Tukio gani kwenye soka huwezi kulisahau?

Binafsi huwa nashabikia timu za epl uefa japo najua ni mbovu.
Sitasahau uefa 2019 timu zote zilipoingia fainali kimiujizaujiza.
come back ya liver na tottenham hatari sana siku ile ajax. Sikuangalia mechi sababu nilijua watatoka ila asubuhi naambiwa wamepita sikuamini.
 
Fainali ya Bayern vs Man UTD UEFA

Nakumbuka nipo darasa la Nne,nilikuwa naishi na Mjomba angu ambaye yeye kipindi kile alikuwa ni shabiki wa New Castle United,na alikuwa haipendi Man UTD kishenzi

Mpka Leo Ile nyumba Man UTD nipo peke yangu,kwani wote Kwa sasa wapo Arsenal

Basi bwana dakika ya 25 kama kumbukumbu zipo sahihi Man UTD tukakandwa kimoko,dah


Kipindi Cha pili wapi,Mjomba angu akaanza kunicheka kinafiki,kuwa nashangilia timu mbovu,na kuumbuka kipindi Man UTD tushabeba FA,Ligi na kama tungeshinda UEFA tungekuwa tumeshinda Treble

Basi bwana kufika dakika ya 85 Mjomba akanifukuza NIKALALE,aiseeeee sijawahi kulia kama siku ileeee,

Na ndiyo mara ya kwanza nalia Kwa ajili ya timu ya mpira,dah nikalala usingizi wa mang'amung'amu,Ile naamuka asubuhi nikiwa nanyata nikaenda nikawasha ITV kuwahi matangazo ya BBC asubuhi


Lahaulaaaaaa,man UTD bingwa aisee nilirukaruka mpaka Mjomba akaja akanitoa baru niende shule,usiku ule nikavizia habari za michezo za ITV Ili niyaone Yale magori mawili ya Beckam na Sheringham

Sitaisahua Ile fainali
 
Hii siku sitaisahau nilikua naumwa homa enzi hizo Niko Ilongero sec school hahhhahh.. kuna PCB mmoja alikua anashangilia Sana alikua ni nyumbu...
Aisee kun Aguero alipofunga Goli jamaa alilia Sana.. dah pole Sana Samweli [emoji23][emoji1787]
 
mastory ya mtaani ni kuwa wakati wanakwenda mapumziko, huku wakiongoza bao 5 nadhani, kocha Joachim Low akawaambia wachezaji wake, tusiwadhalilishe tena Brazil, hivyo tujitahidi kumiliki mpira ila tusitamani tena kufunga.

Kumbe wakati wanaambiwa hivyo wachezaji wa reserve wao hawakuwepo pale kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Walikuwa uwanjani wakipasha. Na mmoja wa wachezaji wa reserve alikuwepo Andre Schurrle.

Kocha akamuingiza Andre Schurrle kipindi cha pili, bila kujua maelekezo ya kocha akapiga goli zake mbili za haraka haraka🤣🤣
 
Huyo dinho amewahi kuwafunga chelsea goal in uefa mpaka Jim beglin aliishia kusema

"what a goalll, Peter cech, Peter cech never move"
 
Aaahaaaaa

Ule mwaka wabrazili walikuwa na uzi mkali kishenziiiii

Nakumbuka mshahara ulupotoka fasta nikaenda Bukoba Mjini kuutungua

Baada ya kutungulia Saba na wajarumani ukawa mzito kuuvaaa,nikawa namwachia wife auvae
 
Duh naikumbuka hii hatafutika katika kichwa changu

 
Sitasahau haya matukio

1. Ile mechi Liverpool kapigwa 3-0 na AC Milan then Steven Gerrard akaja kuisadia Liverpool kupiga comeback ya hatari mechi ikaisha 3-3... Then Matuta yakaipa Liverpool ubingwa
(Kuanzia siku hiyo nikawa shabiki Lia Lia WA Liverpool)

2. Nani alisema Simba haendi Makundi [emoji16][emoji16]
(Sitaisahau hii siku hakyamungu niliumia sana maana sipendi kelele za makolo)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…