Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Ni kweli, watu wanafanya personal attacks kuliko kujibu hoja
 
Kama serikali huwa inakopa bila mikopo kupitiwa na kupewa kibali bungeni Ndugai na Nape wako sahihi kuhoji mikopo na afya yake kwa uchumi wa taifa.
 
Aikane hoja yake, kisha sisi tuseme ni hoja yake? Kama kweli anaiamini hoja yake ajitokeze hadharani tumuunge mkono.
Halafu baada ya kumuunga mkono na uspika utampa?
Hofu yake kubwa ni uspika na si vinginevyo.
 

Mkuu Tua Ngoma ,upo sahihi kwa asilimia 100.
JPM aliwaaminisha "wanyonge" kuwa yeye hakopi, anafanya miradi kwa hela zetu za ndani. Na hilo ndilo lililo ndani ya vichwa vya Watanzania wengi masikini,kwamba JPM hakuwa akikopa wala kusaidiwa na mabeberu.
Leo anapotokea kiongozi mmoja na kuwa "alert" kwamba mikopo imezidi,wao lazima washituke.
Wanajiuliza,kwa nini tukope!? Mbona JPM aliweza bila kukopa!?
Washauri wa Samia ama hawajui athari za hii approach ya kupigia debe mikopo wazi wazi kwa Samia,au wanamwingiza chaka makusudi kwa sababu zao.
Hii "vita",nimeona wananchi wengi wa kawaida, hasa wa CCM wapo upande wa Ndugai wakiamini kuwa JPM hakuwa akikopa.
 
Mimi sipo na yeyote wapambane na hali zao.
 
Kaomba msamaha baada ya kutema nyongo.

Kwa sasa anajisikia mwepesii.
 
Samia asemae hela za tozoamepeleka wap.
 
Mimi naona ndugai ana hoja kwa kuwa tunakopa lakini bado huyu mtanzania anatwushwa mzigo wa Kodi kufanya kitu kilekile, huyo mama yao kapuyanga sana maana kama angetaka kumjibu ndungai angemwita huko kwenye vikao vya chama. mwanzo wa Babel kuanguka ni kupishana lugha kwaiyo chama kinatakiwa kujitazama.
 
Kama serikali huwa inakopa bila mikopo kupitiwa na kupewa kibali bungeni Ndugai na Nape wako sahihi kuhoji mikopo na afya yake kwa uchumi wa taifa.
Kama yuko sahihi, kwanini aliomba msamaha kwa kusema kitu anachoamini kiko sawa?
 
Jambo gani lilipitishwa bungeni na kulikosoa nnje ndugu The Monk !!??

Kwa mujib wa huu mjadala, spika alihoji kuhusu mikopo, kitu ambacho kinaweza kujadiliwa bungeni wakati wa budget. Sasa kama huko wanapitisha na hasemi chochote, iweje huku nje aseme kwamva anashangazwa na mikopo inavyoongezeka?
 
Vyovyote iwavyo, kukopa Trillioni 10 ndani ya miezi 9 kwa miradi isiyo ya kimkakati ni jambo lisilovumilika, hili ni lazima liondoke na mtu!
 
Bajeti ya 32T au 34T au 36 T ni ya serikali yote including taasisi zake ambazo hazitegemei makusanyo ya TRA kujiendesha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…