 'mfumo' katika kumuwekea mtego wa kumshusha thamani ikitokea akaanza kazi akiwa na mitazamo ya kiugomvi na dharau dhidi ya Mamlaka za nchi.

Lissu anafanana na Mwabukusi katika kule kushindwa kuudhibiti ule ukubwa wanaojipa wenye kusababishwa na elimu zao za sheria.

Lakini anguko la mjuzi siku zote lipo humo humo katika elimu pana inayokuwa kichwani mwake.
 
Ndugu Mayala nakuheshimu mno, lakini hapa umepotoka.

Mosi, TLS ni chombo cha kisheria. Kinaongozwa kwa kanuni, taratibu na miongozo wala siyo matakwa ya mtu binafsi, sera au miongozo chama chochote cha kisiasa, kikabila au kidini.

Pili, TLS ni chombo cha kitaaluma cha wanasheria chenye malengo makuu ya kusimamia na kulinda katiba ya nchi, utawala bora, haki za wananchi, na kuimarisha taaluma ya sheria nchini. Hivyo hata Raisi awe MALAIKA, NABII au MTUME, kama hafuati sheria na katiba ni lazima tutamvaa tu na kumbagaza kwasababu sheria imeturuhusu kufanya hivyo.

Tatu, any law society in the world, by its nature is a de facto political organisation, because law in itself is a political phenomenon. Utofauti tu ni kwamba sisi wanasheria hatugombanii nafasi za kisiasa wala kutumia ilani za vyama, bali tunafanya Political, Social and Economic Commentary/Scrutiny on daily undertakings of the Government ili kuhakikisha serikali inafuata kanuni za utawala bora, haki za raia na kuheshimu katiba.

Nne, kuendelea kupambana na wanasheria na kudhoofia taaluma kwa kupitia vyombo vya dola ni kujipiga risasi mguuni. Jambo ambalo wengi hamlifahamu ni kwamba mabadiliko mengi ya kisiasa na kiuchumi hapa nchini Tanzania yameletwa na wanasheria na siyo vyama vya siasa.

WANASHERIA WAZALENDO, wenye ujasiri ambao walihatarisha uhai wao walisamami kidete kuhakikisha Tanganyika/Tanzania inafika hapa ilipo leo. Yote haya uyaonayo kama THE BILL OF RIGHTS, MULTI-PARTY DEMOCRACY, LAW REFORM COMMISSION, THE UNION OF TANZANIA are a result of machinations of our by gone Brilliant Lawyers.

Wakina Mzee Nyalali, Lugakingira, Makame, Makani, Mwalusanya, Chipeta, Samata, Mwakasendo, wangekuwa wanataka kumfurahisha Mzee Nyerere kama ambavyo wengi wenu mnataka TLS ifanye nadhani leo hii tungekuwa na nchi ya ajabu mno hapa Afrika Mashariki.

Raisi Samia aamue kusuka au kunyoa. Vita dhidi ya wanasheria inaweza kuonekana ni jambo zuri mno, lakini ukiiharibu taaluma na kuwafundisha wanasheria wa Tanzania michezo ya rushwa, vitisho na uzandiki, atakayeumia ni watanzania wote siyo TLS.

NB: Hata Raisi Samia mwenyewe amekalia hicho kiti chake cha Uraisi vizuri bila shida kwasababu kuna wanasheria wazalendo hapa nchini ambao walishauri apewe nchi kwa kufuata katiba, hata kama mfumo ulikuwa umeshamkataa na ulikuwa radhi kutumia mbinu yoyote ile asipate Uraisi mwaka 2021.

Hivyo akidhani kwamba sisi TLS tunapambana na Personality then she'll be dead wrong kwasababu hata yeye siku mfumo dume unashika hatamu, hasahasa kuelekea 2025, watakaomlinda na kumetetea kwa kufuata katiba ni sisi TLS na wanasheria wenye UZALENDO NA MAADILI.

Hebu wacheni hizi mambo zenu za kujipendekeza kwa watawala.
Nimeupenda sana mchango wako..

Huu ni ukweli ulio wazi mno. Hawa kina Pascal Mayalla au Adverse Effect au kavulata ni wafuasi wa Sweetbert Nkuba, kada wa CCM aliyekuja kupandikizwa TLS wakidhani atakuwa Rais wa TLS..

Bahati mbaya kwao ni kuwa, mission yao imefeli na Sasa wanakuja na maandiko yanayouma na kupuliza lakini deep inside wakitafuta upenyo wa kupooza misimamo na mitazamo ya Rais mpya wa TLS..

