Tujuzane mwenzenu nimeponea chupu chupu, je hali hii na kwenu Ipo?

Tujuzane mwenzenu nimeponea chupu chupu, je hali hii na kwenu Ipo?

Sikuwahi Kujua kuna mafua Makali kiasi hiki
Kama kweli huu ugonjwa wakutengenezwa na Mwanadamu basi Alaaniwe
Afu ndio miezi yake hii. Juzijuzi hapa Nilipata na mafua kidogo tu yale ya kuchirizika ila ndani ya siku mbili yakaisha yenyewe tuu. Sijaona dalili zingine zaidi. Labda sababu nilichanjaga.
 
kuna flu flani hivi imekaa kibabe mtaani na hasa Kwa watu wasiofanya mazoezi,jitahidini sana kufanya mazoezi hata yale ya viungo,tembea kidogo,push up fanya angalau utoke jasho itakusaidia sana kuukinga na magonjwa madogo madogo,mazoezi ni kinga moja kubwa sana ya mwili
 
Mi nlikuwa nmechoka tu viungo ka mtu kanipiga rungu..ila Sina mafua Wala Nini...ila kuna muda nlikuwa nashindwa kupumua vzur..Sasa sijajua kama ndo yenyew pia...ila kwa Sasa nipo fit...ni mazoez tu na kula tangawiz mbichi
 
Mimi na group O na siuguagi ovyo ovyo yaan mafua ni BALAA wiki 3 Mimi pia plus kuharisha Kama Bata yaan nilikua kifua kinauma, mafua naishiwa nguvu, loss appetite's

Mpaka nikaogipa Ila now alhamdudilah naendelea vyema mafua Yana ishilia ishilia.

Kuharisha na mafua/kifua, hiyo ni tayari kifaduro
 
Mimi wiki ya 3 na mafua makali Sanaa na tangu jumamosi nimekua naharisha Kama Bata mpaka naogopa

Kwa Sasa mafua yamepungua na kuhara kumepungua Ila Kuna mafua makali Sanaa Sanaa ni BALAA Sanaa nakubaliana na wewe

Pembeni yangu hapa Kuna watu nimekaa nao wanakohoa Sanaa
Mafua na kuharisha tena? 😹😹
Pima na wadudu wale walioanzia kagera
 
ila watu wa Dar bwanaa yaani mafua unayaandikia uzi kabisaa😂😂😂😂
 
Mimi wiki ya 3 na mafua makali Sanaa na tangu jumamosi nimekua naharisha Kama Bata mpaka naogopa

Kwa Sasa mafua yamepungua na kuhara kumepungua Ila Kuna mafua makali Sanaa Sanaa ni BALAA Sanaa nakubaliana na wewe

Pembeni yangu hapa Kuna watu nimekaa nao wanakohoa Sanaa
Aisee 🤔
 
Kuna mafua makali tu kwa sababu ya mabadilko ya hali ya hewa. Hata mwaka jana na juzi kipindi kama hiki yalitokea.
 
ila watu wa Dar bwanaa yaani mafua unayaandikia uzi kabisaa😂😂😂😂
Sawa bwana
Acha Dhihaka na Ugonjwa sio mafua uliyo yazoea Kuwa makini
 
Back
Top Bottom