Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

K
MR.MADOSHI (R.I.P) MHONGOLO SEC KAHAMA

Huyu teacher alinifukuzisha shule maana nilishindwa vumilia ukali wake

hiyo siku akakuta namimi nishamchoka liwalo na liwe,kweli tukavaana uso kwa face

sababu tu eti nmevaa sweta nimelikunja,Kanidaka akanipa Kofiii,nikainama chini sikio linalia swiiiiiiii

ile nimeinama akaongezea mijeledi ya mgongo kama mvua, nikaona usinitanie we FAZAAA

niliiinuka na kitofali sijui nilikichomoa kwenye bustani,Nilimtwika kitofa cha tumbo,ananifata bado

nikaokota kingina rusha akapangua,Mara huyu HAPA akanidaka Nikaona isiwe kesi nikamrukia shingo

nikawa nabembea nae nipo kwa mgongoni,ah ile mechi kama sio kuja kuingiliwa na Walinzi ingeisha Bila Bila

siku hiyo hiyo Nilisikia kengele imegongwa nikafukuzwa shule saaa 1 usiku,Naenda wapiii sasa usiku huo,Nikagoma

ondoka,Ah wee saa ngapi asije na difenda ya polisi nikabebwa nikaenda malizia usiku wangu Central asubuhi nikasafirishwa kwetu

ndio mwisho wakusoma ile shule,nilimchukia yule tcha sema ndo hvyo sikua na uwezo nilimuapia viapo vingi sana

Nilipokuja sikia SIR GOD kamnyakua Ajabu et roho ikaniuma nikaona kama Mungu kamuokoa na adhabu niliyompangia...

Dingiiii apumzike tu ila alinigombanisha sana na mshua wangu kwa chumvi alizoongeza.
Kuna ndugu yangu alisoma hiyo shule na yeye walimla kichwa kisa mapenzi. .Gunda alikuwa na mtoto wa kike mkali kinyama ila wenge.
 
Kitu nilicho kigundua ma teacher wakali kupitiliza walikuwa na matizo haya.
1. Uelewa wao wa masomo ya kufindisha ulikuwa mdogo hivyo ku apply intimidation method kufunika kaujinga kake.

2. Walitokea familia katili walitembezewa mboko utotoni kiasi hawakuweza kujitetea sasa wamekuwa hawana namna ya kulipiza kisasi kwa watesi wao na wana substute kwa kuwatandika na kuwa wakali kwa watoto wa shule.
3. Umalaya wa walimu wana wachalaza mboko hovyox2 ili siku akitaka kupita na kitoto cha kike kiwe kioga na kukubali kwa hofu ya mboko.
4. Ugumu wa maisha au tuseme kuwa na msongo wa mawazo.
Hakuna ukweli hapa, sidhani kama umefanya Research juu ya hili.
 
Nimeandika huu uzi baada ya kuwakumbuka waalimu wangu hasa wale wakuu wa miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni waliokuwa wakali sana wasiotaka masikhara kiasi cha kuweza kujulikana hadi mkoa mzima na kanda. Wafuatao walivuma sana kanda ya kaskazini;

1. Mwalimu Kibatala - Shule ya sekondari Karatu, Arusha.
2. Mwalimu Shayo - Shule ya Sekondari Arusha.
3. Mwalimu wa malezi Ilboru sec, jina limenitoka ila ana jina la kimasai. Waliosoma 1998 - 2001 wanaweza kumkumbuka.
4. Mwalimu Teti - Tanga technical Secondary school. Huyu mkuu wa shule ilikuwa sio poa...
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
6. Munga - Kaloleni sec, Arusha.
7. Kipingu -
8. Mwalimu Masatu na Mgimwa - Mkwawa High School (complex)
Ongezeeni majina mengine tujikumbushe enzi za u-teenage.
Kuna Dudu Tosamaganga
 
Galanos msocha alikuwa michosho sana
Mikwara tupo. Nipo form Six mwaka 2001 nilitoroka kwenye majani mapana. Jamaa akaniona usiku huo na kuniambia wewe ni mwanafunzi. Nikamkatalia. Hahaaaa kesho asubuhi kaja Assemble mi sikwenda akanikosa. Akaanza nitafuta madarasani namkwepa. Baada ya wiki akanikuta Assembly pale. Akaniita mbele nikamkatalia. Akaapa kama sio mimi aliyenikuta Majani Mapana usiku alafu namkatalia siku akinikuta tena atanivunja. Nikacheka. Hahaaaa akanipeleka kwa Headmaster kuwa nimemdharau na kumkataa kuwa sio mimi alinikuta majani mapana wakati ana uhakika kuwa ni mimi.
 
Sir Lightfoot Stonebridge Henry

Tabora Boys mwaka 1962

Huyu mwamba ilikuwa ukifanya kosa anakupa wosia mpaka analia yaani. Tulikuwa tunaogopa kumuudhi kwa jinsi alivyokuwa anasikitika. Anakufanya ujifeel guilty na kuwa na sympathy. Ndivyo alivyofanikiwa kubadili maisha ya baadhi yetu...Psychological manipulation!
Kaka kaka...1962????????
 
Looh inatakiwa isomeke father father, dingi dingi, mshua mshua .Kaka teeena wakati keshastafu utumishi wa uma.
Mm namuita kaka..kwa sbb huo umri anaosema humu ni wa uongo...
 
Nimeandika huu uzi baada ya kuwakumbuka waalimu wangu hasa wale wakuu wa miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni waliokuwa wakali sana wasiotaka masikhara kiasi cha kuweza kujulikana hadi mkoa mzima na kanda. Wafuatao walivuma sana kanda ya kaskazini;

1. Mwalimu Kibatala - Shule ya sekondari Karatu, Arusha.
2. Mwalimu Shayo - Shule ya Sekondari Arusha.
3. Mwalimu wa malezi Ilboru sec, jina limenitoka ila ana jina la kimasai. Waliosoma 1998 - 2001 wanaweza kumkumbuka.
4. Mwalimu Teti - Tanga technical Secondary school. Huyu mkuu wa shule ilikuwa sio poa...
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
6. Munga - Kaloleni sec, Arusha.
7. Kipingu -
8. Mwalimu Masatu na Mgimwa - Mkwawa High School (complex)
Ongezeeni majina mengine tujikumbushe enzi za u-teenage.
Ngoja kwanza utuweke sawa shule zote hizo ulizotaja ulisoma?
Umeambiwa au unatupanga ili na sisi tupite humo humo😂
 
Back
Top Bottom