Bahati mbaya kwao ni kuwa, sidhani kama wanaweza kumhonga chochote Adv Mwabukusi Ili a - compromise na mfumo corrupt wa serikali ya Rais Samia na CCM kwa jumla..

Kuna mtu mjumbe mmoja wa JF humu anaitwa Adverse Effect humu..

Huyu jamaa kaweka article yake (soma bandiko #5) huko juu la ajabu kidogo. Anaonekana ni mtu makini na msomi mzuri lakini nyuma ya pazia ni nyoka swila mwenye sumu kali. Utamtambua kwa kusoma maandishi yake..

Katika bandiko lake hilo kaanza kwa kusema "hakuna mkate mgumu kwa chai" . Bila shaka akimaanisha kuwa, hata Adv. Boniface Mwabukusi naye anaweza kuhongwa tu na serikali/CCM na akapoa na kisha ata - compromise na mfumo huu kandamizi wa haki na corrupt..

Na hii ni ishara kuwa, kumbe ni kweli kulikuwa na mkono wa serikali ktk uchaguzi wa TLS mwaka huu Ili kuuvuruga kwa kujaribu kuweka mtu wao Ili kuvunja meno ya TLS ishindwe kuuma kabisa pale inapopaswa kuuma..

Msome vizuri huyu Adverse Effect. Unaweza kudhani ni mtu mwenye Nia nzuri na TLS na Mwabukusi (Rais wa TLS Sasa). Lakini katikati ya maandishi yake utaelewa sura halisi ya mtu huyu..

Tuendelee kuiombea na kuipa support TLS.

Pamoja na CHADEMA, taasisi zingine zilizobaki ambazo hazijaingiliwa na mfumo corrupt wa ki-CCM na bado zina uthubutu wa kuikemea, kuionya na kuishauri serikali, Bunge na mahakama genuinely ni TLS..

Vyama vya wafanyakazi kama shirikisho lao yaani TUCTA, CWT, TUGHE, TALGWU nk wote hawa hakuna kitu, wameng'olewa meno..

Wafanyakazi wa nchi hii hawana mtetezi tena. Serikali na CCM wameweka vibaraka wao kama viongozi kwenye vyama vyao.

Hivi vyama vyao vya kuwatetea vinapitia ktk kipindi kigumu cha giza nene kwelikweli..
 
Very brilliant contribution..

Huu ni ukweli ulio wazi mno. Hawa kina Pascal Mayalla au Adverse Effect au kavulata ni wafuasi wa Sweetbert Nkuba, kada wa CCM aliyekuja kupandikizwa TLS wakidhani atakuwa Rais wa TLS..

Bahati mbaya kwao ni kuwa, mission yao imefeli na Sasa wanakuja na maandiko yanayouma na kupuliza lakini deep inside wakitafuta upenyo wa kupooza misimamo na mitazamo ya Rais mpya wa TLS..

Bahati mbaya kwao ni kuwa, sidhani kama wanaweza kumhonga chochote Adv Mwabukusi Ili a - compromise na mfumo corrupt wa serikali ya Rais Samia na CCM kwa jumla..

Kuna mtu anaitwa Adverse Effect humu. Kaweka article yake (soma bandiko #5) huko juu. Katika bandiko lake hilo kaanza kwa kusema "hakuna mkate mgumu kwa chai" bila shaka akimaanisha kuwa, hata Adv. Boniface Mwabukusi naye anahongeka tu Ili a - compromise na mfumo..

Na hii inaonesha kuwa, kumbe ni kweli serikali hii corrupt ilikuwa ivuruge uchaguzi huu kwa kuweka mtu wao Ili kuvunja meno ya TLS ishindwe kuuma kabisa pale inapopaswa kuuma..

Msome vizuri huyu Adverse Effect. Unaweza kudhani ni mtu mwenye Nia nzuri na TLS na Mwabukusi (Rais wa TLS Sasa). Lakini katikati ya maandishi yake utaelewa sura halisi ya mtu huyu..

Tuendelee kuiombea na kuipa support TLS.

Pamoja na CHADEMA, taasisi zingine zilizobaki ambazo hazijaingiliwa na mfumo corrupt wa ki-CCM na bado zina uthubutu wa kuikemea, kuionya na kuishauri serikali, Bunge na mahakama genuinely ni TLS..

Vyama vya wafanyakazi kama shirikisho lao yaani TUCTA, CWT, TUGHE, TALGWU nk wote hawa hakuna kitu, wameng'olewa meno..

Wafanyakazi wa nchi hii hawana mtetezi tena. Serikali na CCM wameweka vibaraka wao kama viongozi kwenye vyama vyao.

Hivi vyama vyao vya kuwatetea vinapitia ktk kipindi kigumu cha giza nene kwelikweli..
Mkuu, Tanzania yetu iliyopata uhuru wa kuomba imejengwa na WANASHERIA.

Binafsi huwa nawashangaa mno watu ambao wanadharau mchango wa TAALUMA YA SHERIA kwenye ujenzi wa taifa la Tanganyika/Tanzania. Huwa nasema hafahamu kabisa historia ya wapi hii nchi yetu imetoka. Hebu zingatia hii mifano:

Mosi, mwaka 1961, WANASHERIA WAZALENDO ndiyo walimshauri Mzee Nyerere atunge sera maarufu iitwayo "Nyerere's Doctrine of State Succession" ambayo iliisaidia Tanganyika kuweza kujitoa kwenye mikataba mingi ya hovyo ya kikoloni ambaye ingelidhuru taifa letu jipya.

Mpaka kufika mwaka 1976, Nyerere's Doctrine of State Succession ilikuwa imeigwa na mataifa sita ya Afrika yakiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Msumbuji n.k

Pili, Mwaka 1962, WANASHERIA WAZALENDO ndiyo walimshauri Mzee Nyerere na Waziri Job Lusinde wajitoe kwenye mkataba wa kikoloni wa Belbase (Belbase Treaty 1951) ambao uliziua bandari za Kigoma na Dar es salaam kwa Mkoloni Mbelgiji aliyetawala Congo na Rwanda-Urundi.

Tatu, Mwaka 1963, WANASHERIA WAZALENDO ndiyo walimshauri Mzee Nyerere kuhusu sera ya The Intangibility of Frontiers, ambayo aliipendekeza OAU kwamba mipaka ya kikoloni waliyoikuta ni lazima iheshimiwe. Mpaka leo Afrika ina amani kwasababu ya wanasheria wazuri kutoka Tanganyika.

Nne, Mwaka 1969, WANASHERIA WA TANGANYIKA kupitia mahakama kuu walitoa maamuzi yaliyompa mwanamke mjane haki ya kumiliki mali za mume wake. Jambo hili lilikuwa geni barani kote Afrika, ila Tanganyika ikawa moja ya nchi za kwanza kabisa kufanya maamuzi ya namna hii ambayo yalilenga kumkomboa mwanamke kiuchumi.

Tano, LAW REFORM COMMISSION ilivyoanzishwa mwaka 1977, ni WANASHERIA WAZALENDO kama Pius Msekwa walipendekeza kwamba baadhi ya sheria za Tanzania zilikuwa kandamizi na za kikoloni hivyo iundwe tume maamulumu kuhakikisha Tanzania haiachwi nyuma na mabadiliko ya dunia. Hii tume CCM waliipiga vita kwelikweli na imepoteza mwelekeo.

Sita, THE RE-INCLUSION OF THE BILL OF RIGHT IN THE CONSTITUTION 1984, uliletwa na WANASHERIA WAZALENDO wa nchi hii ambao walipiga kelele dhidi ya serikali ya Mzee Nyerere ambayo ilikuwa inaongoza kibabe na kuvunja haki za binadamu kwa kiwango kikubwa mno.

Pia ikumbukwe hata kama kulikuwa hakuna BILL OF RIGHTS, Majaji shupavu wa Tanzania walibuni mbinu kuwawezesha wananchi kudai haki zao binafsi bila hata kutumia BILL OF RIGHTS. Majaji wengi walitishiwa na Mzee Nyerere na vikosi vya majasusi, hadi wengine kudhalilishwa hadharani lakini walikuwa jasiri kulinda katiba.

Saba, RE-INTRODUCTION OF MULTIPARTISM IN TANZANIA, ililetwa na mapendekezo ya NYALALI COMMISSION. Huyu Nyalali ndiyo alikuwa JAJI MKUU wa Tanzania kwa wakati huo. Mbali na kusema kwamba asilimia 80% ya watanzania walikataa vyama vingi, lakini wanasheria na Mzee Nyerere waliona ni heri kuwa na vyama vingi Tanzania.

Mchango wa TAALUMA YA SHERIA hapa nchini Tanzania ni mkubwa kuliko hata mchango wa vyama vya siasa. Kipindi chote cha mfumo wa chama kimoja, waliotetea wananchi walikuwa ni UDSM FACULTY OF LAW, THE JUDICIARY na TLS. Haya mapambano dhidi ya taaluma ya sheria yaliyoanzishwa na Jakaya Kikwete hadi kuendelea leo hii yatalifikisha taifa pabaya mno.

Mara nyingi watu firm wanalambishwa asali.

Kama Mwabu anataka kufika mbali asikubali kulambishwa asali akatema BIG G.

Namuona mbali sana kwa misimamo yake ,atazame kwa Pole Pole alivyokuwa before kulambishwa asali na sasa.
Muda utazungumza

Uteuzi
Asali, pesa, maokoto, hela.
 
Wooh..!

Asante kwa kumbukumbu nzuri za kihistoria..

Mengine honestly, nilikuwa hata siyajui..

Sasa naelewa kwanini mfumo huu corrupt una vita kubwa na TLS na wanasheria kwa ujumla..

Sasa ni naelewa vizuri ni kwanini wanasheria wa aina ya Boniface Mwabukusi, Tundu Lissu, Kibatala, Matata, Peter Madeleka and others wenye misimamo mikali dhidi ya dhuluma, rushwa, ufisadi na uvunjifu wa HAKI na KATIBA wanapigwa vita na kutotakiwa kabisa kuwa viongozi wakuu wa taasisi (TLS) hii muhimu kwa ustawi, mafanikio na maendeleo ya kijamii..

Asante ndugu MALCOM LUMUMBA
 
Itikadi ya Ukomunisti au Ujamaa ni Ushetani. Ilaaniwe.

Miongoni mwa misingi ya Itikadi ya Ukomunisti au Ujamaa ni Juche ambayo inaamini kwamba:-
1. Raia wote waliopo kwenye nchi wanachukuliwa kama ni 'mateka wa Mwenyekiti'
2. Mwenyekiti ndio mtu pekee kabisa katika nchi ambaye Ana akili kubwa zaidi na nzuri zaidi kuliko mtu mwingine yoyote yule.
The reality. Huu ndio ukweli wenyewe.

Nilishangaa sana kuona rafiki zangu wakisherehekea kwa nguvu sana ushindi wa Mwabukusi. Eti umewarudishia matumaini! Siamini kwamba hawa watu na akili zao hawajui tuko kwenye nchi ya aina gani.

Rais wa JMT yuko juu ya katiba, sheria zote, mihimili yote ya utawala wa nchi. Ana uamuzi wa mwisho juu ya fani zote za maisha ya Watanzania. Hivyo basi, hiyo TLS na Mwabukusi wajijue wamesimama wapi vs huyo kiongozi wa nchi na serikali yake.

It’s a completely hopeless situation. Hata kulambishwa asali itakuwa labda kwa kutaka kuonyesha ustaarabu/uungwana tu. Rais wa JMT anaweza kuipigisha magoti TLS na Mwabukusi wake bila hata ya asali kutumika. Sadly wako wengi wanaoukubali na kuushabikia mfumo huu wa “Juche”. Kwao ni “natural”. Comments zao kibao zinaendelea kutiririka humu.
 
Wanabodi,
Wakati tukisubiri salaam za pongezi za mihimili kwa rais mpya wa TLS, sio vibaya tujikumbushe kauli hii ya Rais Samia atafanya kazi na TLS ya aina agani!

View: https://youtu.be/fZ7MWhPeyko?si=LtHTK8wfeAXMAtun
Hizi ni kama salaam kwa rais mpya wa TLS, Wakili Boniphase Mwabukusi .
Swali nI is he a bow down type or a stand firm type?.

Tusubiri time will tell, au tuanze kumfinyanga finyanga na mabandiko kama haya ili kumsaidia mtu wetu?.
Paskali.

Wanabodi,
Kuna hoja kuwa kauli huwa zinaumba, sasa kuna hii kauli ya "Maharage ya Mbeya Maji Mara Moja", Jee kauli hii ina ukweli wowote kuwa ukipika maharerage ya sehemu nyingine zote, ili yaive lazima uongeze maji zaidi ya mara moja, lakini ukipika maharage ya Mbeya, ukiweka maji, ni mara moja tuu hadi yanaiva?.

Kama kauli hii ni kweli kwa maharage ya Mbeya, maji ni mara moja tuu, jee ni kwa maharage tuu au hata kwa wana Mbeya wenyewe yaani Wambeya, nao pia ni ukiwa na shida yoyote, maji ni mara moja tuu, wanatepeta, wanalainika, na kufikia maamuzi ya kukubali au kukataa jambo lolote, mara moja tuu, kirahisi rahisi, kiulani?.
Hata Wakili Mwabukusi ni mtu wa Mbeya, Pindi Chana kaonekana kupwaya hauwezi muziki wa Mwabukusi, sasa ameletewa Baba lao, Prof. Palamagamba Kabudi, amini nawaambieni mtamshuhudia jinsi Mwabukusi atakavyo lainika kama mkate mbele ya chai, mtamshuhudia Mwabukusi kama ni maharage ya Mbeya au la...!
P
 
Back
Top Bottom